Eliud Kipchoge avunja rekodi yake mwenyewe na kuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia KM 42 kwa chini ya saa 2

Eliud Kipchoge avunja rekodi yake mwenyewe na kuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia KM 42 kwa chini ya saa 2

Kenya wametuzidi. Kipindi kile Kenya vs Tanzania mpira ulikuwa unaoneshwa KBC lakini hapa TZ, hola. TBC na zingine wapo busy na mambo yao. KBC imerusha live hili tukio toka Viena ingekuwa bongo sidhani kama ingeoneshwa live. Sasa hivi Safari Tanzania imekuwa ya kisiasa, inatangaza mambo ya kupiga kura, sijui ukajiandikishe. Ila tukio lilonishangaza sana Kenya ni lile la Odinga kuapishwa kama raisi halafu polisi wanalinda usalama wa raia mpaka zoezi likaisha kwa amani na mwisho wa siku Kenyata na Odinga wanakutana ikulu kuzungumza. Ingekuwa bongo, huyo Odinga sijui angekuwa wapi leo maana angeshitakiwa kwa kesi ya uhaini. Kenya wanajitambua
Hongereni Kenya
1:59:40
 
EGqi7dXWwAAOFFn.jpg
EGqfi2GW4AU7oQ6.jpg

GOAT
 
Huyu kwanini msiseme ni kutoka "East Africa", au East Africans ni Diamond na Alikiba na Harmonize tu lakini ikifika upande wa wakenya kufanya vizuri hakuna EAC?.

Tukikataa EPA, free movement of people and businesses, hapo ndio mnaikumbuka EAC kwasababu inawaumiza. Ubinafsi na kupenda sifa ndio ugonjwa wenu.
Kwani unataka aitwe mtanzania? Wewe bwiji sana
 
Hiyo ndiyo kenya bwana, ingekuwa tanzania wangesema kakimbia kuunga mkono juhudi
 
42 km kwa masaa mawili....

Yaaan atakimbia km 21 kwa lisaa limoja,au 21km kwa dakika 60

Ni sawa na kusema atakimbia km 0.35 kwa dakika moja

Hii pia ni sawa tu nikisema atakimbia mita 350 kwa dakika moja

Pata picha tu...dakika moja huyu jamaa anakuwa kakimbia umbali sawa na viwanja vya mpira vitatu na nusu

Zaidi ni sawa na kusema atakimbia mita 5.8 kwa sekunde moja!!

Hehehehe, mita 5.8 kwa sekunde!! yetu macho,ngoja tusubili tujionee

Prophets of doom washapewa aibu. Kabla ya leo ungefaa kujua kwamba alibakisha tu sekunde 26 kutimiza hii ndoto, rekodi ambayo pia aliweka yeye mwenyewe. Chuki ni kitu mbaya sana
 
Taarifa ya mbio za marathon kule Vienna zimetangazwa takriban kwa wiki sasa. Mashindano haya walitaka mkimbiaji yeyote avunje rekodi kwa kukimbia kilomita 42 kwa muda usiozidi masaa mawili juu ya alama. Iliwabidi watayarishaji wamkodie ndege mkimbiaji aliyewahi kukimbia umbali huo wa 42 kwa muda wa 2:02:1 ambaye anaitwa Ndugu Eliud Kipchoge wa Kenya kama kweli anaweza kuvunja rekodi hiyo ili jina lake liweze kuingia katika vitabu vya Guinnes. Leo katika kuithibitishia ulimwengu amevunja rekodi hiyo kwa kukimbia kilomita 42 kwa muda wa 1:40:2 na hivyo kufanya jina lake kuingia katika vitabu vya guinnes. Hili ni funzo kwetu kama Watanzania. Tuwekeze kwa akina Simbu ili majina yao yaje yatambuliwe dunia nzima kama ilivyo Eliud Kipchoge.
Ni 1:59:20
Kuwa mwangalifu na takwimu.
 
Kumbe ataandika historia na sio kuvunja rekodi....na hii ni kwasababu anakimbia mwenyewe na pia uwepo wa pacemakers ambao wanaingia na kutoka. Ila all in all inatuweka vizuri wanaafrika mashariki kwenye uso wa dunia hususan kwenye michezo.
Niambie ni rekodi gani ilishawekwa yenye anavunja leo na uliwekwa na nani
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Aiseee dahh ni sheedah mazeee...jamaa anatupiga promo ya hatareeeee, ila dah kwa wenzetu naona safari tv inawaonesha wahdzabe wakikula kobee!![emoji16][emoji196]
 
hongeraaa Eliud Kipchoge kwa mbio hizooo, well done

...sie twawaza kimbizana viunoniniii tuuuu...adi kwenu tushafikaaa...
 
Back
Top Bottom