Kuna haja utafiti kufanyika kujua kama kovid tunayoambiwa tujikinge kwa barakoa, sanitizer na kunawa mikono ndio njia sahihi ya kupunguza maambukizi?
Je? Kwa namna gani chanjo inasaidia kupunguza madhara na maambukizi ya kovid?
Je? Tubadili namna ya kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi au tubaki na zilezile za awali?
Mwisho, kutafuta namna ya kupunguza hofu na wasiwasi, hofu inaweza kuleta madhara makubwa kuliko hata ugonjwa wenyewe.
Mkuu 'Monk'
Ngoja mimi nikusaidie kwa kifupi tu kujibu maswali yako uliyoweka hapa. Nikipata nafasi nzuri nitaandika mahali kwingine kwa kirefu zaidi ya hapa.
1. Kunawa mikono, kujipaka sanitizer, kuvaa barakoa, na kujitenga kwa umbali kiasi katika mikusanyiko ya watu na mengine ambayo hukuyaorodhesha, utafiti juu ya mambo hayo kupunguza kuenea kwa maambukizi, siyo kwa COVID-19 pekee, bali kwa magonjwa mengine ya milipuko, ulishafanyika miaka mingi sana na unaendelea kufanyika hadi leo hii na ugonjwa mpya kama huu.
Hizo ni njia sahihi kabisa zilizokwishathibitishwa kwamba zinapunguza milipuko.
KUZUIA KUENEA? -Hii inategemea na jinsi watu walivyoelimishwa katika kujikinga kwa kutumia njia hizo. Ni vigumu sana, na hata haiwezekani kila raia afanye kama inavyotakiwa kila mara ili aweze kujikinga kwa njia hizo.
2. Je, ni kwa namna gani chanjo inasaidia kupunguza madhara na maambukizi ya COVID-19?
Chanjo haizuii maambukizi. Inachofanya chanjo ni kupunguza madhara ya covid-19 ndani ya mwili wa mtu aliyechanjwa. Imekwishathibitishwa sasa bila ya shaka yoyote kwamba watu waliopata chanjo wakiambukizwa na COVID-19, na hata hii mpya ya Delta, watu hao hawaugui kiasi kikubwa kama wale wanaoambukizwa wakiwa hawajapata chanjo. Wengi wa wanaolazwa hospitalini sasa hivi kutokana na maabukizi ya corona ni wale ambao hawakupata chanjo kabisa. Na wanaokufa kwa wingi sasa hivi ni wale ambao hawakuwahi kupata chanjo.
Haya ni matokeo ya tafiti zinazoendelea hadi sasa. Matokeo ni bayana kabisa na wala hayana mkanganyiko juu yake.
Kwa hiyo, chanjo ya COVI-19,
Haizuii mtu aliyechanjwa kuambukizwa ugonjwa wa corona, na yeye akiambukizwa, pia huambukiza wengine anaokuwa nao karibu yake. Bahati yake pekee ni kwamba, anapougua, hawi na hali mbovu zaidi, hata kutolazimika kulazwa hospitalini.
Kwa hiyo CHANJO inapunguza madhara ya ugonjwa kwa yule ambaye amepata chanjo.
3. Je tubadili namna ya kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi au tubaki na zile zile za awali?
Hili swali lako kidogo sikulielewa. Tubadili namna ya kuchukua tahadhari vipi, kwa njia zipi zilizokwishafanyiwa utafiti na kuonekana kwamba zinafaa zaidi ya hizi zilizopo?
Na "zile zile za awali", una maana gani, zile za kujifukiza au? Hapa sikukuelewa kwa kweli.
4. Kutafuta namna ya kupunguza hofu na wasiwasi, hofu inaweza kuleta madhara makubwa kuliko hata ugonjwa wenyewe.
Hii ni 'myth' inayotumiwa kisiasa mkuu wangu 'Monk'.
Kuna hofu zaidi ya kumwona mtu mzima akidondoka barabarani na kufa hapo hapo mbele za watu? Tumshukuru Mungu, kwenye eneo letu hili la Afrika, Mwenyezi katuwekea kinga ambayo hadi sasa haijulikani inatokana na kitu gani juu ya ugonjwa huu.
Hebu piga picha hii kichwani mwako.
Hapo kijijini kwenu nusu ya wakazi wake wapate maambukizi ya nguvu, na dispensari na zahanati zilizopo, pamoja na hospitali ya Wilaya hazina uwezo wa kuwahudumia watu hao. Kama kuna mtungi mmoja wa hewa ya Oksijeni, wagombee watu 20 au zaidi. Kuna hofu zaidi ya hapo?
Mungu wetu ni mkubwa, pengine kwa kudra zake tu atatuepusha na madhira ya aina hii yasitokee kamwe. Lakini hilo sio liwe mbadala wa sayansi na kufanya mambo kwa uhakika unaojulikana.
Ngoja nikuachie hapa.