Elimu siyo ngumu lakini mambo kama haya ndiyo yanaifanya iwe ngumu kwa watoto; Wizara ya Elimu, BAKITA boresheni

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Huu ni mfano mdogo tu unaoonesha hatujui tunachokifanya kielimu!

Tazama majina ya sayari kwa kingereza halafu ulinganishe na kiswahili chake, huu ni mzigo kwa watoto lakini hatuoni kama taifa!

Miaka saba asome majina kwa Kiswahili halafu tena kitu kilekile aje aanze upya kukisoma secondary kikiwa na jina tofauti unategegemea nini!

Sayari kwa kingereza
1. Mercury 2. Venus 3. Earth 4. Mars 5. Jupiter 6. Sutan 7. Uranus 8 Netune 9. Pluto

Sayari zile zile kwa kiswahili
1. Mercury > ZEBAKI
2. Venus >ZUHURA
3. Earth > DUNIA
4. Mars > MIRIHI
5. Jupiter >SUMBULA
6. Sutan > SARATENI
7. Uranus> ZOHARI
8. Neptune> KAUSI
9.Pluto >KIBETE AU UTARIDI

Kwanini Wizara ya Elimu na BAKITA majina haya wasingeyatohoa kama yanavyotamkwa kwa Kingereza iwe ndo Kiswahili chake?

Elimu ni nyepesi sana lakini tunaifanya iwe mzigo pasipo sababu ya msingi!

Leo mtoto anafundishwa hii ni ZUHURA baadae tena mtoto huyo kesho anabadilishiwa kuwa ile inaitwa VENUS! Na hatuoni kuwa kuna shida!

Wizara ya elimu na bakita mnaweza saidia kupunguza ugumu wa ELIMU ili kupata wasomi wa kweli wanaoelewa na siyo kukariri!

Chimbuko la kisayansi libakisheni asili yake hata kama litatamkwa kiswahili!
Mambo mengi watoto inabidi wakariri kuliko kuelewa na ndiyo maana hadi Leo hatuna wasomi wakutatua matatizo yetu wenyewe! Kwasababu mfumo unalazimisha tukariri kuliko kuelewa!
 
nchi zilizoendelea elimu inayotolewa macho sana ni msingi. huko kwengine kunakuwa kumepunguza mzigo.
 
Huu ni mfano mdogo tu unaoonesha hatujui tunachokifanya kielimu!

Tazama majina ya sayari kwa kingereza halafu ulinganishe na kiswahili chake, huu ni mzigo kwa watoto lakini hatuoni kama taifa!

Miaka saba asome majina kwa kiswahili halafu tena kitu kile kile aje aanze upya kukisoma secondary kikiwa na jina tofauti unategegemea nini!

Sayari kwa kingereza
1. Mercury 2. Venus 3. Earth 4. Mars 5. Jupiter 6. Sutan 7. Uranus 8 Netune 9. Pluto

Sayari zile zile kwa kiswahili
1. Mercury > ZEBAKI
2. Venus >ZUHURA
3. Earth > DUNIA
4. Mars > MIRIHI
5. Jupiter >SUMBULA
6. Sutan > SARATANI
7. Uranus> ZOHARI
8. Neptune> KAUSI
9.Pluto >PLUTO

Kwanini wizara ya elimu na bakita majina haya wasingeyatohoa kama yanavyotamkwa kwa kingereza iwe ndo kiswahili chake?

Elimu ni nyepesi sana lakini tunaifanya iwe mzigo pasipo sababu ya msingi!

Leo mtoto anafundishwa hii ni ZUHURA baadae tena mtoto huyo kesho anabadilishiwa kuwa ile inaitwa VENUS! Na hatuoni kuwa kuna shida!

Wizara ya elimu na bakita mnaweza saidia kupunguza ugumu wa ELIMU ili kupata wasomi wa kweli wanaoelewa na siyo kukariri!

Chimbuko la kisayansi libakisheni asili yake hata kama litatamkwa kiswahili!
Mambo mengi watoto inabidi wakariri kuliko kuelewa na ndiyo maana hadi Leo hatuna wasomi wakutatua matatizo yetu wenyewe! Kwasababu mfumo unalazimisha tukariri kuliko kuelewa!
Wabadioishe elimu yote tu kuwa ya kiingereza toka chekechea

Kusiwe na discrimination kwenye elimu wengine English medium wengine kiswahili kama ilivyo Kenya na Uganda kiswahili liwe somo tu
 
Wabadioishe elimu yote tu kuwa ya kiingereza toka chekechea

Kusiwe na discrimination kwenyenelimu.wengine English medium wengine kiswahili kama ilivyo Kenya na Uganda kiswahili liwe somo tu
Wazo zuri
 
Alafu 9.pluto sio sayari. inaitwa sayari kibete
Aisee kumbe sayari ya Pluto inaitwa Kibete.Ah kumbe huko ndiko anatoka Mbunge wetu wa sasa Busokelo anayeitwa Mwakibete nilikuwa najiuliza ni wa wapi huyu Mwakibete kumbe kwao Kibete ndio maana barabara ya katumba hadi mwakaleli kunakotoka gesi na chai haiwekwi lami
 
Walimu wenyewe kimalikia kinawashinda ndo waje waweze kukifundisha.
Unaongelea wepi ? Nenda shule zote za English Medium walimu wanaofundisha kule ni hao hao waliotoka vyuo vya serikali na watoto wako vizuri wasoma English medium

Hizo shule walimu watanzania wenzetu waliosomo vyuo vya ualimu hivi hivi vilivyopo Tanzania
 
Kabisa
 
Aisee kumbe sayari ya Pluto inaitwa Kibete.Ah kumbe huko ndiko anatoka Mbunge wetu wa sasa Busokelo anayeitwa Mwakibete nilikuwa najiuliza ni wa wapi huyu Mwakibete kumbe kwao Kibete ndio maana barabara ya katumba hadi mwakaleli kunakotoka gesi na chai haiwekwi lami
Pluto ilishapokwa sifa ya kuwa sayari

Sayari zimebaki nane tu.

Wazungu wajinga sana, miaka yote tuliambiwa Pluto ni sayari kumbe uongo
 
Unaongelea wepi ? Nenda shule zote za English Medium walimu wanaofundisha kule ni hao hao waliotoka vyuo vya serikali na watoto wako vizuri wasoma English medium

Hizo shule walimu watanzania wenzetu waliosomo vyuo vya ualimu hivi hivi vilivyopo Tanzania
Ndiyo maana watoto wanauliza maswali ya kiingereza kwa muundo wa Kiswahili.

"My pen is where?" [emoji3]
 
Shida yako ni hayo majina kuwa ya Kiswahili...ama? Jivunie cha kwako
 
Back
Top Bottom