Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
umepanic gentleman 🤣Kila mwanasiasa ni tapeli , nakuonea huruma dogo bado hujajitambua utakufa maskini kwa uchawa wa siasa...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
umepanic gentleman 🤣Kila mwanasiasa ni tapeli , nakuonea huruma dogo bado hujajitambua utakufa maskini kwa uchawa wa siasa...
Waambie Bagonza na Jenerali Ulimwengu kwamba wao ni mfano mzuri wa waliyoyaandika. Kwamba baada ya kumaliza chuo kikuu walienda kuua elimu kuanzia ya msingi na kuendelea kama wanavyodai kwani wao walimaliza mapema. Ikitokea kuwajibishwa wao ndio wa kwanza. Mkumbushe Jenerali Ulimwengu kwamba Joseph Sinde Warioba na yeye walipigwa/walichapwa bakora Ikulu na mwalimu Nyerere kwa kauli kama hizo, hivyo asisahau.Inasikitisha sana.
Sahihi kabisa😂😂Hapo umewashika ni hao hao maprofessor na wapiga dili ,sisi ilikuwa ukitaka kitini nenda stationary fulani hapo tunajaaa watu nyomi.
Hao waliopata elimu mwanzo mmoja wapo ndio huyo Ulimwengu wao ndio wameharibu elimu kwa tamaa zao ,kwa vile hawana uwezo zaidi ya kujua kingereza.
Zile handouts ukisoma sana unafaulu kwa alama za juu ila hamna kitu utafnya ukija kweny uhalisia mambo ni mengi.
Upo sahihi, mimi siku nikisikia vitini vimepigwa marufuku vyuoni kote nchini nitafurahi sana. Hiyo italazimisha wanafunzi kutafuta rejea hasa kupitia Google scholars, Amazon, etc etcHiyo Elimu ya Tz inahitaji kuijiongeza hata hao waliosoma zamani walikuwa wanajisomea vitabu kutoka Sehemu na sio kutegemea maarifa ya mwalimu tu.
Hamna Cha werevu, Bali wamepata ulemavu wa woga. Tunaona kinachofanyika huko vyuoni toka kwa watawala wanaolazimisha kupandikiza woga na nidhamu za kinafiki. Hayo ni baadhi ya madhara ya chama kulazimisha kubaki madarakani kwa shuruti, ni lazima waue uwezo wa wanafunzi kujieleza kwa uhuru.hawaambii anawabeza kwa kebehi na madharau wao, walezi na wazazi wao.
Wajukuu waerevu wamechanuka, wako rada, wamestukia janja janja ya Babu
Ni wapi Askofu Bagonza na Jenerali ulimwengu wamewahi kuwa policy makers Wa nchi hii?! Angalau Jenerali nasikia aliwahi kuwa Mbunge, lakini siyo Bagonza. Kwa hiyo hizo lawama zako haiwahusu.Waambie Bagonza na Jenerali Ulimwengu kwamba wao ni mfano mzuri wa waliyoyaandika. Kwamba baada ya kumaliza chuo kikuu walienda kuua elimu kuanzia ya msingi na kuendelea kama wanavyodai kwani wao walimaliza mapema. Ikitokea kuwajibishwa wao ndio wa kwanza. Mkumbushe Jenerali Ulimwengu kwamba Joseph Sinde Warioba na yeye walipigwa/walichapwa bakora Ikulu na mwalimu Nyerere kwa kauli kama hizo, hivyo asisahau.
Kadri vyuo vikuu/nchi inavyozalisha wajinga/machawa ndivyo ccm wanashangilia maana kudumu kwao madarakani kunakuwa na uhakika. Uzalishaji wa machawa/wajinga ni mkakati wa muda mrefu wa ccm ili waendelee kutawala.ELIMU ILIFIA CHUO KIKUU au ILIZIKWA CHUO KIKUU?
Imeandikwa na ASKOFU BAGONZA
Mzee Jenerali Ulimwengu kasema vyuo vikuu vyetu ni kama Extended High School. Anayebishi anitafute. Sababu ni nyingi kama idadi ya wajinga wetu waliosoma vyuo vikuu.
1. Tulipokuwa na Chuo Kikuu kimoja, tulifuta ujinga kwa asilimia 85. Sasa tuna vyuo vikuu zaidi ya 50, tuna wajinga wengi mitaani na maofisini kuliko enzi ya chuo kikuu kimoja.
2. Vyuo vilitengeneza wanasiasa na viongozi makini. Waliposhika madaraka wakapiga marufuku mijadala ya kisiasa na kijamii katika vyuo vikuu.
3. Wakati ule wanafunzi wa vyuo vikuu waliwahoji watawala, siku hizi watawala wanawahoji wanafunzi wa vyuo vikuu.
4. Vyuo vikuu vilizalisha wachambuzi na watafiti. Siku hizi vinazalisha ma-chawa na wapiga debe. Hata mbunge mwenye darasa la saba anaajiri wapiga debe kutoka chuo kikuu. Nampongeza.
