Elimu ya dini iwekewe mkazo mashuleni na iwe ni somo la lazima kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu

Sijawahi kuona uvumbuzi wowote uliofanywa na dini, dunia iko katika mapinduzi ya 4 ya viwanda na teknolojia kuelekea mapinduzi ya 5 bado unawaza watoto wetu wafundishwe stori za muhammad na yesu wa nazareth?? si bora hata wafundishwe stori za kina chief mkwawa na mangungo zinazoendana na mazingira yao.
 
Tunahitaji kutenganisha dini na Taifa, wewe unataka kutuendeleza kwenye giza.

Imani ni shambulio la akili.
 
Ili madrasa na sunday school ziheshimike na zipate watoto ni lazima Serikali iliweke somo la dini kua lazima katika mitaala.
Mawazo yako yananishangaza sana,

How serikali iingilie mambo haya ya kiimani!?

Uko sawa kweli wewe?
 
Unataka kutuletea balaa tuu, dini yako nenda msikitini au kanisani huku nje hatutaki kusikia, matatizo na mavita yote katiba historia ya hii Dunia 99% ni hizo dini tuu, tafadhari mtuache, Sheria tulizonazo zinatosha kutuweka msitalini na kuishi kwa amani baina yetu
 
Ukiristo hauna code ya mavazi hata wakivaa mini skirt wanaenda kusali
 
Na mkiongea habari za dini mpaka mbalance ukiristo na uislam kana kwamba mtoa maada una dini mbili

Unaogopa nini kuelezea maadili katika nyanja ya dini yako, nijuavyo maadili ni suala pana kuna maadhi ya dini hazina maadili naturally bora hata mila na tamaduni nyingine ambazo hazihusiani na dini

Mtoa mada kuwa specific
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…