Embassy Hotel na Motel Agip: Nini hasa kilitokea?

Embassy Hotel na Motel Agip: Nini hasa kilitokea?

Wadau siku ya Tatu sasa napita eneo hili naona mafundi wakichomelea bodi ya gari(Lori).

Ina maana ssasa ni karakana rasmi kwa kazi hiyo!?

Tujuzane jamani!
Ile hotel ina matatizo gani mbona haifunguliwi? Agip Hotel nayo imekuwaje?
 
Agip ndiyo walikuwa wanafanya biashara ya mafuta na Idd Dadaa wakati tunamtandika, siyo ? Au nimewafananisha !
 
Hii motel agip si ndo ilikuwa na parking ya magari kwa juu? Nakumbuka bi mkubwa alikuwa anatupeleka kunywa soda miaka hiyo, viwanja vyake vilikuwa motel agip na makondeko
 
kuna Wawekezaji Wazawa walinunua Embassy Hotel but awana pesa ata za kumalizia deni na ata la kuwalipa mafao wafanyakazi wake.
ununuaji similar na ule wa UDA na Simon Group.
Okei, kapatikana mzawa tena.
 
Out of curiosity,kwanini hizi hoteli mbili watawala wa awamu zote zilizopita na hii iliyopo hawazizungumzii kuzirudisha??nini ilikua sababu ya kubakia magofu mpaka leo hii??
 
Ukitembelea maeneo ya posta hapa Dar zipo hoteli 2 zilizowahi kuwa maarufu sana za Embassy Hotel na Motel Agip. Huko Moshi pia kuna Moshi Hotel nayo inaoza katikati ya mji.

Cha kushangaza zimefungwa karibu mwaka wa 20 sasa na haziuzwi wala hazitafutiwi mwekezaji na serikali ambayo naamini ndio wamiliki.

Je hii sio hujuma?

Je ni Hazina, wizara ya biashara au wizara ya maliasili na utalii?

Anayejua tafadhali aseme hili swala likoje?
 
hoteli embassy jengo lao limeuzwa na wanataka kubomoa kujenga jengo jipya ni miaka mitano na zaidi tangu habari isambae kuwa jengo lililopo kuwa litabomolewa kujengwa upya. na agip nayo hivyo hivyo
 
Hata hivyo, Hotel Embassy na Motel Agip,sio mali ya Serikali
 
Kuna nyingine nimeiona pale ir inaitwa iringa hotel nayo inaoza wenyeji wanasema ni miaka mingi zaidi ya 15
 
WanaJF,

Ni jambo la kutia huzuni kuona vijana wanaangaika wanakosa hostel wakati kuna majengo yanaoza, Kama hawataki kiyaendeleza basi watangaze tenda watu wayakarabati yawe hostel za bei nafuu Serikali iendelee kupata kodi kuliko kuyaacha yakioza.

Hivi kweli Serikali haiyatambui mpaka kutelekezwa miaka yote?
 
Nashauri majengo yote yenye mgogoro serikali iyatumie kwa manufaa ya umma hadi watakapo imaliza.
 
Mkuu ungetupa picha ikiwa serikali imeshindwa kuya simamia basi ituuzie ili tuweke ofisi zetu na makazi ya biashara
 
Pia Kuna yake ya NSSF Geza ulole na NHC kawe na kijichi.bora yangemaliziwa wakae Jeshi au Police kuliko kuyaacha vile.so sad a white elephant project.huwa nahudhunika mno nikipita nayaona yapo tu
 
Back
Top Bottom