Elimu ya Kinywa: Usafi wa meno na kinywa kwa ujumla, sababu, kinga na tiba za harufu mbaya

Elimu ya Kinywa: Usafi wa meno na kinywa kwa ujumla, sababu, kinga na tiba za harufu mbaya

Adui namba 1 wa meno ni sukari na sukari inakaribisha bacteria ambao wakiwa wamezoeshwa hiyo sukari basi hupiga kambi kwenye meno.

Hivyo sukari kwenye chai na vinywaji au vyakula vyenye sukari kama doughnuts, cocacola ukitumia lazima ufahamu kwamba ukienda kulala bila kupiga mswaki na kusafisha kinywa basi bacteria wataendelea kula mabaki 24/7 na ndio unaona jino linachimba.

Wenye tatizo la fizi wanatakiwa wamwone hygienist ambae atakushauri namna ya kupiga mswaki na dawa za zinazofaa kutumia.

Hayo maduka ya uzunguni yanaweza kuwa na dawa aina mbalimbali hasa za Uingereza (GlaxoSmithKline - GSK) zenye kazi mahsusi kushughulikia meno likiwemo tatizo la unjano.

Mbali ya dawa maarufu ya Colgate kuna dawa zingine maalum kama vile Oral- B White, Oral B expert, Sensodyne, Pronamel, Corsodyl Daily Original Toothpaste 75ml na Colgate MaXWhite.

Hygienist anashauri namna ya kuondoa uchafu kwenye meno na matabaka au plaque na kuepusha kuoza kwa meno au tooth decay. Pia anashauri vyakula vya kuepuka kula ambavyo vinaharibu meno kwa kasi ya ajabu kama vile chips mayai, vinywaji baridi kama bia na soda.

Hii inasaidia sana kwa wale ambao wana matatizo ya meno ambayo mengine ni ya kurithi.
 
Aiseee!! Hivi matatizo ya meno nayo ni ya kurithi!!

Yes, unaweza kukuta mama au baba akiwa na tatizo la meno basi wanaweza kabisa kurithisha.

Utakuta mama au baba wanan'goa meno kila mara au wana meno mabovu na baadae
mtoto anafuata nae anakuwa na meno mabovu.

Lakini kesi nyingi ni za watoto wengi kuzoeshwa kula vitu vitamu tangu wadogo na kupelekea kuanza kupata ubovu wa meno wakiwa wadogo.
 
Oooh! Nashukuru kwa somo mpendwa, barikiwa.
 
Unatumia baking powder na lemon juice au maji...fanya mara moja au mbili kwa wik...hii ni kutokana na acidic nature ya mchanganyiko huo...kitaalum haushauriw sabab ukitumika continuosly inaweza kuharibu teeth enamel na kufanya meno kua much sensitive kwa vitu vya baridi na moto ....aĺl in all huu mchanganyiko ni njia mbadala ya kuyang'arisha meno kwa gharama nafuu... ila tumia kwa kwa uangalifu....natanguliza shukrani!!
 
Basi kule kuunguza ndo kunakoua wale bakteria sasa.

Kama umesoma Baiolojia vizuri utakuwa unajua kwamba bakteria hawawezi kustahimi hali ya moto au joto kali.

Na ndo maana hizo mouthwash zimetengenezwa ziwe hivyo kwa makusudi ili kusaidia kuua hao bakteria wanaosababisha harufu mbaya.

Zingekuwa zina madhara basi aminia hata sokoni zisingekuwepo.
Mi mshamba hebu tupiamo picha ya hiyo mouthwash angalau
 
Yes, unaweza kukuta mama au baba akiwa na tatizo la meno basi wanaweza kabisa kurithisha.

Utakuta mama au baba wanan'goa meno kila mara au wana meno mabovu na baadae
mtoto anafuata nae anakuwa na meno mabovu.

Lakini kesi nyingi ni za watoto wengi kuzoeshwa kula vitu vitamu tangu wadogo na kupelekea kuanza kupata ubovu wa meno wakiwa wadogo.
vipi kwa wale wenye ya brown ya arusha ukitaka yawe meupe njia ipi n bora isiyo na madhara
 
Kuna mtu wangu wa karibu sana amabe yeye hupiga mswaki kila asubui na anapolala usiku lakini hua anakua na harufu mbaya sana ya mdomo..tatizo linaweza kua ni nini na anawezaje kupata tiba ya hilo tatizo mkuu.
Anasugua ulimi? Maana kunuka mdomo kunaletwa na ulimi mchafu
 
vipi kwa wale wenye ya brown ya arusha ukitaka yawe meupe njia ipi n bora isiyo na madhara

Sidhani kama inawezekana iwapo tunao wataalam kwa TZ, ila kwa nje ya nchi ya nchi hasa Ulaya, inawezekana ila itakuwa ghali sana.

Wanaita "whitening"
 
Sidhani kama inawezekana iwapo tunao wataalam kwa TZ, ila kwa nje ya nchi ya nchi hasa Ulaya, inawezekana ila itakuwa ghali sana.

Wanaita "whitening"
hizi zinazofanyika uku TZ n zip mkuu maana naona watu wanasafisha
 
Back
Top Bottom