Elizabeth, kabla ya kifo chako uliwahi kuwaomba msamaha watu weusi?

Elizabeth, kabla ya kifo chako uliwahi kuwaomba msamaha watu weusi?

Waandishi wa vitabu vingi vya historia wengi wameandika upotoshi na uzushi mwingi sana Ili kuwabrainwash waafrika wajenge chuki pia ni kama njia za watawala wa kiafrica kujifichia kutupa lawama juu ya kushindwa kwao kuwaletea waafrika maendeleo.
Kutawaliwa sio kizuizi cha nchi kutokuendelea
Ukweli mchungu!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biashara ya watumwa wasilaumiwe wazungu pekee hata mwafrika akwepi lawama hii. Mzungu wala muarabu akuingia field vijijini kukamata watu bali Kazi hii ilifanywa na waafrika wenzetu wakiwemo machief, ndugu nk. Kama mwafrika anatolewa congo kwa escot ya watu sita wakiswaga rundo la watu kwa miezi huku wakipita vijijini na wanavijji wakiwaaangalia tu wenzao wanaswagwa bila hata kuwasaidia kwa kuwaua hao wafanyabiashara na kuacha wenzao waafrika waswagwe hadi Pwani. uoni kwamba mwafrika nao ni sehemu ya lawama.
Mbona wamasai na wakurya wao awakuchukuliwa utumwani.
High iq[emoji3581][emoji3581]
 
Japo kwa cheo QUEEN ELIZABETH wewe ulikuwa malkia kwa maana kiongozi hakosei.

ila kwa upande wengine tukitoa cheo chako wewe Elizabeth Alexandra Mary Windsor ulikuwa ni binadamu kama binadamu wengine.

na japo kosa haukulifanya wewe walifanya watu wengine ila ungetudanganya basi hata kwa neno samahani tu.

Maana mtoto anapokesea nje na kwao watu aanza kuuliza yule ni mtoto wa nani na sio yule ni nani

Habari zenu wapendwa pia poleni na msiba wa kiongozi wenu. ila bado tunawakumbusha tunawadai na tutaendelea kuwadai

Hili lipo wazi kabisa japo kuwa hadhani masikio yenu hayataki kusikia aya maneno (Ukweli ambao hatumatiki kuisikia).

Ukisiliza nyimbo ya Bob Marley " Buffalo soldiers" basi kuna vitu vingi sana utajifunza .

Kuna mstari unasema

"If you know your history then you would know where you coming from "

Kwa maana ya uo mstari kinyume chake kama haujui unatoka wapi basi pia hauwezi kujua historia yako.

Kauli ya kiongozi wa kambi ya upinzani Africa kusini Bwana Julius Malema naomba usitafsiriwe kama chuki au hajielewi ni kauli safi kabisa.

Ila kama unatumia hisia kwenye tukio linalotakiwa kutumia akili hauwezi kumuelewa Julius malema.

"We do not mourn the death of Elizabeth, because to us her death is a reminder of a very tragic period in this country and Africa's history.... If there is really life and justice after death, may Elizabeth and her ancestors get what they deserve."

Hii kauli unaweza kusema imebeba chuki kwa watu weupe ila hiyo kauli haijatoka kwa mtu ambae ajielewi. nadhani julius malema alikuwa anajua anasema nini na pia anaijua historia ya afrika juu ya waingereza.

Turudi kwenye historia karne ya 17.

Mwaka 1619 meli ya kwanza ilifika katika katika Amerika ( Virginia) na ilikuwa na waafrika ambao walikamatwa na maalamia wa kiingereza kutoka pwani ya Mexico . waafrika ao walikuwa wametoka kwenye meli ya watumwa iliyokuwa inamilikiwa na Wareno.

Meli hiyo ilikuwa imebeba waafrika 350 kama watumwa sio abiria . ambao walitokea Angola na wengi wao walikuwa wamekufa njiani kutokea ndani ndani na hata wengine walikufa ndani ya meli wakiwa safarini miili yao ilitupwa baharini.

Walikufa kutokana na mazingira magumu na waliobaki hai walienda kuuzwa huko Amerika na ulaya ya Magharibi. Waafrika ao walitumika kama wafanyakazi wa ndani wengine walipelekwa mashambani.

Hizi safari za watumwa zilianza karne ya 16 hadi 19 na zilikuwa safari za kulazimishwa hakukuwa na muafrika hata moja aliyetaka kwenda ulaya na amerika kufanyishwa kazi bila malipo na kuwekwa mazingira kama mnyama.

Ambapo biashara hiyo alichukua takribani watu Million 12 wakiwemo Wanaume , wanawake na watoto

Lakini mnamo karne ya 17.

Ndani ya Ulaya inazaliwa sera ya Mapinduzi ya kilimo (Agriculture revolution) ni bidhaa ghali zaidi inajulikana ni sukari.

