Electrical eel samaki anayetoa umeme

Electrical eel samaki anayetoa umeme

Maji yanapitisha umeme(conductor of electricity) ,kwa nini electric eel hajipigi short ya umeme anopojihami na volti 600 za umeme. Kumbuka volti mia sita inakaribia mara tatu volts ya umeme wa nyumbani.

Stumbled upon interesting/funny explanation -not very convincing
uA1JA.png
 
Mkunga aina ya poraquê (Electrophorus electricus) anaweza zalisha volts 650 za umeme. Samaki huyu hutumia umeme kujikinga dhidi ya maadui zake. Anaweza kukua hadi kufikia urefu wa mita 1.8. Anaishi kwenye maji baridi na anapenda mazingira ya tope. Wale wanaoishi kwenye maji chumvi maarufu kama Ibrahimu huzalisha volts220 tu

Makazi ya samaki huyu ni kwenye tope, pigo moja la samaki mkunga linatosha kumfanya mtu akose nguvu na azame majini, akipiga mara tatu ana uwezo wa kumuua mwanadamu

Inasemekana kuwa wale tunawaita chunusi, ni huyu samaki anapompiga shoti mwanadamu na kufanya mtu azame majini na kufa. Na kwa kuwa samaki hawa huishi kwenye tobe, watu wengi wanataja chunusi huwa ni maeneo ya tope ambayo ndio makazi ya mkunga

Samaki huyu ni kiumbe aliyevunja rekodi ya kuzalisha umeme mwingi

Samaki huyu amevunja rekodi ya kuzalisha umeme mwingi kati ya viumbe wote
Mikunga yenye umeme haiui kwa kuzamisha bali pweza ndiye hasa hufanya hivyo. Ukimtibua kwenye eneo lake anaweza kukubana pua macho na midomo kwa kutumia mikia yake ambayo ina suctions nyingi tu. Hukuacha pale unapotulia au anapokuwa umezirai au kufa kwa kukosa pumzi. Maiti ya aina hii ya vifo inaambatana na damu kutoka aidha puani,midomoni na au masikioni.
 
Huyu ni samaki mwenye umeme yani mwili wake unatengeneza umeme wenye nguvu ya volt 600.
Wanapatikana bara la Amerika Kusini.

Kisayansi wanaitwa "Electrophorus electricus" hawa samaki wala nyama yaani carnivores wana urefu wa futi 5-8.

Miili yao imeundwa na organs zipatazo 6000 ambazo ndani yake zina cell ziitwazo "electrocytes" special kwa ajili ya kugenerate umeme ambao hutumika kukamatia prey na kujikinga na predators

Wanaishi kwenye mabwawa na maji katika mito ya amerca kusini na kusambaa pia baadhi ya maeneo Africa katika mito na mabwawa, chakula chao kikuu ni samaki na ndege hawaoni vizuri hvyo muda wa chakula hutoa kama volt kumi kuijua direction ya prey pale atakapopigwa shoti.

Wanaua sana mamba na samaki wengine kwasababu mamba anapokamata hupigwa shoti mfululizo ambapo husababisha kifo hata binadamu pia walishauliwa na hawa samaki kwa kuendelea kumshika wakati wa shoti ambapo hupoozesha mapigo ya moyo.

Uzao wao ni wa tofauti sana na samaki wengine wakati wa kutaga mayai jike hutaga kufikia mayai 17,000 na hutotoa watoto wapatao 1200 na muda wote kiota kinakua kimezungukwa na ulinzi ambao ni mate ya dume.

Wanaishi miaka 10-15
Huyo ndo electrical eel ni samaki ambae hana noma usimpomgusa, sasa mamba hasa hawa alligator hawajui kwamba huyu ni umeme unaotembea mamba akajua msosi umejileta umeona kilichompata? Amekula shoti za kutosha mpka kafa hapo hapo ndani ya sekunde 30 hapo ndio eel katoa volt 600.

Umeme tu wakaida wa volt 220 wa (tanesco) unaua sasa jiulize huu wa samaki ambao ni 600-650 volt inakuaje?

Lakini sehemu za brazili wanamla ila wanamuua na kumuacha baada ya masaa nane. UKISKIA mtu kakaushwa damu na Chunusi anakuwa si Chunusi bali samaki huyu mwenye umeme wa kutisha.

FB_IMG_1667374083290.jpg
 
Umeme tu wakaida wa volt 220 wa (tanesco) unaua sasa jiulize huu wa samaki ambao ni 600-650 volt inakuaje??
Umeme wa tanesco unawezaua cuz ni wa 'muendelezo'

Wa huyo samaki ni waku-stun (ku shock, sawa na zile mosquito racket ) , siyo wa kuua
 
Umeme wa tanesco unawezaua cuz ni wa 'muendelezo'

Wa huyo samaki ni waku-stun (ku shock, sawa na zile mosquito racket ) , siyo wa kuua
kwahiyo huyo mamba alivyotaka kumla huyo samaki hakufa sio kwasababu sio umeme wa Tanesco?
 
kwahiyo huyo mamba alivyotaka kumla huyo samaki hakufa sio kwasababu sio umeme wa Tanesco?
possibly huyo mamba alikufa sababu ya shock ilipelekea ku-drown, siyo sababu alikaushwa na umeme wa huyo kiumbe,

huo umeme haufi, japo ni wa kiwango kikubwa ila una-last kwa mda mchache sana, tofauti na wa tanesco

zile mosquito racket/zapper, defibrillator, electric fence, etc, zinafanya kazi sawa na umeme wa huyo kadudu
 
Back
Top Bottom