Elon Musk: China inavutia sana. Ninawahimiza sana watu kutembelea huko

Elon Musk: China inavutia sana. Ninawahimiza sana watu kutembelea huko

America alirejesha asilimia kubwa ya viwanda vyake tena America
Baada ya hilo mbona China ndipo inazidi kuwekeza zaidi kwenye teknolojia za semiconductors, robotics, magari ya umeme ,battries n.k kiasi kwamba hivi sasa wanashindana na makampuni ya US, Japan na EU...

Mi naona hawajaikomoa China, wamempiga chura teke..

Kuna viwanda vimeenda Mexico na vingine nchi za Asia zenye gharama ndogo ya maisha kama Vietnam.. hapo lengo ilikuwa kuidhoofisha China.. lakini haijasaidia..

Unatoa kiwanda China unakipeleka Mexico ama Vietnam, kwanza umeingia gharama kuhama na bado hakuna faida iliyopatikana zaidi ya serikali kuikomesha China...
 
Baada ya hilo mbona China ndipo inazidi kuwekeza zaidi kwenye teknolojia za semiconductors, robotics, magari ya umeme ,battries n.k kiasi kwamba hivi sasa wanashindana na makampuni ya US, Japan na EU...

Mi naona hawajaikomoa China, wamempiga chura teke..

Kuna viwanda vimeenda Mexico na vingine nchi za Asia zenye gharama ndogo ya maisha kama Vietnam.. hapo lengo ilikuwa kuidhoofisha China.. lakini haijasaidia..

Unatoa kiwanda China unakipeleka Mexico ama Vietnam, kwanza umeingia gharama kuhama na bado hakuna faida iliyopatikana zaidi ya serikali kuikomesha China...
Na bado hivyo viwanda vinaagiza critical components kutoka China ili vizalishe
 
Braza sijui hata kama ushawahi fika mataifa haya mawili...
Marekani anaizidi china kwa uhuru wa watu wake tu kwa sasa na uwezo wa kushawishi nchi washirika katika vikwazo,japo hili dawa yake muda si mrefu itapatikana ...


Siku china akiziweka nchi za kiarabu mfukoni jeuri ya marekani kweshnei..

Anamzunguka Marekani mdogo mdogo bila vita kwa bidhaa za viwandani...Now ndio muwekazaji mkubwa amerika ya kusini....
Mimi huwezi kunidanganya kuhusu Marekani kwa sababu nimewahi kuishi huko labda China ndio sijafika.

China kamwe haitaweza hata siku moja kuwa na ushawishi iliyonayo Marekani kwa sababu ni nchi ambayo imekaa kiimla zaidi, watu wa kizazi cha sasa duniani hawapendi uimla.

China hata ielewane na mataifa ya kiarabu haina shida kwa sababu Marekani inaagiza asilimia 8 tu ya mafuta kutoka mashariki ya kati ambayo ni crude oil medium sour grade. Most U.S. output is light sweet crude, whereas some few regional refineries are built specifically to run heavier, medium sour grades.

Hivyo hoja yako kwamba siku sijui China ikiziweka nchi za kiarabu mfukoni eti ndipo jeuri ya Marekani itaisha haina msingi.
 
China ina cheap labour sababu wana purchasing power kubwa, si kwa sababu ya umasikini... are you serious unasema China ni masikini? China ina nyumba milioni zaidi ya 90 ambazo hazina watu.. zipo sehemu tofauti wanaita ghost cities... hio nyumba kwa Tanzania ni apartment ya kiwango. Unasemaje ni nchi masikini...
Hawa hawa ambao vijana wao wapo hapa wengi wanafanya umachinga na kuuza bidhaa feki.
 
Kuna kitu unashindwa kuelewa bwana mdogo

Makampuni mengi makubwa ya uchimbaji madini yanayoinyonya Tanzania ni ya Magharibi

Wananunua machines na equipments za makampuni ya mataifa yao

Ni kama vile tu Civil Companies za China zinavyotumia heavy duty machines za China kwenye projects zao

Nenda kwenye projects za China popote duniani ukajionee mitambo ya China inavyofanya kazi
Kwanza elewa kwamba mimi sio bwana mdogo angalia profile yangu uone nina umri gani kwani sijaficha kitu na inawezekana hata baba yako akawa mdogo wangu.

