Elimu ya Kinywa: Usafi wa meno na kinywa kwa ujumla, sababu, kinga na tiba za harufu mbaya

Elimu ya Kinywa: Usafi wa meno na kinywa kwa ujumla, sababu, kinga na tiba za harufu mbaya

Asante kwa kuleta uzi wenye tija.

Mengi yamesemwa.Ila ukipiga mswaki usisukutue na maji ukimaliza.Iache dawa mdomoni iue vijidudu.

Piga mwaki mara mbili kwa siku na utumie si pungufu ya dakika tano.Hakikisha unasugua na ulimi.

Tumia baking soda mara moja kwa mwezi kuswakia ili ikupe meno meupe.

Msikilize mganga wa meno hapo juu.

Ulimi si wa kusugua. Ni wa kukwanguliwa.
 
Napiga mswaki mara mbili kwa siku asubuhi na usiku kabla ya kulala, pia baada ya kupiga mswaki huwa nasukutua mdomo kwa kutumia mouth wash ya listerine. Dawa za meno ambazo naona ziko vizuri ni Colgate, sensodine na close up ila ni muhimu kununua original.
Tupe trick za kupata orijino na kuzitofautisha na fake kiongozi
 
Niwashauri watu wanaonunua zile dawa za meno kwa wamachinga zile sio dawa aiseh nilijlaumu nilipopoteza 1500 kuchukua Colgate nikakuta ina ladha/Radha tofauti na ile nilozoea Colgate ni moja tu nenda pharmacy au duka linaloeleweka kiufupi naona Colgate ni dawa sahihi ya meno na ulimi karibuni.
 
Kuna mtu wangu wa karibu sana amabe yeye hupiga mswaki kila asubui na anapolala usiku lakini hua anakua na harufu mbaya sana ya mdomo..tatizo linaweza kua ni nini na anawezaje kupata tiba ya hilo tatizo mkuu.

Ubovu wa meno yani meno kua na matobo au visiki akazibwe yani filling na akiwa ana visiki vikang'olewe...ufizi ukiwa katika hali mbaya yani gingvits
 
MKUU KWA DAR ES SALAAM HIYO DAWA YA GSK INAPATIKANA WAPI? ASANTE

Mkuu, GSK ni kampuni kubwa ya madawa mbalimbali iliyoyopo Uingereza.

Lakini ukitaka dawa nzuri za meno zinozalishwa na kampuni hii ni Aquafresh au Sensodyne.

Hizi ni dawa bora kabisa za meno zenye kukufanya unukie kinywa na meno yawe yameremeta.

Kumbuka ukipiga mswaki usisukutue na maji bali uteme tu dawa na kuiacha kinywani ikiyeyuka na kufanya kazi yake iliyokusudiwa.
 
Mkuu bei ya braces ya upande wa juu ni sh ngap?
 
Hv kuuliza SI ujinga hv vile vichuma vinavyopitaga kwenye meno katikati huwa ni vya nini au meno yakilegea ndo unatia hvyoo
 
Back
Top Bottom