5. Kuna tofauti ndogo inayotenganisha uchawa na ujinga. Wote wanazalishwa katika vyuo vikuu. Mmoja anaishi ofisini na mwingine anaishi mitaani akiunga mkono asiyoyajua.
6. Elimu ya wakati ule ilichochea uasi mtakatifu (holy rebellion). Hii ya sasa inachochea woga na utii usiomnufaisha anayetii.
Nini kilitokea?
Waliohitimu chuo kikuu walienda kuua elimu kuanzia shule za msingi. Vyuo vikuu vikageuka kuwa mhanga wa mafanikio yake. Kwa hiyo elimu ilifia chuo kikuu na kuzikwa chuo kikuu.Shule za Msingi na sekondari ni vitalu vya uzalishaji unaoenda kukuzwa chuo kikuu.
View attachment 2822820
Je huoni huyu mwanzilisha wa jf kafanya la maana kuanzia hili jukwaa na anafaa kupewa pongezi, huu ndio usomi ndio maana mwanzilisha wa Facebook alipata Phd kutokana na ubunifu zake.
Yule mzee ni educational ego han cha maana na hana mchango zaidi ya lopo lopo ....Kila siku kuona wenzie wajinga ila hana cha maana amefanya na elimu ya kizamani.
usijiskie vibaya kukosa kuungwa mkono kwa ushawishi wa hoja zako au upande wako. Acha watu wawe huru, na haina haja kumbeza alie na wazo tofauti na lako na kuanza kusingizia vitu hata visivyo na maana.Hamna Cha werevu, Bali wamepata ulemavu wa woga. Tunaona kinachofanyika huko vyuoni toka kwa watawala wanaolazimisha kupandikiza woga na nidhamu za kinafiki. Hayo ni baadhi ya madhara ya chama kulazimisha kubaki madarakani kwa shuruti, ni lazima waue uwezo wa wanafunzi kujieleza kwa uhuru.
Sioni shida ww ukipinga asemacho huyo mzee, maana ww ni zao la walemavu asemao huyo mzee kutoka kwenye elimu yetu. Inshort ww ni muhanga wa ukweli wa huyo mzee.
🤣umepanic Kinyungu relax banaKadri vyuo vikuu/nchi inavyozalisha wajinga/machawa ndivyo ccm wanashangilia maana kudumu kwao madarakani kunakuwa na uhakika. Uzalishaji wa machawa/wajinga ni mkakati wa muda mrefu wa ccm ili waendelee kutawala.
Hii nchi lazima tutafute ukombozi mara ya pili kwa kuing'oa ccm, maana hata ile hatua kidogo ya kujitambua tuliyokuwa tumeifikia ccm wamefanya kila mbinu kuirudisha nyuma
Mkuu hakuna anayefaidia na ujinga wa watz zaidi ya ccm.🤣umepanic Kinyungu relax bana
the impact ya CCM into you, saikolojikali na spiritually inaelekea kukufanya hata ukijikwaa barabarani pekeyako utasema ni CCM wamesababisha ujikwae
kwahiyo akina kitila wamekuacha unalalama tu bila kuchukua hata hatua?Mkuu hakuna anayefaidia na ujinga wa watz zaidi ya ccm.
Ukitaka kujua angalia watu waliokuwa timamu kabisa kama Kitila, Kabudi, walipoingia ccm wamekuwaje? Wamekana hadi vitu vya msingi kabisa walivyokuwa wakipigania.
Haishangazi Ulimwengu anasema vyuo vikuu vimekuwa sawa na extension ya form six. Unajua kwa nini? Ni kwa sababu kwenye vyuo vyetu hautakiwi kupingana na mawazo ya serikali, ya chama na hata ya walimu wako. Wamekuwa kama wanazalisha mazombie
Wala sihitaji kuungwa mkono na watu ambao tayari ni zao la elimu ya woga, na Sasa uchawa. Nimeunga mkono ukweli wa Ulimwengu. Na Sina sababu ya kuacha kuunga mkono ukweli huo wakati dhahiri naliona tatizo.usijiskie vibaya kukosa kuungwa mkono kwa ushawishi wa hoja zako au upande wako. Acha watu wawe huru, na haina haja kumbeza alie na wazo tofauti na lako na kuanza kusingizia vitu hata visivyo na maana.
Hoa vijana wasomi wa vyuo unaowaita waoga, wahanga, walemavu na waoga wenye nidhamu za kinafiki nikuhakikishie wako chonjo, wako makini na wako rada mbaya sana. Wanajitambua vizuri sana. Hawawezi kuwa driven mathalani kwa hoja kama zako Tindo, coz its full of mihemko na negativity. Hayupo wa kujisumbua kuambatana na wewe. Vijana hawa wataendelea kuunga mkono upande ambao akuna kejeli wala mabezo.
Na uzuri ni kwamba vijana hawa wametulia tuli, mentally na saikolojikali, hawana papara wala hawabughudhiwi na dhihaka,dharau na mihemko yenu wanasonga mbele vizuri sana na kuwaunga mkono wale wanowaskiliza na kuwaelekeza kwa heshima, utu, upendo na ungwana.
