ELIMU: Gari yenye Cc 650 kutumia mafuta kuliko gari yenye Cc 1300

Mkuu uko sahihi, mleta maada anajaribu kupotosha watu makusudi au hajui anachoongea.
 
kwa mfano bmw mini cooper.kina cc chache halafu dashbord inasoma 240km.

hapa lazima kuna umwagaji wa tui.
Gari inaendeshwa na msukumo wa pistons ambazo zinasukumwa na mlipuko kati ya oxygen na mafuta. Ili iwe na nguvu inabidi msukumo huu uwe mkubwa. Je msukumo(mlipuko) huu unakuwaje mkubwa?
1. kuwa na cc nyingi :mfano kila carina ya 1.8 itakuwa na nguvu kuliko carina ya 1.6
2.kuongeza mafuta na oxygen kwenye combustion chamber. hii hufanywa kwa kuweka turbo charger au super charger. maanake ni kuwa gari ya cc2000 yenye turbo inakuwa na nguvu kuliko gari ya cc2000 isiyo na turbo. Na usishangae gari ya cc2000 yenye turbo inakuwa na nguvu kuliko gari ya cc2500 isiyo na turbo
 
Huwa nasikitika sana nikiona mtu ni dereva by profession halafu hana clue ya vitu vidogo. Huo umeme unazalishwa na nini? Kuna generator humo au ? Gari za sasa hivi zina effiency nzuri kwenye mafuta kutokana na kukuwa kwa teknolojia. Gari inaweza kuwa cc4500 hybrid maanake ina electric motor inayotumika wakati gari iko kwenye mwendo mdogo kwahio mafuta hayaendi kabisa.
 
Kweli
 
Alichikiongea jamaa ni sahihi ila amefanya misconception katika kupresent.

Miaka ya nyuma mifumo ya fuel injection ilikuwa ni full mechanical ambapo kwa sehemu kubwa walikuwa wanatumia Carburator. Kiasi kikubwa cha mafuta kilikuwa kinapotelea kwenye carburator hivyo hata kama gari ina Engine capacity ndogo lazima ionekane inakula mafuta.

Recently umekuja mfumo wa Electronic fuel Injection (EFI). Huu ni mfumo ambao ni computerized yaani unauwa na sensors, actuators na ECU. Ni mfumo wa injection ambao una efficiency kubwa sababu mafuta na hewa vitaingia kwenye engine katika amount ambayo inahitajika tu.

Kwa maelezo hayo siyo kitu cha ajabu kukuta gari ya cc 1000 ambayo ni inatumia carburator inakula mafuta zaidi au sawa na gari ya 1400cc ambayo inatumia EFI.

Nadhani nimeeleweka.
 
Uko sahihi. Lakini kwa sasa hivi na gari alizotaja hamna ambayo sio EFI.
 
Wewe nawe unachanganya watu. Kama gari siyo hybrid basi nguvu ya kuendesha gari inatoka kwenye Engine.

Ila gari ambalo mifumo yake ni mechanical linakula mafuta zaidi ukicompare na gari ambalo mifumo yake ni electronic. Assume hizo gari zote mbili zinafana vitu vyote except mifumo ya kuinject mafuta
 
Nakuunga mkono,ziko gari cc kubwa ila consumption ndogo,ila pia kuna factors nyingi zinachangia ulaji wa mafuta mfano mzigo,matairi e.g upana,upepo mdogo n.k,ukanyagaji wa mafuta,ukubwa wa gari,service,land terrain,upepo,matumizi ya AC,gear unayotembelea n.k...
 
ndio boss. passo na raum haswa raum ni nzuri kwa mafuta na inatunza thamni ya pesa yako na pia unaweza kwendea safari ndefu ya kati
 
Samahani kwa kuchelewa kujibu boss.

Gari hizo ni kama vile Toyota Passo, Vitz, Porte, Ractis, Nissan Note, Toyota Bb, Fun Cargo, Sienta, Platz, Raum na Mitsubish zenye Cc chini ya 1400 zenye injini ya GDi.
 
Mimi naomba sifa za Suzuki carry tofauti
Bei
Ubora
Mafuta
Suzuki Carry kwa kuagiza inafika kwa 8m, ni gari ndogo kwa ajili ya shughuli ndogo ndogo za ubebaji mizigo, haihitaji mzigo mzito kwa kua pia chasis yake ni rahisi kukatika na haihitaji njia mbovu sana kwa kua inawahi kuchoka na hata kuua turbo kwa zile zenye turbo na pia huweza kuharibu gia box na 4while yake mapema iwapo inatumika sana njia mbovu.

Hii ni kwa mizigo ya mjini mjini, ukizingatia service inakaa japo haina maisha marefu sana kama ilivyo kwa toyota hilux, kwa mafuta sio mbaya maana lita moja huenda wastani wa km 18 mpaka 21.
 
Acha kututia moyo, gari unanunua milioni 3 lakini hadi unaitoa port ni 14m, si mambo ya ajabu haya?
Kwa kweli ushuru uko juu. Muhim sana kabla hujaamua kuagiza gari flani uhakikishe umeipigia hesabu vizuri ili isije kukusumbua kwenye ushuru. Faham ushuru kabla ya kuagiza
 
Shukrani kwa mfano huo hai kabisa. Technolojia imebadirika na kwa gari za hybrid mafuta ni kidogo zaidi.
 
Shukrani boss
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…