UTAKUWA ulisha wahi sikia mambo mengi mbalimbali yenye imani ya kutisha kuhusiana na afya ya kinywa na meno ,nimeandaa baadhi ya mambo na ukweli wake naomba uongeze za kwako ambazo ulisha wahi sikia sehemu,kuhusia na afya ya kinywa na meno tusharee.
IMANI POTOFU KUHUSU KUHUSU AFYA YA KINYWA NA MENO.
1.IMANI POTOFU;
KUKATA KIMEO (TRADITIONAL OVULECTOMY)
UKWELI ;Kimeo (ovula)hakikatwi ,ila huwa na maambukizi ya bacteria hivyo mgonjwa anatakiwa kutibiwa kwa dawa ,
2.IMANI POTOFU
MENO YA PLASTIC HUTOLEWA KWA IMANI ZA KIMILA
UKWELI; meno ya plastic kwenye mwili wa binadamu , neonatal teeth ( mtoto anazaliwa na meno ) mara chache mtoto kuzaliwa na meno na hayana madhara isipokuwa kama yana muumiza mama ,hutolewa hospitali.
3.IMANI POTOFU
MAMA MJAA MZITO HATAKIWI KUTIBIWA MENO
UKWELI ;ni kwamba mama mjamzito anatakiwa kupata matibabu yote ya meno kulingana na ushauri wa dactari atakavyo ona.
4.IMANI POTOFU
HUTAKIWI KULA CHOCHOTE KABLA YA KUNG’OA MENO na HAITAKIWI KUNG’OA meno mchana
UKWELI,tunashauri mtu awe amekula na kushiba wakati anakuja kung’oa meno na meno yana naweza ng’olewa muda wowote.
5.IMANI POTOFU
DAWA YA JINO NI KUNG’OA
UKWELI ,ni kwamba kuna aina nyingi za matibabu ya meno ikiwemo kuziba ama kujaza ; matibabu ya mzizi wa jino root cannal treatment na kukuta mizizi ya jino yaani APICECTOMY.
IMEANDALIWA NA
DR.MBOBOYU …….076221006 .THE DENTAL SURGEON(DDS)