DOKEZO Elimu wilaya ya Ubungo hii ni aibu ifike mwisho

DOKEZO Elimu wilaya ya Ubungo hii ni aibu ifike mwisho

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mbogi

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2021
Posts
803
Reaction score
997
Nimekuwa na madudu mengi katika idara ya elimu Ubungo baadhi kwa kutaja ni kama;
1. Kucheleweshwa kwa watumishi kupandishwa madaraja.

2. Kila mara kutolipwa au kukopwa posho kwa wasimamizi wa mitihani ya utamilifu (mock).

3. Kutokuwa na utaratibu mzuri wa mawasiliano na kutoa maagizo ya zima moto nk

Leo ni aibu kubwa Mtihani wa mock mkoa kufanyika hadi usiku wa Saa 12: 45 na kwa ratiba tofauti,

Wilaya zingine wamefuata ratiba kama ilivyopangwa ila Ubungo imekuja mitihani pungufu kwa masomo yote hali iliyolazimu kikao shule kuanza kufanya mtihani uliopatikana kwa utofauti wake na muda wake.

Je thamanii ya mtihani iko wapi na je matokeo yake yatakuwaje maana kuna tetesi kuwa zipo shule hadi mwisho zimefanya masomo matano badala ya sita.

Hii ni aibu iliyotokana na mazoea yaliyopita, sasa ni muda wa kurekebisha madudu haya ambayo yamekuwa yakiwaumiza walimu na wazazi waliochangia mitihani hii.
 
Kimsingi anamalalamiko na idara ya elimu ubungo,hujaelewa nini au ndio mhusika wa malalamiko yake ,🤔
"Leo ni aibu kubwa Mtihani wa mock mkoa kufanyika hadi usiku wa Saa na kwa ratiba tofauti, wilaya tano wamefuata ratiba kama ilivyopa"

👆 hiyo paragraph wew umeielewa? Ndio maana Mpwayungu Village huwa anawasema walimu mnasema anawaonea. Sasa angalia mwalimu mwenzako alichoandika as if wote tunasimamia hyo mitihani
 
Kumekuwa na uendeshaji mbovu na wa dhuluma wa mara nyingi ktk mitihani muhimu ya shule za Ubungo kama vile mock nk.

1. Walimu kunyimwa posho au kukopwa kila mara tofauti na wilaya nyingilne zote za Dar es s
Salaam.
2. Kucheleweshwa kupanda madaraja kwa walimu ktk wilaya ya Ubungo ni kawaida na wala hawaoni kuwa ni tatizo.

3. Kituko cha sasa ni mtihani wa mock mkoa kufanyika nusunusu hadi usiku wa Saa moja na kila shule ikiwa inaamua Somo lolote la kuanza na hata baadhi ya shule wamefanya masomo matano badala ya huku shule zingine za wilaya hiyo hiyo zikiwa zimefanya masomo yote sita.

Swali la msingi je ni namna gani matokeo yatatolewa na kukubaliwa kwa shule zote za mkoa? Ikumbukwe kuwa shule za binafsi zinachangia sh 8500 kwa kola mtoto huku zile za serikali zikitoa sh 1000 kea kila mwanafunzi kutoka fedha za ruzuki.

Hii ni aibu ambayo kamwe isifumbiwe macho na uwe mwanzo wa kurekebisha kasoro nyingi zinazofanywa ktk wilaya hii na kuwaumiza si watumishi tu bali hata Wananchi walio na watoto ktk shule za Ubungo.
 
