Ile hotel ina matatizo gani mbona haifunguliwi? Agip Hotel nayo imekuwaje?Wadau siku ya Tatu sasa napita eneo hili naona mafundi wakichomelea bodi ya gari(Lori).
Ina maana ssasa ni karakana rasmi kwa kazi hiyo!?
Tujuzane jamani!
Okei, kapatikana mzawa tena.kuna Wawekezaji Wazawa walinunua Embassy Hotel but awana pesa ata za kumalizia deni na ata la kuwalipa mafao wafanyakazi wake.
ununuaji similar na ule wa UDA na Simon Group.
hoteli embassy jengo lao limeuzwa na wanataka kubomoa kujenga jengo jipya ni miaka mitano na zaidi tangu habari isambae kuwa jengo lililopo kuwa litabomolewa kujengwa upya. na agip nayo hivyo hivyoUkitembelea maeneo ya posta hapa Dar zipo hoteli 2 zilizowahi kuwa maarufu sana za Embassy Hotel na Motel Agip. Huko Moshi pia kuna Moshi Hotel nayo inaoza katikati ya mji.
Cha kushangaza zimefungwa karibu mwaka wa 20 sasa na haziuzwi wala hazitafutiwi mwekezaji na serikali ambayo naamini ndio wamiliki.
Je hii sio hujuma?
Je ni Hazina, wizara ya biashara au wizara ya maliasili na utalii?
Anayejua tafadhali aseme hili swala likoje?