Elimu kwa Umma: Maswali na Majibu kuhusu Safari za Ndege na Changamoto zake

Wananikera kufika eapot mapema, ndege inaondoka saa tisa wananambia nifike saa nane, pili kwa uwanja wa zamani kwa hapa kwetu wanakagua mara mbili (temino 2) ila kule mbeya nilikaguliwa mara moja tu
Tumia terminal III(Ila usiwe unaenda chato na the like, safiri kwenda duniani), ukaguzi rasmi wa kale ka scanner kao ni mara moja tu lakini jiandae kwa usumbufu wa kabla ya safari kama wa kuchokonolewa puani wakitafuta corona na ishu za passport na visa [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mkuu safari za ndani passport ya nini kama una kitambulisho na wewe ni Raia?
 
Mala nyingi ndege hulipuka na kuua abiria pale tu inapopata hitilafu huko juu,.. sijawahi kusikia abiria wameruka Kwa parachuti au miamvuli unaweza kututoa hofu hapo?
Hata mimi nimeshangaa sana kuhusu parachute aisee
 
Mkuu Samahani kama nakukwaza lakini hakuna shirika na ndege linalotaka uwe na passport kwa safari za ndani hasa hapa nazungumzia nchi ya Tanzania. Kama lipo nitajie please, labda kama takwa hili limeanza two months ago. Ukiwa na kitambulisho hata driving license inatosha.
 
Ni kweli kwenye safari ndefu kuna wakati marubani huwa wanauchapa usingizi, ndege ikabaki inajiongoza peke yake
Dhana ya ndege kujiongoza yenyewe (auto pilot) huwa inaeleweka vibaya.

Ni kweli kuna huo mfumo ambapo unapotumika rubani hatumii nguvu kubwa (manual operation) kuendesha ndege, lakini haina maana kwamba mfumo unaweza kujitegemea wenyewe kiasi cha marubani kulala usingizi na safari ikawa shwari.

Asante.
 
Bila samahani mkuu.

Hizi taratibu si lazima ziwe applicable Tanzania pekee, tunachoeleza kwenye majibu yetu ni kuwa baadhi ya taratibu zinatofautiana nchi kwa nchi au shirika la ndege kwa shirika la ndege.

Hata kwa Tanzania, inapotokea huna ID nyingine basi Passport inaruhusiwa kutumika kama nyaraka itakayokuwezesha kutumia usafiri wa Anga.
 
Hati ya kusafiria( passport) kwanini lazima uwe nayo hata kwa safari za ndani ya nchi?
Kama tulivyoeleza kwenye majibu hapo juu, sio lazima kwa safari za ndani ya nchi bali huweza kutumika pale unapokosa ID nyingine zinazokubalika zikiwemo leseni ya udereva, kitambulisho cha taifa n.k.
 
Majibu na maelezo yetu kuhusu usafiri wa anga ni jumuishi na tunayaweka kwenye kapu moja. Pengine ndio sababu za mkanganyiko huu.

Hoja yako ni sahihi kuhusu parachutes.

Asante.
 
Mkuu mnadili na tiketi tu au hata taratibu za kupata visa ya nchi fulani mnaweza kusaidia?
 
Unaelezea vipi usalama wa ndege hasa zile za masafa marefu kuvuka bahari.
Hii barafu ingemfaa sana
Kuna utaratibu upi unaozuia ndege zisigongane angani
mnamvuruga mtoa mada, yeye maelezo yake ni kupata tiketi kwa urahisi na jinsi ya kufanya unapofika airport na hadi unapanda kwenye ndege basi lakini watu tunauliza tecnical issues
 
Nyie ni independent institution sasa kama hamtanichaji kwa kunisaidia kupata tiketi kwa urahisi na gharama nafuu nyie mnafaidika vipi?
 
ATCL wana utaratibu ukikata mapema bei inapungua?
 
Nimekupata mkuu kama mnazungumzia utaratibu wa kidunia, mwanzo nilifikiri unazungumzia Tanzania. Big up kwa majibu murua.
 
Mkuu mnadili na tiketi tu au hata taratibu za kupata visa ya nchi fulani mnaweza kusaidia?

Asante kwa kuuliza mkuu.

Tunahusika na tiketi, visa processing, accommodation, usafiri kutoka Airport (cab) na kwa wasafiri wanaokuja nchini tuna baadhi ya maeneo tunaweza kuwaandalia kwenda kutalii kama watahitaji.

Kwahiyo jibu ni ndiyo, tunatoa huduma ya kumsaidia abiria kupata visa ya nchi yoyote.
 
Nyie ni independent institution sasa kama hamtanichaji kwa kunisaidia kupata tiketi kwa urahisi na gharama nafuu nyie mnafaidika vipi?

Swali zuri na tulilitarajia. Tunaamini wengi watakuwa wamejiuliza hivi pia. Tunaomba tujibu hapa kwa ujumla.

Kama tulivyoeleza awali kwenye baadhi ya majibu huko juu, sisi tuna ushirikiano wa kibiashara na makampuni ya ndege ya ndani na nje ya nchi, hivyo tunapofanya nao biashara kuna makubaliano ya malipo ambayo wanalazimika kutulipa kwa kuwarahisishia kupata wateja.

Si hivyo tu, kuna hotels na makampuni ya usafirishaji na utalii pia ambayo tunapofanikisha huduma za accommodation, transportation na tour traveling, nao hutulipa kwa wateja wanaofika kwao kupitia sisi.

Hivyo, hatuoni sababu ya kumcharge abiria/mteja kama makampuni mengine mengi ya uwakala yanavyofanya.

Asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…