Elimu siyo ngumu lakini mambo kama haya ndiyo yanaifanya iwe ngumu kwa watoto; Wizara ya Elimu, BAKITA boresheni

Shida yako ni hayo majina kuwa ya Kiswahili...ama? Jivunie cha kwako
Umekigundua wewe.....ita jina kwa lugha yako lakini litamke kama lilivyo kwa kingereza hutapungukiwa
 
Nakubali tatizo lipo, lakini ni kubwa kuliko lugha.

Ukitaka kunielewa zaidi fuatilia matokeo ya mitihani ya somo la kiswahili na yenyewe huwa ni mabovu vile vile.

Kama kweli lugha ni moja ya vikwazo ningetegemea kuona watoto na wadogo zetu wanapasua sana kwenye somo la lugha mama.
 
Umekigundua wewe.....ita jina kwa lugha yako lakini litamke kama lilivyo kwa kingereza hutapungukiwa
Kwani kuziita Kwa Kiswahili ndio inabadilisha wagunduzi ama? Ondoa fikra za kitumwa kichwani ndugu!
 
Uwelewa ni mkubwa! Kwa maana ya maarifa
 
Kwani kuziita Kwa Kiswahili ndio inabadilisha wagunduzi ama? Ondoa fikra za kitumwa kichwani ndugu!
Inaleta mkanganyika na matumizi mabaya ya muda mtu anasoma kama kitu kipya wakati alitakiwa apigwe brush tu
 
Kuna sayar inaitwa saratan, hiyo ni mpy
 
No.6 tuweke Sarateni
No.9 tuweke utaridi (japo wanasema imepoteza sifa ya kuwa sayari)
 
Ungejua baraza la kiswahili limejaa wajinga na wapumbavu wa kutupwa ndiyo utajua kwanini kiswahili kinajengeka vizuri nje ya baraza.kuna matatizo mengi ya kijinga mfano sijui kama hapa JF kuna page yao kama ilivyo tanesco na ttcl nk maana tungeweza kuwapa maoni na ushauri ...kuna siku mtu wa baraza la kiswahili alikuwa redioni ana jimwambafai kama ilivyo kawaida yao ya kujiona wataalamu kwa kukosoa wengine na kuwaona awajui....basi kuna neno alisema lina ukakasi ni kama tusi ila yeye kung'ang'ania sehemu ya matumizi yake hadi mtangazaji wa redio akamshangaa maana lile neno lilikuwa ni tusi kabisa .....yule mtangazaji akamwambia mbona ilo neno lina tamkika kama tusi kabisa ...lakini jamaa kangangania ilo neno lao walilo buni wao hatakama halina ladha .....sasa hivi baraza la kiswahili wana lazimisha kiswahili kiwe wanavyo taka wao siyo jamii inavyo penda wakibuni neno basi awataki neno jingine lolote kutoka nje hata kama neno lao alikubaliki.
 
Wabadioishe elimu yote tu kuwa ya kiingereza toka chekechea

Kusiwe na discrimination kwenye elimu wengine English medium wengine kiswahili kama ilivyo Kenya na Uganda kiswahili liwe somo tu
Ujinga ...watu mnao waza hivyo mnaufinyu wa akili sana ...nitaweza kukusmbieni kwa nini mnaufinyu wa akili kama mtataka kujua
 
Pluto ilishapokwa sifa ya kuwa sayari

Sayari zimebaki bane tu.

Wazungu wajinga sana,miaka yote tuliambiwa pluto ni sayari kumbe uongo
Kwani umesahau tulivyo fundishwa kuwa reli ina gapu ili kuzuia inapo pigwa na jua na kutanuka isipinde ila cha ajabu kwa sasa inachomelewa yote na magepu kuondolewa kwa huko kuichomea ...kumbe ndiyo inakuwa bora zaidi
 
Sasa jiulize jina la somo GEOGRAPHY > Unaliita vizuri JIOGRAFIA
halafu yaliyomo ndani unayabatiza jina jingine la kwako kama umegundua wewe!

Wangeyaacha kwa uhalisia elimu yetu ingekuwa nyepesi sana!
Watoto wetu wanadabo elimu bila kujua!
Ebu waza Leo hii watoto watohoe jina kwa kilugha then kiswahili ligeuke, na tena kiswahili nalo baadae ligeuke ..
Tunawachosha wanaikimbia elimu au wanaamua kukariri tu bhaasi
 
Labda kama maana ya lugha imebadilika siku hizi ila nilichofundishwa hapo kale ni kwamba lugha ni sauti za "nasibu".

Keyword hapo ni nasibu; sauti za bahati zinazozuka katika jamii kwa ajili ya mawasiliano. Bakita wao wanatungia lugha mezani? Duh!
 
Nikweli maneno mengi ya kisayansi yanatakiwa kuachwa kama yalivyo kama kompyuta ,redio nk ...hii ndiyo maana wazungu wakabuni wakasema kuna majina ya kisayansi ....maana yake siyo ya lugha ya nchi fulani ni scientific language tosha maana mgunduzi wa sayansi au tekinolojia fulani anaweza akatokea pande yoyote ya dunia ..pia majina ya wavumbuzi yanatumika pia
 
Wanaoendelea na masomo kwenye nchi kama Ukraine, Germany, Japan, China au Russia wanakaa darasani mwaka mzima kujifunza lugha hizo tu.

Kuna haja kutokana na mabadiliko ya ghafla ya lugha toka msingi kwenda sekondari kuwe na mwaka mmoja wa kunoa Kiingereza chao thereafter ndio masomo mengine yafundishwe. Kiingereza cha msingi kimsingi hamna kitu unless English Medium at least.
 
Kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…