Embassy Hotel na Motel Agip: Nini hasa kilitokea?

WanaJF,

Ni jambo la kutia huzuni kuona vijana wanaangaika wanakosa hostel wakati kuna majengo yanaoza, Kama hawataki kiyaendeleza basi watangaze tenda watu wayakarabati yawe hostel za bei nafuu Serikali iendelee kupata kodi kuliko kuyaacha yakioza.

Hivi kweli Serikali haiyatambui mpaka kutelekezwa miaka yote?
...In kweli mkuu. Ila nasikia kuna Wajanja pale katikati ya mji wameifanya Embassy Hotel kama guest house ya short time fasta na wanajikunjia uchache wao na kutajirika huku serikali yetu ikiendelea kung'aa macho tu. Very sad.
 
20 yrs ni muda mrefu sana,kuna nini hasa kilitokea...
 
WanaJF,

Ni jambo la kutia huzuni kuona vijana wanaangaika wanakosa hostel wakati kuna majengo yanaoza, Kama hawataki kiyaendeleza basi watangaze tenda watu wayakarabati yawe hostel za bei nafuu Serikali iendelee kupata kodi kuliko kuyaacha yakioza.

Hivi kweli Serikali haiyatambui mpaka kutelekezwa miaka yote?
Nakumbuka mmiliki wa majengo hayo(Embassy) alikuwa na
mgogoro na wafanyakazi wake walikuwa wanadai haki zao
na chama cha wafanyakazi CHODAWU kilikuwa kinawasimamia
wanachama wake kudai haki zao.Mpaka sasa sijui kilichoendelea
kuna kipindi wale wafanyakazi walikuwa wanakaa pale kwa zamu
kulinda mpaka haki yao itendeke.
 
WanaJF,

Ni jambo la kutia huzuni kuona vijana wanaangaika wanakosa hostel wakati kuna majengo yanaoza, Kama hawataki kiyaendeleza basi watangaze tenda watu wayakarabati yawe hostel za bei nafuu Serikali iendelee kupata kodi kuliko kuyaacha yakioza.

Hivi kweli Serikali haiyatambui mpaka kutelekezwa miaka yote?
Nchi ya ajabu sana..sector ya hoteli ni ngumu sana nchini! Embassy ilivyokaa pale centre ni kwa kufungiwa miaka 20 kweli?wizara za utalii na biashara kweli zipo serious na nchi hii?sio hizo tu kuna hoteli kama Blue Pearl pale ubungo ni mambo ya kusikitisha,
Hivi mtu anayetaka kuwekeza ktk hotel industry Tanzania bara sio atawaza mara 2/2?
 
...In kweli mkuu. Ila nasikia kuna Wajanja pale katikati ya mji wameifanya Embassy Hotel kama guest house ya short time fasta na wanajikunjia uchache wao na kutajirika huku serikali yetu ikiendelea kung'aa macho tu. Very sad.
hilo nimelichunguza ni kweli kabisa ni gest elfu tano unamaliza kabisa
 
Majengo yale yatakua yamesomewa ALBADIRI kama wale mbuzi wanaozagaa pale magomeni, ukithubutu kuyafuatilia tu unakufa
 
WanaJF,

Ni jambo la kutia huzuni kuona vijana wanaangaika wanakosa hostel wakati kuna majengo yanaoza, Kama hawataki kiyaendeleza basi watangaze tenda watu wayakarabati yawe hostel za bei nafuu Serikali iendelee kupata kodi kuliko kuyaacha yakioza.

Hivi kweli Serikali haiyatambui mpaka kutelekezwa miaka yote?
Weka picha
 
Ni kama mali za urithi zinavyogeuka kuwa shubiri... Pamoja na hilo jengo la iliyokuwa Embassy Hotel ambalo liko kwenye sehemu nzuri kimkakati, lipo hilo la Agyp Motel na lile la Twiga Hotel ambalo angalau kuna mishemishe. Haya majengo matatu yamesahaulika na hayatajwi iwe serikalini au hata kwenye sekta ya utalii... Huwa mtu akihoji kama hivi anaibuka mtu anazungumzia mipango ya baadaye ya majengo hayo kisha inakuwa kimya hadi yatakapoguswa tena.. Ifike mahali sasa Serikali iamue au yabinafsishwe au yapigwe mnada. Mzee Lukuvi anaweza kuwa na la kusema hapa.
 
WanaJF,

Ni jambo la kutia huzuni kuona vijana wanaangaika wanakosa hostel wakati kuna majengo yanaoza, Kama hawataki kiyaendeleza basi watangaze tenda watu wayakarabati yawe hostel za bei nafuu Serikali iendelee kupata kodi kuliko kuyaacha yakioza.

Hivi kweli Serikali haiyatambui mpaka kutelekezwa miaka yote?

Matunda ya namna mbovu za ubinafsishaji. Zile hotel zinahitaji kufufuliwa. Wahindi waligawana mali zote nzuri nzuri. Wakiongowa na Sir(RIP).
Inashindikana nini kuzifufua hizo hotel? Basi zivunjwe tuwe tunapaki magari yetu tujue moja
 
Kama wakikubali kuniuziahayo majengo ya embassy kwa dollars za Marekani milioni ishirini nitayanunua. Lakini zaidi ya dollar million 20 sitoi
 
Matunda ya namna mbovu za ubinafsishaji. Zile hotel zinahitaji kufufuliwa. Wahindi waligawana mali zote nzuri nzuri. Wakiongowa na Sir(RIP).
Inashindikana nini kuzifufua hizo hotel? Basi zivunjwe tuwe tunapaki magari yetu tujue moja
Unaamasha Sir lile lifreemason lililokubuhu?
 
Enzi hizo ukisikia Kilimanjaro Hotel, New Africa Hotel Agip Hotelna Embassy Hotel ilikuwa ina tisha
 
Makonde kashindwa wapi? Au hana taarifa juu hili!
 
Back
Top Bottom