Wewe mbona hujui unachokiongea, makampuni ya nchi za magharibi yanainyonya Tanzania kivipi? Kwani hawalipi kodi au hawalipi mrahaba...!!!???

Unafahamu utaratibu wa uwekezaji kwenye sekta ya madini ulivyo au unajisemea tu. Je, nchi gani sasa hiyo ambayo imejiwekea sheria za uwekezaji kwenye sekta ya madini inayo ruhusu inyonywe.

Be serious and factual when commenting on critical issues in this forum.
 
"China is awesome. I strongly encourage people to visit."
— Elon Musk

View attachment 3648262​

Hii ndiyo kauli ya Elon Musk kwenye ukurasa wake wa X (Twitter), mtu ambaye si mtazamaji wa mbali bali ni mfanyabiashara mwenye uwekezaji mkubwa China kupitia Tesla Shanghai gigafactory

Musk ameiona China kwa macho yake: kutoka teknolojia ya hali ya juu, viwanda vinavyofanya kazi kwa kasi ya ajabu, hadi uwezo wa kujenga miundombinu mikubwa ambayo mataifa mengi yanaweza kuota kwa miongo.

China leo ni mshindani mkubwa kwenye magari ya umeme, betri, roboti, akili bandia (AI), treni za mwendo kasi na teknolojia ya kizazi kipya

Wakati baadhi ya watu bado wanaijadili China kwa picha za zamani, China ya sasa inaonyesha sura mpya: miji ya kisasa, barabara na reli za kiwango cha dunia, viwanda vikubwa na vijana wanaoongoza ubunifu wa teknolojia

Ndiyo maana Elon Musk anasema watu waende wakaione wenyewe


Swali ni moja tu: Kama China imeweza kubadilika kwa kasi hii ndani ya miongo michache, Afrika na mataifa mengine duniani yatachukua muda gani kuamua kuingia kwenye njia hiyo ya maendeleo? China ni somo kubwa la maendeleo kwa dunia.
​
Swali muhimu mkuu. Si ndo hawa hawa wachina wamagharibi waliponda na propaganda kibao duniani eti ukomunisti unakandamiza kikaenda kikarudi, hadi kuunda duniani itikadi kuu mbili - ubepari na ukomunisti.
Leo hawa wakomunisti ni matajiri dunia nzima umma ukifaidika na kukua kimaendelea kila kizazi!🤔.
Na yule mkomunisti mwingine mruskie nae anapaa mtindo mmoja... du
basi bhana ndo ulikuwa mfumo - west vs east, magharibi au mashariki hata mashuleni na vyuoni tulikaziwa, mwiko huruhusiwi kuchanganya mazuri ya kote, lazma uikane moja, aisee...
😳afu sirikali zetu zilienda na upepo :3Dance:

wachina tukumbuke walikotokea, na wakatembea mwendo mdo mdo ila endelevu kila kizazi kikifanya yake ila endelevu kupokelewa na kuendelezwa na kizazi kichajo...
waliwahi kejeliwa mbaya ka nchi maskini, washamba nk, wajua ya mdhungu ila nidhamu yao haikuterereka. Sawaa kuna wakati nidhamu na viboko vimehusika... Wazee wao waliendesha baiskeli na kulima mashambani, vijana wao wakaendesha pikipiki wakiwa viwanda vidogo na vikubwa wakimtengenezea bepari flani vifaa na nguo hadi chupi - wakinufaika elimu ya viwandani na ndio dizaini mbele yao..., sasa kizazi ni wasomi balaa, wanajenga na kutengeneza maajabu ya kiteknikia na wanaendesha bonge za magari ya kila dizaini --ndani ya labda vizazi vitatu ama vinne. Mbinu zenyewe tajwa za usafiri zinaoneka endelevu na ajira ongezeko - viwanda na kwingineko.
Hawa jamaa, wachina, mwaka Tanzania inapata uhuru 1961, tulikuwa pamoja ndani ya listi orodha ya nchi maskini duniani. Kuna Singapore, pia kwa kuchunguza niaje manake maendeleo murua kipindi hiki hiki ss tushapata uhuru.


