Ni ngumu kumeza hii, huyu Mkenya anataka kufanya kitu ambacho hakiingii akilini, sijui nini anawaza muda huu, neno 'badass' litapata maana na tafsiri mpya leo.
Mbio zenyewe ataanza 09:15am
Kwa watani wetu wa Kusini, ili kuwapa picha ya umbali anaokimbia chini ya masaa mawili, ni kama kutoka Dar hadi Mlandizi, kwa ndugu zangu hapa Kenya hiyo ni kama kutoka Nairobi hadi Lari.
TV nyingi duniani zitapeperusha moja kwa moja mubashara, hata zetu hapa Kenya naona zimeweka live, anajadiliwa kitaani nyumba kwa nyumba. muhimu sana maana inawapa hamasa vijana wengi kwamba linawezekana na itawezekana.
Pia kampuni ya Youtube inapeperusha mubashara