"Leo ni aibu kubwa Mtihani wa mock mkoa kufanyika hadi usiku wa Saa na kwa ratiba tofauti, wilaya tano wamefuata ratiba kama ilivyopa"

👆 hiyo paragraph wew umeielewa? Ndio maana Mpwayungu Village huwa anawasema walimu mnasema anawaonea. Sasa angalia mwalimu mwenzako alichoandika as if wote tunasimamia hyo mitihani
Amekurupuka kwenye uandishi wake, nahisi wakati anaandika Uzi alikua anagombania usafiri wa tandika
 
Mkuu huku kwetu hiyo mitihani ya mock walimu huwa wanasimamia bure kabisa tena kiroho safi.... Mpwayungu anasafari ndefu sana ya kuweka sawa haya mambo
 
Mkuu huku kwetu hiyo mitihani ya mock walimu huwa wanasimamia bure kabisa tena kiroho safi.... Mpwayungu anasafari ndefu sana ya kuweka sawa haya mambo
Sawa, vipi uthamani wa mtihani, mtihani gani wa mkoa kila shule inaanza na Somo wanalotaka kwa muda wanaotaka hasa ktk wilaya moka?

Je wilaya zingine zitakubaliana na matokeo?

Watoto na walimu kufanya mtihani hadi Saa 1:00 usiku ni sawa?

Je tatizo ni nini kwa Ubungo matukio ya hovyo kwenye mitihani hii kujirudia mara kwa mara?
 
Sawa, vipi uthamani wa mtihani, mtihani gani wa mkoa kila shule inaanza na Somo wanalotaka kwa muda wanaotaka hasa ktk wilaya moja hii ya ubungo?

Je wilaya zingine zitakubaliana na matokeo?

Watoto na walimu kufanya mtihani hadi Saa 1:00 usiku ni sawa?

Je tatizo ni nini kwa Ubungo matukio ya hovyo kwenye mitihani hii kujirudia mara kwa mara?
 
Sawa, vipi uthamani wa mtihani, mtihani gani wa mkoa kila shule inaanza na Somo wanalotaka kwa muda wanaotaka hasa ktk wilaya moka?

Je wilaya zingine zitakubaliana na matokeo?

Watoto na walimu kufanya mtihani hadi Saa 1:00 usiku ni sawa?

Je tatizo ni nini kwa Ubungo matukio ya hovyo kwenye mitihani hii kujirudia mara kwa mara?
Mkuu kwa mfano mwaka jana huku kwetu mitihani ilisaishwa hovyo.... Matokeo unakuta mwanafunzi wa art ana A ya physics na chemistry wakati hayo masomo hakufanya. Hii nchi ni kituko.
 
Mkuu kwa mfano mwaka jana huku kwetu mitihani ilisaishwa hovyo.... Matokeo unakuta mwanafunzi wa art ana A ya physics na chemistry wakati hayo masomo hakufanya. Hii nchi ni kituko.
Ndiyo maana tunasema ifike muda haya mambo yakome kwa ajili ya afya ya elimu yetu. Tunalalamika kuwa walimu serikali haiwajali kumbe hata viongozi wao wa ngazi za chini nao hawajali. Mwl anasimamia hadi usiku hata nauli hajapewa, wanafunzi nao hawaelewi ratiba haifuatwi na taarifa ni za zima moto, sijui huko ni wapi ila kwa Ubungo naona imezidi mbona hayo malalamiko hatuyasikii wilaya zingine za Dar?
 
Kwa hiyo hakuna ratiba specific mpaka kila wilaya wanafanya kivyao?
 
Walimu kama kawaida yenu wajungu na fitina.
Siyo majungu, madudu yakifanyika yasemwe kuendelea kunyamaza ndiko kunakowafanya watendaji kuendelea kufanya mengi zaidi. Na mbaya zaidi hata waligundua anayetoa habari anakiona cha mtema kuni.
 
Huyu ni mwalimu. 😁
cdf252bed12a2e635224ed85abc83767.jpg
 
Wakati Wilaya ya Kinondoni inagawanywa na kuipata Ubungo. Wale wapigaji wooote waliondolewa Kinondoni wakapelekwa Ubungo. Huko kwenye elimu ni madudu matupu...

Hata hivyo Dsm kitengo cha elimu tangu ameondoka Lissu kama Afisa elimu akaingia sijui nani yule yani ni madudu matupu
 
Back
Top Bottom