Na sukari kwa karne hiyo ndo ilikuwa bidhaa yenye thamani zaidi ulaya .

Muingereza anagundua ardhi nzuri yenye kutoa miwa mizuri ni ile ya pale caribbean. lakini binadamu wenye rangi nyeupe inakuwa ngumu kuishi mda mrefu kutokana na mazingira.

Wanachukuliwa watu weusi wanaenda kulimishwa miwa ndani ya caribbean ambapo msanii maarufu wa kike duniani Rihanna alipozaliwa.

Mtu mweusi (mtumwa) anaenda kulimishwa sehemu ambayo kiufupi yeye hana maslahi napo anayeenda kufaidika ni Muingereza.

Sina mahana mbaya na wala musitoe tafsiri mbaya. Mnufaika namba moja wa kilimo cha caribbean ilikuwa ni Familia ya Kifalme ya pale nchini Uingereza.

Kwa kipindi hiko life expectancy ya binadamu walikuwa wanaishi hapo ilikuwa ni miaka 18 tu sasa vuta picha leo hii Tanzania life expectancy yetu ni miaka 66. 08 ( 2022) kwa report ya World bank

Hayo tufanye hayapo ni ya miaka mingi sana yamepita

Twende 1915- 1918

Zaidi ya Wamarekani weusi 380,000 walihudumu katika Jeshi wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia.

Wanajeshi Waafrika milioni mbili waliuawa atika vita ya pili ya dunia pia 1939-1945.

bahati mbaya Waafrika wamekuwa hawatajwi sana katika historia rasmi za vita ya pili ya dunia. Ingawa wengi walilipwa, wengi wamesahaulika kabisa.

Wanajeshi 15,000 wa Kiafrika walipoteza maisha yao wakipigania Uingereza.

15, 000 ndio waliokufa . je unaweza kujiuliza ni wangapi walirudi na ulemavu

Na je, vita hiyo inawahusu nini waafrika wakati vita ilikuwa ni ya watu weupe kwa weupe.

Wanajeshi wao walipigana vita wanawatunza na kuwapa mahitaji mazuri, ila wazee wetu ambao walipigana vita kwa faida zao wapo na wengine washakufa hakuna walichofaidika nacho zaidi ya kulalamika tu na kutupa historia ambazo kiufupi hatuna faida nazo yoyote.

Sasa ni mda wa uingereza kuiomba samahani Afrika kwa yote waliyoyafanya au musituombe samahani tuendelee kuwapa lawama na musituone wabaya mukae kimya.

Kama hipo video inayomuonesha kiongozi wa ulaya akiiomba samahani Afrika naomba munitumie

Na kama haipo basi Samahani iusike mara moja sio samahani ya maneno na vitendo vionekane.

Leo hii julius Malema kauli yake imetoka baada ya kujijua yeye ni nani ila wanaompinga julius Malema ni wale ambao hawajui historia yao.
Ni lin mwafrica aliwah kuwa huru hadi hizo monarch ziombe msamaha? Tuanzie hapo kwanza
 
Yawezekana aliomba au pia hakuomba.

Njaa yetu nayo inachangia kudharaulika.

Huyo huyo mtamwita mbaya huyo huyo anawakopesha, utakuwa na nguvu gani za kumlaumu
 
Inasikitisha sana
Kulialia hakuwezi kukupa muongozo, 60 years baadae ya ukoloni Bado unajisaidia porini, wanafunzi wanakaa chini mama mjamzito anakufa Kwa kukosa huduma halafu unawalaumu waingereza FOOL
 
Wachina na Wakorea Kusini wenyewe pia wamewahi kuwa watumwa wa Japan hapo karibu kabisa karne ya 19 na 20.
Hakuna ukweli wowote maana utumwa ni human nature shukuru hao wazungu wameukomesha... Afrika tu utumwa ulikuwepo hata kabla ya kuja wazungu... Babu zako wa Tabora wamekuwa wakinunua na kuuza weusi wenzao wakati wa long distance trade na warabu
 
Uko sahihi
Dunia haiko fair.
Binafsi nadhani ni mihemko kumwaga chuki mtandaoni dhidi ya bidada Eliza.

Waafrica tumenyanyasana sana baada ya utawala wa hawa watu kiasi sioni tofauti yoyote.

Hebu tuombane misamaha sisi kwa sisi halafu baada ya hapo tudai misamaha kutoka ughaibuni.


Aibu zetu.
 
Hawa ni wazalendo weusi uchwara.
Hao wazungu ndiyo walioenda Tripoli au Misrata kuanzisha maandamano? Kwani Ghadaf alikuwa Rais wa kwanza kupinduliwa na kuuawa na watu wake? Madikteta wote hufa in the same way, kuanzia Samwel Doe. Sami Abacha nawengine vifo vyao vilikuwa ni Kama stori tu.
 
Back
Top Bottom