Mkuu, Embu Twende tu kimahesabu ya kawaida kabisa ya darasa la Saba
Fanya hivi, CCM inawanachama na wapiga Kura, wanaolipia uanachama wao Kwa mwaka ni watu 14m+
Okey, Fanya wale ambao wataasi kuipigia Kura CCM pamoja na wale wanachama haohao ambao hawakujiandikisha wawe idadi ya M.4+, maana yake, wale wanachama M.10 ndio wawe wamejiandikisha na ndio watakaoipigia Kura CCM, Kati ya wapiga Kura wote nchini 29m+
Maana yake idadi ya wanaobaki 19m+ ndio pengine kuna wanachama wa Chadema m6+ hivi mfano, nao sio wote watakuwa wamejiandikisha, na sio kwamba wote hakuna wataoisaliti Chadema,
Idadi inayobaki ya wanabakia ni 13m+, ndio hao Vyama vinaingia kuwashawishi ili wawapigie Kura wagombea hao
Sasa Fanya hivi tena, Kampeni za CCM Kwa siku moja pengine zinawafikia watu laki tano tu katika kila mkoa wanakofanyia Kampeni, kuanzia Mgombea Uraisi, waziri mkuu, wabunge na madiwani kote nchini
Chukua hiyo idadi uzidishe Kwa siku zote za uchaguzi, Utaona kwamba, CCM itakuwa imewafikia watu zaidi ya m.30+ ukiondoa idadi ya watu ambao Wapo kibindoni kuipigia Kura CCM hata wasposikia Sera za ccm, wale wanachama m.10 wa uhakika
Sasa utaona kwamba, Kati ya watu watakaofikiwa na CCM hao therathini M. Fanya tu Hesabu za kawaida kabisa, yaani useme tu, Kati ya hao, CCM iwashawishi wapigakura wapya M7+ Tu ,Kati ya wapiga kura ambao hawako CCM Wala Chadema
Utaona kwamba, tayari CCM itakuwa inajumla ya idadi za Kura zisizopungua M17+ Kati ya wapiga Kura wote M29+, idadi ya wapiga Kura waliobaki ambao Chadema na Vyama vingine vitawashawishi ni M6+ Baada ya kuwaondoa wanachama wa kudumu wa CCM ambao ni M10, na Chadema wanachama M6
Huoni kwamba CCM itakuwa na idadi nyiiingi za Kura M17+ isiyofikiwa na Chama chochote?