SoC02 Elimu kwa Watoto wenye Usonji na kujua namna ya kuwasaidia

SoC02 Elimu kwa Watoto wenye Usonji na kujua namna ya kuwasaidia

Stories of Change - 2022 Competition

Erenestina Ernest

New Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
2
Reaction score
6
JamiiForums

UTANGULIZI.
Asilimia kubwa ya jamii inayotuzunguka imekuwa na uelewa mdogo juu ya watoto wenye usonji hivyo kupelekea watoto kunyanyasika na kutojua haki zao na pia kutopewa kipaumbele katika nyanja mbalimbali Kama upande wa afya na elimu pia.

MAANA YA USONJI/AUTISM.
Ni Changamoto inayompata mtoto katika kipindi Cha ukuaji hasahasa uathiri milango yake ya fahamu.
Utaweza kumtambua mtoto mwenye usonji kuanzia umri wa miaka miwili(2).
Mtoto mwenye usonji mara nying uelewa wake uko taratibu tofauti na watoto wengine wenye umri sawa na wake.
Tarehe 2 mwezi wa 4 ni siku ya usonji duniani ivyo elimu utolewa zaidi katika jamii ili kuweza kubadili mitazamo hasi kwa watoto wenye changamoto iyo.

DALILI ZA USONJI.
Zifuatazo ni baadhi ya dalili za mtoto mwenye usonji na mpaka inafikia hatua ya kusema uyu mtoto ana tatizo la usonji walau awe na dalili kuanzia 3 ambazo ni
•Kupenda kujitenga na wenzake
•Kuchelewa kupokea taarifa.
•Kupenda kurudia rudia maneno kwa mfano;(Amina naomba iyo sabuni)nae anarudia jinsi ulivyotamka.
•Kuwa mtukutu Sana.
•Kukosa utulivu
•Baadhi yao ni wakimya Sana.
•Kupenda kulia uku anajidhuru mwenyew.
•Kujipiga ukutani na kujijeruhi.
•Wakipenda kitu hawana kipimo mfano kula,kuoga nk
•Kuwa na hasira Sana .
•Mawasiliano yao mara nyingi ni ya vitendo zaidi(lugha) n.k

JINSI YA KUWASAIDIA.
•Wanahitaji upendo na kusikilizwa kwa kila wakati anaokuw anakuhitaji.

•Hakikisha kila kitu unachotaka kumfundisha iwe mkono kwa mkono(hand to hand)

•Hakikisha ukiwa unamfundisha kitu chochote kile iwe ni hatua kwa hatua kwa mfano;unataka kumfundisha mtoto kupiga mswaki, hatua

~Kuwa na utambuzi wa kujua huu ni mswaki na hii ni dawa
~Kushika mswaki na dawa
~kuchukua mswaki na dawa.
~Kufungu dawa ya meno
~Kuweka dawa ya meno kwenye mswaki
~Kuanza kupiga mswaki,juu chini kushoto kulia na ulimi

Izo Ni baadhi ya hatua kwa kitu ambazo unataka kumfundisha hakikisha na kesho unamfundisha ivyo ivyo kama ulivyofanya Jana sababu ni wepesi kusahau.

~Mzazi/mlezi hakikisha unaelewa ishara za mwanao katika hatua ya kutaka kujitegemea yeye mwenyew mfano kwenda msalani.
~Wanahitaji kusikilizwa na kuzijua lugha zao za ishara.

MATIBABU.
Mpaka Sasa hakuna dawa maalumu ambayo mtoto mwenye usonji anaweza kupewa na akapona bali Kuna vitu vya kufanya ili kumsaidia kupiga hatua kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

MAPENDEKEZO
•Tusiwabague watoto kutokana na hali zao,watoto wote ni sawa,Kama walivyo na mahitaji maalum pia kuna masomo maalumu kutoka kwao ambayo watoto wengine hawana.

•Serikali ipanue elimu hii aswa vijijini ili watu waondokane na imani potofu kwamba huu ugonjwa unatokana na laana au imani za kishirikina

•Mzazi/mlezi kutokuwachukulia awa watoto Kama hawawezi.

HITIMISHO
Wazazi/walezi Ni vyema kuwa makini katika malezi ya mtoto,endapo ikitokea mtoto amezaliwa na tatizo ili inasidia kugundua mapema na kuchukua hatua.
Na mara nyingi wao ndo utufundisha jinsi ya kuishi nao.


1658818986641.png
 

Attachments

  • 1658818984795.gif
    1658818984795.gif
    42 bytes · Views: 27
  • 1658818985169.gif
    1658818985169.gif
    42 bytes · Views: 24
  • 1658818985558.gif
    1658818985558.gif
    42 bytes · Views: 22
  • 1658818985946.gif
    1658818985946.gif
    42 bytes · Views: 18
  • 1658818986287.gif
    1658818986287.gif
    42 bytes · Views: 20
  • Thanks
Reactions: TEK
Upvote 2
Back
Top Bottom