Elimu yetu Tanzania: Mbona International Schools hazina 'Holiday Package' kama shule nyingine?

Kisanduku

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2009
Posts
284
Reaction score
483
Shule zinakaribia kufungwa. Hii maana yake ni nini? Maana yake walimu wamefanya kazi wakamaliza syllabus wamefunzidha vizuri. Wanafunzi mwamesoma vizuri na wamesimamiwa vizuri.

Sasa wanaenda kupumzika kwa mwezi mzima. Ratiba ya shule imeisha inaanza ratiba nyingine ya nyumbani. Mtoto anahitaji kupumzisha akili. Mtoto anahitaji ku socialize na ndugu, majirani marafiki na wanafunzi wenzake toka nchi mbalimbali.

Kama anawea huu ni muda wa kwenda kuanglia tembo anafananaje kule Serengeti.

Kimsingi ratiba ya shule imeisha kwani ratiba ya mwalimu ni vipindi vyake vya darasani. MWalimu mzembe au shule yenye wazembe ndizo hupenda sana kupelekea mambo ya shuleni nyumbani.

Mojawapo ni hili kwamba sasa shule zinafungwa, badala ya mwanafunzi kupumzika wanamrundikia rundo la homework za likizo wanaziita "Holiday Package" na bila aibu zimefikia kiwango cha kutangawzwa mitandaoni.

TUmeuendekeza hadi umekuwa sehemu ya maisha.

Shule za Kimataifa, International Schools hazifanyi jambo hilo, wao wanahakikisha kila kitu mwalimu umemaliza ndani ya dakika 80 za kipindi chako. Shule hizi hukuti hata siku moja mtoto anapewa "Holiday Package" aifany wakati wa likizo, mwalimu wa namna hiyo akifanya anafukuzwa kazi.

Kumbe, hili "Holiday Package hazitakiwi bali ni uzembe tunaoundekeza kwa kushindwa kukagua yanayoendelea mashuleni.

Kinachosababisha ni kwamba baadhi ya wamiliki wa shule wanadhani kuwekeza kuwapata walimu wazuri ni gharama. Mwanzoni hawaajiri walimu wa somo fulani, ikiaribia ndipo wanaajiri. Au kama wamemuajiri utakuta walimu hawalipwi mishahara kwa wakati na wakati mwingine hawalipwi kabisa.

Mwalimu wa namna hiyo lazima ataandaa "Holiday Package" kwa wanafunzi wake, kwa sababu ya uzembe huo ambao hauwezekani kwenye international schools.

shule ziache uzembe, tuhimize kufutwa hizi "Holiday Package" ibaki kwa wale tu wanaozipenda.
 
Private (english medium) schools ni holiday package, serikali (kayumba) ni hakuna kufunga likizo, ni mitihani kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 12 jioni, walimu wanataka wanafunzi wafaul wasijepewa vinyago kama walivyopewa walimu wakuu wa shule za Arusha. Mtoto anakuwa anakariri tu, full kuchoka.
 
Kwa hiyo tunatengeneza taifa la watu wanaokariri.
 
Mleta mada shule ziko za aina tofauti kwa lengo moja mzazi aamue ampeleke mwanawe wapi

Kama hupendi hizo shule zenye holiday package hamisha mwanao peleka kwingine.Full stop na usiongee Tena kuwa shule ile ooh Wana holiday package wacha waendelee na yao na wewe na yako
 
Shule zinakaribia kufungwa. Hii maana yake ni nini? Maana yake walimu wamefanya kazi wakamaliza syllabus wamefunzidha vizuri. Wanafunzi mwamesoma vizuri na wamesimamiwa vizuri.

Sasa wanaenda kupumzika kwa mwezi mzima. Ratiba ya shule imeisha inaanza ratiba nyingine ya nyumbani. Mtoto anahitaji kupumzisha akili. Mtoto anahitaji ku socialize na ndugu, majirani marafiki na wanafunzi wenzake toka nchi mbalimbali.

Kama anawea huu ni muda wa kwenda kuanglia tembo anafananaje kule Serengeti.

Kimsingi ratiba ya shule imeisha kwani ratiba ya mwalimu ni vipindi vyake vya darasani. MWalimu mzembe au shule yenye wazembe ndizo hupenda sana kupelekea mambo ya shuleni nyumbani.

Mojawapo ni hili kwamba sasa shule zinafungwa, badala ya mwanafunzi kupumzika wanamrundikia rundo la homework za likizo wanaziita "Holiday Package" na bila aibu zimefikia kiwango cha kutangawzwa mitandaoni.

TUmeuendekeza hadi umekuwa sehemu ya maisha.

Shule za Kimataifa, International Schools hazifanyi jambo hilo, wao wanahakikisha kila kitu mwalimu umemaliza ndani ya dakika 80 za kipindi chako. Shule hizi hukuti hata siku moja mtoto anapewa "Holiday Package" aifany wakati wa likizo, mwalimu wa namna hiyo akifanya anafukuzwa kazi.

Kumbe, hili "Holiday Package hazitakiwi bali ni uzembe tunaoundekeza kwa kushindwa kukagua yanayoendelea mashuleni.

Kinachosababisha ni kwamba baadhi ya wamiliki wa shule wanadhani kuwekeza kuwapata walimu wazuri ni gharama. Mwanzoni hawaajiri walimu wa somo fulani, ikiaribia ndipo wanaajiri. Au kama wamemuajiri utakuta walimu hawalipwi mishahara kwa wakati na wakati mwingine hawalipwi kabisa.

