Eliud Kipchoge avunja rekodi yake mwenyewe na kuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia KM 42 kwa chini ya saa 2

Eliud Kipchoge avunja rekodi yake mwenyewe na kuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia KM 42 kwa chini ya saa 2

20191012_112441.jpg
20191012_112441.jpg
 
Thank God. Congrats Eliud. You make us proud to be Kenyans.
 
Ni ngumu kumeza hii, huyu Mkenya anataka kufanya kitu ambacho hakiingii akilini, sijui nini anawaza muda huu, neno 'badass' litapata maana na tafsiri mpya leo.
Mbio zenyewe ataanza 09:15am
Kwa watani wetu wa Kusini, ili kuwapa picha ya umbali anaokimbia chini ya masaa mawili, ni kama kutoka Dar hadi Mlandizi, kwa ndugu zangu hapa Kenya hiyo ni kama kutoka Nairobi hadi Lari.
TV nyingi duniani zitapeperusha moja kwa moja mubashara, hata zetu hapa Kenya naona zimeweka live, anajadiliwa kitaani nyumba kwa nyumba. muhimu sana maana inawapa hamasa vijana wengi kwamba linawezekana na itawezekana.

Pia kampuni ya Youtube inapeperusha mubashara

Kutoka Dar mpaka Mlandizi ni km 55.

Get your facts right.
 
Kutoka Dar mpaka Mlandizi ni km 55.

Get your facts right.

Short of a paltry 12km, pia kumbuka nimetumia neno 'ni kama', ni vile sikuweza kukumbuka wapi panafahamika Tz na pana umbali wa kilomita 42km exactly.
 
Taarifa ya mbio za marathon kule Vienna zimetangazwa takriban kwa wiki sasa. Mashindano haya walitaka mkimbiaji yeyote avunje rekodi kwa kukimbia kilomita 42 kwa muda usiozidi masaa mawili juu ya alama. Iliwabidi watayarishaji wamkodie ndege mkimbiaji aliyewahi kukimbia umbali huo wa 42 kwa muda wa 2:02:1 ambaye anaitwa Ndugu Eliud Kipchoge wa Kenya kama kweli anaweza kuvunja rekodi hiyo ili jina lake liweze kuingia katika vitabu vya Guinnes. Leo katika kuithibitishia ulimwengu amevunja rekodi hiyo kwa kukimbia kilomita 42 kwa muda wa 1:40:2 na hivyo kufanya jina lake kuingia katika vitabu vya guinnes. Hili ni funzo kwetu kama Watanzania. Tuwekeze kwa akina Simbu ili majina yao yaje yatambuliwe dunia nzima kama ilivyo Eliud Kipchoge.
 
Jamaa noma sana na miaka yake 34. nimeikosa hiyo kitu live, nilchanganya nikajua ni kesho
Kumbe tayari imeisha
 
Hili jukwaa halihusiani na mambo ya siasa bhana, peleka kwenye majukwaa ya siasa huko
 
CONGRATULATIONS TO ELIUD KIPCHOGE CLOCKED @ 1:59:40
 
Tetesi za dawa pia zikianza usiache kutuarifu
 
Back
Top Bottom