Embu waza viongozi ambao Africa tunapata wangekuwa na silaha za nyuklia, ingekuwaje?

Embu waza viongozi ambao Africa tunapata wangekuwa na silaha za nyuklia, ingekuwaje?

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,809
Reaction score
6,948
Wakati mwingine tushukuru kwa kila jambo. Waafrica huwa tunalia sana kwa nini hatuna nguvu duniani na kutamani na sisi tungetawala dunia.

Ila embu waza aina ya viongozi tunaowapata karibu nchi zetu nyingi. Ukimaliza, waza hawa viongozi wangekuwa na access ya silaha za nyuklia. Kwamba nchi fulani ikizingua, tunaiteketeza yote inabaki majivu.

Imagine kiongozi kila kinachomzunguka kuanzia viatu, magari vifaa ya kielectronic kama microphone, simu na TV, pombe, silaha zinazomlinda, nk na sitashangaa hadi lupi alilovaa vyote vinatoka kwa mabeberu. Unapata wapi ujasiri wa kuwa na kibri dhidi ya wanaokutengenezea hivyo na wewe hauna kiwanda hata kimoja cha kusingizia kuvitengeneza?

Hapohapo anategemea misaada ya kila aina, na unanuka mikopo ya kutoka kwa hao mabeberu. Hata biashara tu za nje ili nchi iende na muweze kununua hayo maV8 na maLamborghini, yote hayo unawategemea wao. Unapata wapi ujasiri wa kuwauliza "Who are you?"

Hapohapo una makandokando kibao ya kijinai na ni suala la muda tu kabla hawajakunyakua. Ningetegemea kaunyenyekevu kidogo. Kukutoa hapo wala hawahitaji nguvu kubwa kihiiivyo. Hawahitaji hata maandamano ya Gen-Z.

Imagine kwa kiburi hiki, halafu viongozi wa aina hiyo uwape kasanduku ka kulipua silaha za nyuklia kwa wabaya wake, dunia ingekuwa kwenye hali gani?

Hao mnaoita mabeberu hawataki nchi zinazoyumba. Wanataka stability. Chaos is not good for business. Msisikilize propaganda za wanasiasa. Hata hayo madini ya Congo hayatoroshwi bure, kuna wahuni wa kiafrica wakishirikiana na wanasiasa wanayachimba na kuyauza kwa hao mabeberu, hawawapi bure. Wanapotoa misaada au kufanya biashara halali na nchi husika wanataka kutengeneza taswira iliyo njema siyo tu na serikali husika ila pia na wananchi wake.

Wanapoona wanatoa mabilioni ya pesa kama misaada, wanakupa hadi access ya soko lao halafu kiongozi wa nchi kila siku anawabagaza mbele ya wananchi wake, taswira ya wananchi dhidi yao inaharibika na wataona ni bora uondoke aje mwingine.
 
Back
Top Bottom