Mwalimu wa namna hiyo lazima ataandaa "Holiday Package" kwa wanafunzi wake, kwa sababu ya uzembe huo ambao hauwezekani kwenye international schools.

shule ziache uzembe, tuhimize kufutwa hizi "Holiday Package" ibaki kwa wale tu wanaozipenda.
Mkuu maisha hayana holiday...kila aliefanikiwa hamalizi kazi zake zote ofisini.japo unaona kama hawana...ukichunguza wana (projects and assignments)....
Usizoeshe wanao kuwa kuna muda ambao mambo yote muhimu yanawekwa pose ili ale bata kwanza.....
Nina uhakika kuwa mtoto wako hasomi international school.

Shule unazolinganisha hazifanani,kwenye ufundishaji,mtaala,hadhi,sinyllabus na hata malengo ya elimu na kadhalika.kwa mfano kuna CBC ya English medium, CBC ya kiswahili,British Carriculum na Cambridge.....

Sasa wewe na Mimi watoto wetu wanasoma CBC ya kayumba alafu unataka waende na curriculum ambayo hata haitambui mitihani kama assessment ya uwezo wa mtoto.
Usikariri.

Mwalimu mkuu hapa.
 
I think wanangu watasoma kwa Raha sitataka ma too much homework enzi tukiwa tunasoma hapakuwaga na holiday package wala too much homework sikuhizi Hadi chekechea wanapewa homework inasikitisha sana
Watoto wa primary wa kipindi hiki kuna hatari ya kuja kupinda vibiongo, maana hilo begi limejaa macounter book mpaka mtu unashangaa kwani hakuna ratiba ya masomo kwamba leo madaftari gani yanahitajika?

Ni majanga taslim kwakweli.
 
Mwalimu mkuu,
Japokuwa response yako ina tone ya kejeli khna sehemu nitaziongelea.

Kwanza sijajizungumzia hivyo wanangu wanasoma wapi, hivyo siyo hoja humu.

Ila umeongelea curriculum nalo halikuwa jambo langu. Nilichoongelea ni uzembe wenu walimu kumaliza syllabus tena hiyohiyo ya Wizara.

Mmeweka vipindi hadi vinaitwa REMEDIAL lakini bado hamalizi syllabus.

Kama umemaliza syllabus una haja gani ya Holiday Package.

Umesema hata maofisini ni hivyohivyo, nakukubalia, ila bado ni uzembe vilevile.

Ukiwa kazini piga kazi maliza katika muda wako, zaidi ya hapo ni uvivu tu.

Ni kweli baadhi ya curricullum hazimpimi mtu kwa rundo la mitihani, nyinyi mnaita Question Bank. Hawa walisha research wakaona it was useless and they benefit and they are ruling the world.

Hivyo walimu pigeni kazi wakati wa vipindi vyenu vya darasani. Walipeni walimu mshahara wasihamehame.

Mathematics form 1 ina vipindi 231, sasa utavimalizaje kwa mwaka ukiendekeza uvivu.

Fuateni ratiba, full stop.

Mkuu maisha hayana holiday...kila aliefanikiwa hamalizi kazi zake zote ofisini.japo unaona kama hawana...ukichunguza wana (projects and assignments)....
Usizoeshe wanao kuwa kuna muda ambao mambo yote muhimu yanawekwa pose ili ale bata kwanza.....
Nina uhakika kuwa mtoto wako hasomi international school.

Shule unazolinganisha hazifanani,kwenye ufundishaji,mtaala,hadhi,sinyllabus na hata malengo ya elimu na kadhalika.kwa mfano kuna CBC ya English medium, CBC ya kiswahili,British Carriculum na Cambridge.....

Sasa wewe na Mimi watoto wetu wanasoma CBC ya kayumba alafu unataka waende na curriculum ambayo hata haitambui mitihani kama assessment ya uwezo wa mtoto.
Usikariri.

Mwalimu mkuu hapa.
 
Watoto wa primary wa kipindi hiki kuna hatari ya kuja kupinda vibiongo, maana hilo begi limejaa macounter book mpaka mtu unashangaa kwani hakuna ratiba ya masomo kwamba leo madaftari gani yanahitajika?

Ni majanga taslim kwakweli.
Ma Aunt zangu wanabeba ma counter mengi Hadi wanapindia chini Hasa hizi English medium, na hayo ma counter book ni mengi kuliko ni liyotumia olevel, Mimi primary nilitumiaga mda mwingi kwa kucheza sana na kusoma kiasi na nilifaulu watoto wa sikuhizi ni mwendo wa ma homework na hawajui kazi nyingine za nyumbani wako busy tu na madesa kitu ambacho ni hatari sana
 
Kwanza mimi O level enzi zetu kuwa na kitabu ni deal, sasa mimi kuna masomo nilikuwa na vitabu sikujisumbuwaga kuandika notice kujaza madaftari bila sababu.
 
I think wanangu watasoma kwa Raha sitataka ma too much homework enzi tukiwa tunasoma hapakuwaga na holiday package wala too much homework sikuhizi Hadi chekechea wanapewa homework inasikitisha sana
Hayo madubwasha Yana DUMAZA UBONGO WA WATOTO ila tukisema tutapingwa na wazazi wasio elewa
 
Back
Top Bottom