Elimu siyo ngumu lakini mambo kama haya ndiyo yanaifanya iwe ngumu kwa watoto; Wizara ya Elimu, BAKITA boresheni

Elimu siyo ngumu lakini mambo kama haya ndiyo yanaifanya iwe ngumu kwa watoto; Wizara ya Elimu, BAKITA boresheni

Huu ni mfano mdogo tu unaoonesha hatujui tunachokifanya kielimu!

Tazama majina ya sayari kwa kingereza halafu ulinganishe na kiswahili chake, huu ni mzigo kwa watoto lakini hatuoni kama taifa!

Miaka saba asome majina kwa Kiswahili halafu tena kitu kilekile aje aanze upya kukisoma secondary kikiwa na jina tofauti unategegemea nini!

Sayari kwa kingereza
1. Mercury 2. Venus 3. Earth 4. Mars 5. Jupiter 6. Sutan 7. Uranus 8 Netune 9. Pluto

Sayari zile zile kwa kiswahili
1. Mercury > ZEBAKI
2. Venus >ZUHURA
3. Earth > DUNIA
4. Mars > MIRIHI
5. Jupiter >SUMBULA
6. Sutan > SARATENI
7. Uranus> ZOHARI
8. Neptune> KAUSI
9.Pluto >KIBETE AU UTARIDI

Kwanini Wizara ya Elimu na BAKITA majina haya wasingeyatohoa kama yanavyotamkwa kwa Kingereza iwe ndo Kiswahili chake?

Elimu ni nyepesi sana lakini tunaifanya iwe mzigo pasipo sababu ya msingi!

Leo mtoto anafundishwa hii ni ZUHURA baadae tena mtoto huyo kesho anabadilishiwa kuwa ile inaitwa VENUS! Na hatuoni kuwa kuna shida!

Wizara ya elimu na bakita mnaweza saidia kupunguza ugumu wa ELIMU ili kupata wasomi wa kweli wanaoelewa na siyo kukariri!

Chimbuko la kisayansi libakisheni asili yake hata kama litatamkwa kiswahili!
Mambo mengi watoto inabidi wakariri kuliko kuelewa na ndiyo maana hadi Leo hatuna wasomi wakutatua matatizo yetu wenyewe! Kwasababu mfumo unalazimisha tukariri kuliko kuelewa!
Hapo bado maneno mapya kwenye masomo mengine nilisikia
  1. Kani
  2. Neli mtoleo
  3. Viasili
  4. Makadi
  5. Ngamizi
  6. Puku
  7. Zandawizi
  8. Ndaki
  9. Dindilimunyo
Frustration tupu
Hii inawahusu watoto wa makabwela wanasoma vitu vipya kwa lugha mpya wakati watoto wa watengeneza mitaala wanasoma vitu kwa kiingereza
 
Wanaoendelea na masomo kwenye nchi kama Ukraine, Germany, Japan, China au Russia wanakaa darasani mwaka mzima kujifunza lugha hizo tu.
Huwezi kuwalinganisha hao na watoto
 
Mada bomba kabisa ambayo nimeanza nsyo mwaka nashukuru mtoa mada sisi kama wadau tujitahidi kulisemea hili kwenye majukwaa mbalimbali
 
Kuna haja kutokana na mabadiliko ya ghafla ya lugha toka msingi kwenda sekondari kuwe na mwaka mmoja wa kunoa Kiingereza chao thereafter ndio masomo mengine yafundishwe. Kiingereza cha msingi kimsingi hamna kitu unless English Medium at least.
Kuna ubaya gani shule zote zitoe elimu inayofanana toka awali hadi vyuo, watoto wa wenye uwezo wanasoma kiingereza from day 1, hawa wengine wanasoma kwa kiswahili halafu mbele wanabadiilishiwa lugha kiasi cha kuwachanganya na kuwachelewesha kujifunza na kuelewa
 
Ndiyo maana watoto wanauliza maswali ya kiingereza kwa muundo wa Kiswahili.

"My pen is where?" [emoji3]
Hata viongozi wenyewe wakiwa majukwaani wanahangaika kuchanganya lugha hawaeleweki
 
Kuna ubaya gani shule zote zitoe elimu inayofanana toka awali hadi vyuo, watoto wa wenye uwezo wanasoma kiingereza from day 1, hawa wengine wanasoma kwa kiswahili halafu mbele wanabadiilishiwa lugha kiasi cha kuwachanganya na kuwachelewesha kujifunza na kuelewa
Kama kuna advocate wa elimu nchini kutolewa kwa Kiingereza from elimu ya awali to the highest level ni mimi.

Ushauri ulioni-quote ni endapo Serikali itaendelea kung'ang'ania mfumo uliopo wa Kiswahili then Kiingereza.
 
Pluto ilishapokwa sifa ya kuwa sayari

Sayari zimebaki bane tu.

Wazungu wajinga sana,miaka yote tuliambiwa pluto ni sayari kumbe uongo
Na bado miongoni mwao mpaka majuzi wanaendelea kubishana
 
Hapo bado maneno mapya kwenye masomo mengine nilisikia
  1. Kani
  2. Neli mtoleo
  3. Viasili
  4. Makadi
  5. Ngamizi
  6. Puku
  7. Zandawizi
  8. Ndaki
  9. Dindilimunyo
Frustration tupu
Hii inawahusu watoto wa makabwela wanasoma vitu vipya kwa lugha mpya wakati watoto wa watengeneza mitaala wanasoma vitu kwa kiingereza

Mkuu kama umeweza kuyahifadhi majina hayo kwa namna hiyo basi hapo unawapa nguvu hao wabunifu wa hayo majina kuendelea na ubunifu zaidi wa maneno mapya, inatakiwa wavunjwe moyo ili majina ya kiingereza yaliyokuwepo kitumika ili kutowachanganya watoto na elimu yetu kwa ujumla.
 
Nimeyatafuta kitabuni kwakuwa mpaka leo nimeshindwa kuyakariri
 
Hapo bado maneno mapya kwenye masomo mengine nilisikia
  1. Kani
  2. Neli mtoleo
  3. Viasili
  4. Makadi
  5. Ngamizi
  6. Puku
  7. Zandawizi
  8. Ndaki
  9. Dindilimunyo
Frustration tupu
Hii inawahusu watoto wa makabwela wanasoma vitu vipya kwa lugha mpya wakati watoto wa watengeneza mitaala wanasoma vitu kwa kiingereza
Duh
 
Screenshot_20230101_132933.jpg
 
Aisee kumbe sayari ya Pluto inaitwa Kibete.Ah kumbe huko ndiko anatoka Mbunge wetu wa sasa Busokelo anayeitwa Mwakibete nilikuwa najiuliza ni wa wapi huyu Mwakibete kumbe kwao Kibete ndio maana barabara ya katumba hadi mwakaleli kunakotoka gesi na chai haiwekwi lami
We jamaa ni wa tukuyu..?
 
Back
Top Bottom