Elon Musk: China inavutia sana. Ninawahimiza sana watu kutembelea huko

Kuvutia sawa ila kuwa ndoto ya wengi hapana. Life gumu sana China graduate waliokuwa boda boda ni wengi mno.
China sio sehemu salama kwa wawekezaji wa uraia wa nje, hili ndio jambo ambalo pro china hawataki kulizungumzia, china imejengwa kwa misingi ya kuwafaidisha wachina pekee, ndiomaana kila fursa ambayo mchina anaiweza wanamjaza mchina hata kwa makampuni yanayo operate nje ya China, wapo tayari kuwatoa vifungoni hata wafungwa lengo tu wakajazie nafasi za kazi ktk makampuni yanayochukua tender kwa nchi za nje.

China ni best economic partner ambaye huvutia upande wake pekee lkn watu hawalioni hili wako bize kumchongea mmarekani kwamba ni muhuni, wanasahau kuwa china ndio Muhuni nambari moja hapa duniani

China hata akija nchini kwako kujenga barabara hatoishia kuijenga tu atabeba madini na kuchukua mpaka kazi za uchuuzi wa bidhaa ndogo ambazo ni sehemu ya raia wazawa wa nchi, yaani anapita na kila hela bila uoga wala huruma.

China ni mkoloni mpya ambaye asipodhibitiwa mapema ataiharibu hii dunia.
 

Nikinunua 10HP ya China for 2M hata ikifanya kazi 6 months tu ikaungua inakua imenilipa. Naitupa kabisa sitafuti fundi wala nini.
 
Nimekuelewa sana mkuu 👊
 
Yani nchi nguchiro ndio utalii.!?

Mazafanta

Kama wanataka Tech Isiwe habari ya mjini wasitumie sarvaival mode kujipata
 
Unafikiri bidhaa zao wanazopeleka nchi za playa na marekani ubora wake ni kama wanazoleta huku?...besides huku migodini asilimia 90 ya vifaa tunavyotumia vinatoka china,magari makubwa ya kichina ndo yanaweza kuhimili huku porini gari za ulaya huku haziwezi kabisa!...sasa kama musk anaisifia china wewe unatuletea hadithi za zamani!
 
Malori mengi yanayotumiwa kwenye migodi ni za China na hii ni kwa sababu ya gharama ndogo japo kwa economic life hayana muda mrefu ukilinganisha na yale ya nchi za magharibi ambayo ni ghali sana hata kwa service.

Nimeona kwenye migodi mingi mikubwa majenereta ya kuzalisha umeme na pampu za kuvutia maji na hata vifaa vingine vya kutumia umeme vya kichina hawavitaki kabisa kwa sababu vina kawaida ya kusababisha ajali.

Kiuhalisia China bado ni nchi ya dunia ya tatu inayokua na ndio maana bidhaa zake bado hazina ubora wa kimataifa na ndio maana ni vigumu sana kukuta bidhaa yao iliyo na manufacturer's warranty.
 
Mchina anakutengezea bidhaa kutokana na pesa yako na hata hivyo inakua bei nafuu kulinganisha na nchi nyengine japokuwa ubora unakua ule ule mchina atabaki kua namba moja
 
Wewe inaonekana hata mambo ya magari hujui kabisa ni wale watu wa kukariri kariri tu.
 
Mama yake na Elon Musk anayeitwa Maye Musk naye kakubaliana na mwanae.

Unajua kwa nini?

Maye amekuwa akiishi na kufanya biashara zake Shanghai kwa miaka kadhaa sasa, amejionea ukweli huo
​
Yule bi-mkubwa she's brain kinyama
 
Umewajaribu hawa NTGD Pump Co., Ltd
 
Swali ni moja tu: Kama China imeweza kubadilika kwa kasi hii ndani ya miongo michache, Afrika na mataifa mengine duniani yatachukua muda gani kuamua kuingia kwenye njia hiyo ya maendeleo? China ni somo kubwa la maendeleo kwa dunia.
Ukifuatilia historia ya China kuanzia kwa Den Xiaoping na crew yake mfano huyu former premier aliefariki juzi kati unaona kabisa nchi ili iendelee inahitaji cream fulani ya viongozi wenye maono na uzalendo otherwise kama taifa mtapiga mark time tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…