Moja kwa moja hojani,
Kwa mjibu wa website ya CCM, na Kwa mjibu wa kauli ya mwenezi wa CCM ndugu Hamphuley Polepole, CCM inawanachama wa kudumu M.14+
Na kikawaida, ili uwe mwanachama wa Chama chochote, maana yake uwe umefikia umri wa miaka 18+
Na kwa idaadi ya waliojiandikisha kupiga Kura nchi nzima ni M.29+
Kama ndio hivyo, maana yake CCM, Kati ya wapiga Kura M.29+ CCm inamtaji wa nusu ya wapigakura wote ikiwa wote watakuwa wamejandikisha na kuipigia Kura CCM siku ya uchaguzi
Sasa basi, Ni Kwa namna Ipi Chadema wataishinda CCM?
Let go...
Mada hii imejikita kutaka kujua ni kwa kigezo kipi Chama cha Chadema kinatumia hadi washabiki na wanachama wake hasa mitandaoni kusema eti kitashinda?
Je, ni kwa sababu ya mwitikio wa watu kwenye Kampeni za mgombea wa Chama chao?
Je, ni kwa sababu ya kuhesabu uwingi wa washabiki na wachangiaji kupitia Mitandao ya kijamii?
Je, ni kwa sababu mgombea wa Chama hicho anajua sana sheria?
Je, ni kwa sababu mgombea wake anafahamiana na kujulikana na viongozi wa mataifa mengi duniani
Ni kwa sababu zipi haswa hawa Chadema kujiaminisha kuwa watashinda uchaguzi huu?
Kama ni Kwa sababu ya watu wengi kujaa katika mikutano yake, mbona hata haifikii uwingi wa watu wa mgombea na mpinzani wake Kutokea CCM?
Mbona Mikutano yake na jinsi watu inavyo jaa, ni kama Tu Ile mikutano anayoifanya waziri mkuu Majaliwa?
Mitaani watu wengi ukiwahoji, wanasema kwamba, Mgombea uriais kupitia Chadema, atashindana, lakini kushinda atashinda wa CCM
Nimalizie kwa kuuliza, je, ni kwa kigezo kipi kinachowapa wanachadema waseme Chama Chao kitamwangusha Magufuli?
Chadema inaweza kushinda kwenye majiji makubwa mfano Dar, Mbeya, mikoa mingine kama Moshi, Arusha, Kigoma, Bukoba nk. Ila hata huko watagawana kura na CCM.
Wanachama wa muda mrefu wa CCM watakwenda kupiga kura kwa wingi ukilinganisha na vijana ambao wengi ndio wafuasi wa CDM.
Nilitegemea CDM watajikita kwenye Sera zinazowagusa Watanzania wengi washikilie hapo hapo kila siku. Wakisema wenyewe watafanya nini?
Kilimo - Nchi inahitaji kilimo cha kisasa cha umwagiliaji,mbolea pembejeo hapa wangeweza kutoa hata incentive kama Tax break kwa miaka kadhaa ili wawekezaji waanzishe viwanda hapa Tanzania.
Masoko ya bidhaa za kilimo hasa ya nje yaimarishwe na kuongezwa. Mahindi (Kenya) Mchele (Rwanda, Burundi, DRC, Comoro, South Sudan hadi Ulaya, USA,Uarabuni hadi Far East.
Avocado, machungwa, Tangarine, mananasi,mapapai, mboga mboga, hadi maua, yote yanaweza kutafutiwa masoko ya uhakika kwenye supermarkets za huko.
TRA :-- Hapa wangekuja na sera za kuhakikisha watu hawaonewi na kubambikiwa kodi ambazo haziendani kabisa na uhalisia, Camera kwenye Ofisi zote za umma, body camera kwa maofisa wote wa TRA, askari wa barabarani, Polisi ingewezesha kupunguza mambo ya rushwa kuongeza uwajibikaji makazini.
Kutumia zaidi IT kungeongeza ufanisi na kupunguza gharama. Kodi kwenye Bandari, Airports inabidi ziangaliwe kwa umakini upya, mfano gari sio luxury item, ni kama simu, necessity of life.
Uvuvi na ufugaji wenye tija, Mikopo kwa ajiri ya kununua boti za kisasa za uvuvi. Ufugaji wa kisasa, pamoja na kutafuta masoko ya uhakika ya ndani na nje kwa samaki na nyama zetu. To streamline process (kurahisisha, kuondoa ukiritimba) ya kupata export license.
Mfumo wa elimu inabidi ufumuliwe, ujikite zaidi kuwasaidia vijana kuwa tayari kukabiliana na changamoto za ajira na maisha kwa ujumla.
Afya:- hospitali, vituo vya Afya inabidi kuzidi kuimarishwa hasa vijijini.
Maji:- salama kila sehemu ya Tanzania itasaidia sana kupunguza magonjwa mengi, hivyo kuongeza nguvu kazi na kupunguza gharama za matibabu kwa serikali.
Miundombinu siyo vitu vya kubeza (barabara, bandari, reli, meli, umeme wa uhakika, ndege).
Hivi ni vitu ndivyo vitasaidia mazao kuchukuliwa vijijini na kupelekwa masokoni mijini na nje ya nchi hiyo itasaidia ku - improve utalii na uchumi wa watu.
Issue, discussion labda iwe asilimia ngapi?iwekezwe wapi? kwa muda gani? Kwa uwiano upi?