ndio maana waswahili husema ujana maji ya moto. Utumie vizuri kuepuka majuto na maumivu moyoni baadae.
Mzee ana mawazo mazuri sana. Lakini pia kama haridhiki na mawazo na uwezo wa kujieleza na kuhoji wa vijana wanaohitimu vyuo vikuu kwasababu hakuna mijadala hilo ni tatizo lake binafsi. Lakini vijana wa sasa wana ujuzi, umahiri na uwezo mkubwa sana wa kujieleza na kuhoji mambo.
Na mimi binafsi na mpa pole sana generali kama jambo hilo linamkwaza. Mambo yanabadilika wakati wake uliisha, awape fursa vijana wajiandalie kesho yao kulingana na mazingira yao yaliopo.
Vijana wanaohitimu vyuo vikuu mbalimbali nchini. Wanaohitimu na kutoka na maarifa, ujuzi na umahiri mkubwa sana wa kadre mbalimbali na wanasonga mbele kwa furaha na mikogo kama yote ama hamuhudhuriagi graduations, wameridhika na kwakweli inaridhisha na kutia moyo sana.
Babu jenerali tunampenda na tunamuheshimu sana. Anajaribu kufundisha na kuichochea jamii ya hususani ya wasomi ujasiri wa kubeza kama ilivyo hulka yake. Umri wake umesonga kidogo ni vigumu vijana kumuunga mkono kwenye pendekezo lake. Nashukuru vijana na wasomi makini wamekua wakimpuuzia kisomi zaidi ,Mzee wetu huyu ambae tunaempenda sana asijiskie vibaya, na kwakweli wamefanikiwa pakubwa na mambo yanasonga vizuri...
Mawazo yake mazuri ikiwa yanafaa basi atathiminiwe na yatekelezwe na vyuo husika kwa wakati wana ona unafaa na kama jambo lenyewe linamanufaa.
Ana uhuru wa kutoa maoni, kukosoa, kupendekeza mambo yawe vipi ili tusonge mbele kama Taifa, ila nia yake ya ndani inafahamika vizur sana muda mrefu. Na kwahivyo hasira na ghadhabu ndani ya maoni mazuri sana ya generali ulimwengu vinafahamika sio jambo geni humu nchini.
Maoni yangu kwenye pendekezo na na maoni juu ya mijadala.
Mijadala mbalimbali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi iendeshwe na vyama vya kisiasa, kupitia jumuiya zake mathalani jumuiya za vijana, wanawake, wazazi, chipukizi n.k ili kuwajengea vijana uwezo wa kujieleza na kuhoji, ikiwa hilo ndio tatizo kama anavyodai Mzee general ulimwengu.
Platforms za mijadala ni nyingi mno si vyuo vikuu tu.
Kwako
Tindo