Binafsi, naona siasa si sihasa, wachina nidhamu na dhamira vilishindiliwa kiumoja na kutekelezwa endelevu hadi kufikia sasa; kila kizazi kikiwa na sehemu yake na mchango wake. ENDELEVU na Nidhamu ya pamoja ndo ishu mzima - uwe umechagua au kulazimishwa, almuradi nidhamu na maendeleo endelevu. Pia ni nchi kubwa yenye watu wengi.

Hapo ndo kasheshe kwa nchi zetu za kibantu... Hiyo nidhamu hutokea kwa nadra na kuzimwa chap... ndo kina Sankara, Raisi Magu hadi kina Ibrahim Traore leo... tatizo hawa wazuri ni wa nadra, wakichomoshwa, anakuja mkoloni mweusi alishanunuliwa kitambo. Kalipwa auze nchi na kuinyonya juu yake, na hata ahadi akijisikia akandamize watu wake hata kikatili watamfumbia jicho... afu hawa ndo wanadumu ka BIA ya kikameruni na kahawa za kule kanda ya ziwa (ndefu na fupi)...i🤔kwa leo hii dalili za bongo na nchi kadhaa kwenda kihivo ni asilimia finyu. Kwetu tunahitaji Uhuru wa siasa na vyombo vya habari kwanza - wananchi kuwa huru ndo msingi wa umoja wa nia moja.
Swala ndo what's next. Na nchi zetu zaeza fuata nyayo, kwa mfano za mchina? pa kulima papo, uvumilivu upo? vizazi kujitolea muhanga kwa lengo endelevu upo?
 
Braza sijui hata kama ushawahi fika mataifa haya mawili...
Marekani anaizidi china kwa uhuru wa watu wake tu kwa sasa na uwezo wa kushawishi nchi washirika katika vikwazo,japo hili dawa yake muda si mrefu itapatikana ...


Siku china akiziweka nchi za kiarabu mfukoni jeuri ya marekani kweshnei..

Anamzunguka Marekani mdogo mdogo bila vita kwa bidhaa za viwandani...Now ndio muwekazaji mkubwa amerika ya kusini....
China ni jambazi anachomfanya North Korea Dunia inabidi iingilie kati.

Ananufaika na vikwazo vya North Korea kwa 100%.

Bidhaa zote za North Korea zinapitia China.

Wafanyakazi wa viwandani wana tokea North Korea.

Hivyo North Korea akipunguziwa au kuondolewa kabisa vikwazo China itaanguka.

Huo Uchumi wa China in reality ni backup ya Uchumi wa North Korea.
 
China ni jambazi anachomfanya North Korea Dunia inabidi iingilie kati.

Ananufaika na vikwazo vya North Korea kwa 100%.

Bidhaa zote za North Korea zinapitia China.

Wafanyakazi wa viwandani wana tokea North Korea.

Hivyo North Korea akipunguziwa au kuondolewa kabisa vikwazo China itaanguka.

Huo Uchumi wa China in reality ni backup ya Uchumi wa North Korea.
Are you mad ?
 
Mchina anakutengezea bidhaa kutokana na pesa yako na hata hivyo inakua bei nafuu kulinganisha na nchi nyengine japokuwa ubora unakua ule ule mchina atabaki kua namba moja
Hili waga watu wamekaririshwa tu lakini hua ni uongo mtupu.
 
China bado wana kazi kubwa sana ya kuja kutengeneza bidhaa bora na zenye uimara kama nchi za magharibi zilivyokuwa zikitengeneza wakati China ikiwa bado wachoma mahindi.

Juzi tu kuna kampuni moja ya China ilikuwa inaniomba niwatafutie soko la Submersible Water Pumps hapa Tanzania hasa kwenye migodi lakini nikawaambia ni vigumu sana kwa pampu za kichina kushindana na zile za nchi zilizoendelea kama Franklin Electric (USA); Wilo (Germany); Grundfos (Denmark); Zylem (USA); Tsurumi (Japan); DAB (Italy); Godwin (England) or Sulzer (Switzerland) because all this have two to three years warranty which the Chinese pumps conspicuously lack.

Nina mifano mingi tu kuhusu bidhaa nyingi za China na changamoto zao za ubora.
Na hapo ndio tofauti inapokuja, mzungu mzungu tuu
 
Back
Top Bottom