Elimu ya Kinywa: Usafi wa meno na kinywa kwa ujumla, sababu, kinga na tiba za harufu mbaya

Elimu ya Kinywa: Usafi wa meno na kinywa kwa ujumla, sababu, kinga na tiba za harufu mbaya

Nyani Ngabu,
Mimi huo ushauri nilipewa na daktari sikuweza kumbishia,ukizingatia alinifanyia maajabu kwa kunipa tiba ya tatizo lililonisumbua kwa muda mrefu sikuwa na budi kumuamini,japo nakubaliana na wewe kwani hizo product zipo kwa miaka mingi ila kuna tofauti aisee,

Kwani hizi za bongo ukizitumia ni kama umemeza kemikali,zina joto mpaka zinakua kama zinaunguza vile na povu kama la sabuni.
 
Mimi huo ushauri nilipewa na daktari sikuweza kumbishia,ukizingatia alinifanyia maajabu kwa kunipa tiba ya tatizo lililonisumbua kwa muda mrefu sikuwa na budi kumuamini,japo nakubaliana na wewe kwani hizo product zipo kwa miaka mingi ila kuna tofauti aisee,kwani hizi za bongo ukizitumia ni kama umemeza kemikali,zina joto mpaka zinakua kama zinaunguza vile na povu kama la sabuni.

Basi kule kuunguza ndo kunakoua wale bakteria sasa.

Kama umesoma Baiolojia vizuri utakuwa unajua kwamba bakteria hawawezi kustahimi hali ya moto au joto kali.

Na ndo maana hizo mouthwash zimetengenezwa ziwe hivyo kwa makusudi ili kusaidia kuua hao bakteria wanaosababisha harufu mbaya.

Zingekuwa zina madhara basi aminia hata sokoni zisingekuwepo.
 
Nyani Ngabu,
Nimekulewa mkuu,ndo maana zina ridhaa ya TFDA,labda ntakapoanza kutumia tena nitatafuta kwenye hizo supermarket ulizo mshauri yule bwana wa mwanzo.
 
Halafu ukiwa unajisugua sana kwenye ulimi unatengeneza mazingira ya kutapika au kutoa udenda na siyo mate. Huwa inaboa unaweza kusukutua na maji udenda hauishi aiseee

Unazungumzia gag reflex?
 
Nadhani mkuu, japo sina uhakika, terminology ngumu kwangu hiyo. Ila ukiwa unaswaki at the end ukianza kusafisha ulimi kwa kusugua ni udenda au kutapika hasa ukigusa eneo la mwisho wa ulimi, ukijaribu kusukutua na maji bado ukitema mate yanatoka kama udenda.

Yup...ndo gag reflex hiyo.

Na zipo mbinu za kuipunguza...
 
Sasa Ngabunocchio umesahau kuhusu watoto wadogo kuweka Sealants kwenye meno.
Huwa inasaidia kinoma kwasababu umri huo wanpenda sana vitu vya sukari,
It works well kabisa na meno huwa yanakuwa meupe hadi akishakua na matundu matundu kwenye meno yanakuwa hayapo.
 
Nyani Ngabu.. Wanasema hizi toothpick ninasababisha kuharibu meno na fizi je linaukweli jambo hili..!?
 
Ni kweli dawa zinauzwa mtaani kwenye maduka madogo madogo nyingi ni feki wanao sambaza huwa ni jamaa flan utawaona wana baskeli halafu wamebeba ma box hao huwa wana dawa nyingi feki hata mswaki, utagundua ukienda nakuma supermarket au supermarket zenye hadhi ya juu kuna miswaki inayotolewa na Colgate inauzwa sh 3,000 hadi 5,000 zina ubora wa hali ya juu sana na zilizopo mtaani za 200-600 zinatofauti sana na hizo sasa matengenezo ndio tofauti licha ya kuwa wanasema ni kuwasaidia watu wa hali ya chini kupata bidhaa lakini sio sahihi wangeuza bei hiyo ila ziwe na ubora.

nliwahi kutumia whitedent nliyonunua mtaani bado mdmo ukabaki una harufu kama vile nimekula samaki sikuelewa kwann badae nligundua ladha ya iyo dawa na nyingine nliyonunua vinatofautiana ila jina hilo hilo.
zinc,
 
Halafu watu na makampuni mengine yameamua kutengeneza tooth pick ili kujipatia kipato na si kwa ajili ya kuwasaidia wenye meno inayo nasa vyakula, kuna toothpick flani zipo kwenye kopo la round ukiweka mdomoni zinakuwa kama na touth paste utasikia kama ladha ya dawa ya meno hizo nzuri maana zina dawa ila hayo makampuni mengine yanachonga vijiti bila hata ya kuzingatia aina ya mti na ubora wake.

Ukizichoma fizi zinatoa damu hapo pana baki na kama kidonda kidogo usipopata dawa kinaweza kikaendelea kutoa damu taratibu na kisikauke sasa hapo yamekuwa mengine ukila chakula kinaingia hapo ukila tena kinaingia sasa panaanza kuunda kitu flani, ni vema kuzingatia usafi wa meno na dawa.
@Kaabah,
 
Nyani Ngabu.. Wanasema hizi toothpick ninasababisha kuharibu meno na fizi je linaukweli jambo hili..!?

Ndivyo wanavyosema,ninaweza kuamini kwani kuna dada mmoja enzi hizo nikiwa bwana mdogo alikua ana tabia ya kuweka kijiti kati ya meno ili aweze kuwa na mwanya na hatimaye aliupata japo haukua mkubwa sana,sasa wanasema mazoea hujenga tabia,kwa hiyo unapochokonoa meno yako na vijiti hasa kati ya jino na jino baada ya muda mrefu wanasema huwa inaacha athari ya aidha meno/jino kulegea.

Wanashauri watu wawe wanatumia zile nyuzi wanazoziita dental floss kama unataka kusafisha meno badala ya vijiti.
 
Ndivyo wanavyosema,ninaweza kuamini kwani kuna dada mmoja enzi hizo nikiwa bwana mdogo alikua ana tabia ya kuweka kijiti kati ya meno ili aweze kuwa na mwanya na hatimaye aliupata japo haukua mkubwa sana,sasa wanasema mazoea hujenga tabia,kwa hiyo unapochokonoa meno yako na vijiti hasa kati ya jino na jino baada ya muda mrefu wanasema huwa inaacha athari ya aidha meno/jino kulegea.

Wanashauri watu wawe wanatumia zile nyuzi wanazoziita dental floss kama unataka kusafisha meno badala ya vijiti.
Asante.. na hizo mara chache mno kupatikana maana sehemu zetu za vyakula wanaweka zaidi vijiti.
 
Ni kweli huwa hawaziweki lakini unaweza kununua ya kwako ukawa nayo nyumbani sio mbaya, ukienda kwenye maduka ya dawa huwa wanakua nazo.
 
Back
Top Bottom