El Salvador yakamata tani 6.6 za cocaine, meli iliyobeba unga ina bendera ya Tanzania!

Tunataka kurudisha pesa zetu tulizokichangia chama wakati wa uchaguzi
 
Sawa msigwa
 
Inawezekana, lakini majuzi mkurugenzi wa kuzuia madawa ya kulevya alikua analalamika kuwa maisha yake yapo hatarini. Jaribu kuwaza kwa unyeti wa nafasi yake lakini anatumiwa meseji za vitisho, TCRA wapo wapi kufatilia hizo namba na kujua wahusika?
Tanzania kwa muda mrefu imekua kituo kikuu cha kusambaza unga unaotoka Nchi nyingi Rais Magufuri alijitahidi sana kutokomeza wauza sembe papa kwa kipindi chake ingawaje kwa sasa naona kama wamerudi na wana nguvu sana na wakiona Tanzania njia ni ngumu walikua wanaitumia Mozambique kupitishia ili ufike SA na kwingineko sasa hivi unashukia hapo hapo Daslm ndio wanapeleka Nchi wanayotaka uende..
 
Si mnasema si ishu kuchukua bendera ya nchi nyingine na kuichomeka kwenye meli yako ili tu uzugie mambo yapite. Labda hiyo meli si ya tanzania wameamua tu kuweka bendera wasishitukiwe
Wahuni sio bendera tu wanafanya na usajiri nadhani online na wanalipia gharama zake kabisa kwa malengo yao unakuta hiyo meli imesajiriwa kama meli ya uvuvi au utafiti baharini ila ndio wasafirisha Sembe..
 
Meli imesajiliwa na nani? Mtu yeyote anaweza kupata bendera ya nchi yoyote anayotaka!
 
Mabeberu hayatupendi ndio maana...!
 
Bendera hutabulisha registration ya hiyo meli(Ensign) imefanyika nchi ipi, kwa hiyo meli iliyokamatwa obviously registration imefanyika TZ.
Kwa wale wazee wenzangu watakuwa wanakumbuka kwenye eighties na nineties meli nyingi zilizokuwa zikikamatwa na contraband goods zilikuwa either na registration za Liberia au Panama.
 
Dipii Welding
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…