Elimu ya dini iwekewe mkazo mashuleni na iwe ni somo la lazima kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu

Na asiye na dini afundishwe nini? Nafikiri kuwe na mtaala wa uraia mwema, huko wafundishwe Katiba yote, haki na wajibu wao, mambo yanayochukuliwa kama ni uhalifu, jinai, uhaini n.k. Upendo, nidhamu kwa kila mtu, kila jambo na kujitolea na ushirikiano.
 
Dini haijawahi kuacha mtu salama, Historically dini zimeua millions na zinaendelea kuua, kuanzia crusades mpaka leo Gaza chanzo ni dini tuu, tafadhari kaeni na dini zenu misikitini au makanisani kwenu, tukitaka tutakuja kujifunza huko
 
Kwasababu uislamu na Ukristo ndio dini kuu
 
Mbona hata kuna Viongozi wa Dini wala Rushwa.

BAKWATA hutengezewi Cheti cha Ndoa bila kuhonga Mlungula.
Ni kwasababu wameingia pasipo mfumo rasmi, akhalabu katika wastaaribu wadhalimu hawakosekani.
 
Dini inahusika na mahusiano kati ya Mungu na mtu binafsi. Maadili hutegemea hiari na dini juu ya hisia za kiakili. Katika maendeleo ya mwanadamu, maadili na dini vyote viwili hukua pamoja na kuathiriana.
Kwa ni lazima wote twende mbinguni? Hamuoni kama mkienda nyie inatosha? Mbona mnapenda watu wengine nao wakajazane kwenye hiyo pepo yenu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…