Nyie kuna engo wanawasubiria tu ili wawaadhibu na kuwanyorosha vizuri sana mpaka mseme yote, mtukane matusi yote na mihemko yote iwatoke ili hatimae akili ziwakae sawa na muwe na heshima, utu na nidhamu kwa wasio waunga mkono.
Sasa Hv kuna vitabu vya kijinga vitupu vimetamalaki hakuna maarifa tena na ni kweli vyuo vikuu vinasikitisha sana,Taifa linakoelekea Sijui tuombe MUNGU atunusuru.ELIMU ILIFIA CHUO KIKUU au ILIZIKWA CHUO KIKUU?
Imeandikwa na ASKOFU BAGONZA
Mzee Jenerali Ulimwengu kasema vyuo vikuu vyetu ni kama Extended High School. Anayebishi anitafute. Sababu ni nyingi kama idadi ya wajinga wetu waliosoma vyuo vikuu.
1. Tulipokuwa na Chuo Kikuu kimoja, tulifuta ujinga kwa asilimia 85. Sasa tuna vyuo vikuu zaidi ya 50, tuna wajinga wengi mitaani na maofisini kuliko enzi ya chuo kikuu kimoja.
2. Vyuo vilitengeneza wanasiasa na viongozi makini. Waliposhika madaraka wakapiga marufuku mijadala ya kisiasa na kijamii katika vyuo vikuu.
3. Wakati ule wanafunzi wa vyuo vikuu waliwahoji watawala, siku hizi watawala wanawahoji wanafunzi wa vyuo vikuu.
4. Vyuo vikuu vilizalisha wachambuzi na watafiti. Siku hizi vinazalisha ma-chawa na wapiga debe. Hata mbunge mwenye darasa la saba anaajiri wapiga debe kutoka chuo kikuu. Nampongeza.
5. Kuna tofauti ndogo inayotenganisha uchawa na ujinga. Wote wanazalishwa katika vyuo vikuu. Mmoja anaishi ofisini na mwingine anaishi mitaani akiunga mkono asiyoyajua.
6. Elimu ya wakati ule ilichochea uasi mtakatifu (holy rebellion). Hii ya sasa inachochea woga na utii usiomnufaisha anayetii.
Nini kilitokea?
Waliohitimu chuo kikuu walienda kuua elimu kuanzia shule za msingi. Vyuo vikuu vikageuka kuwa mhanga wa mafanikio yake. Kwa hiyo elimu ilifia chuo kikuu na kuzikwa chuo kikuu.Shule za Msingi na sekondari ni vitalu vya uzalishaji unaoenda kukuzwa chuo kikuu.
View attachment 2822820
basi sawa,Wala sihitaji kuungwa mkono na watu ambao tayari ni zao la elimu ya woga, na Sasa uchawa. Nimeunga mkono ukweli wa Ulimwengu. Na Sina sababu ya kuacha kuunga mkono ukweli huo wakati dhahiri naliona tatizo.
Hakuna kijana utasema Yuko chonjo kwenye mazingira ambayo tayari mfumo umeshaundwa kuaccomodate waoga, na akitokea yoyate anayetaka kuhoji mazingira hayo ni lazima apoteze nafasi yake ya masomo. Yaani mfumo wetu wa elimu huko vyuoni ni rafiki kwa wasio na uwezo wa kuhoji mambo ya msingi. Ili uwe salama kwenye elimu yako ni lazima kuwa kondoo. Na ukondoo kwenu chawa ni dalili ya utulivu na uelewa.
Wanasubiri watuadhibu wapi boss, kungekuwa na mazingira ya kweli ya kuadhibiana ungeona matokeo ambayo ingekuwa fedheha kwenu vibaraka wa watawala, na mnaoawasujudu. Sio ule upuuzi ambao vyombo vya Dola vinaona fahari kutumika kulinda mabox ya kura za wizi.
🫡6. Elimu ya wakati ule ilichochea uasi mtakatifu (holy rebellion). Hii ya sasa inachochea woga na utii usiomnufaisha anayetii.
Mkuu tupo kwenye mjadala kuhusu mada nyeti (seroius). Kwahivyo rejea tena kusoma hili bandiko, halafu rudi tujadili seroiusly. Madai ya Bagonza na Ulimwengu ni very serious na hivyo tujadili seriously.Waambie Bagonza na Jenerali Ulimwengu kwamba wao ni mfano mzuri wa waliyoyaandika. Kwamba baada ya kumaliza chuo kikuu walienda kuua elimu kuanzia ya msingi na kuendelea kama wanavyodai kwani wao walimaliza mapema. Ikitokea kuwajibishwa wao ndio wa kwanza. Mkumbushe Jenerali Ulimwengu kwamba Joseph Sinde Warioba na yeye walipigwa/walichapwa bakora Ikulu na mwalimu Nyerere kwa kauli kama hizo, hivyo asisahau.