Eminem: Kiumbe ambacho wana hiphop wanaogopa kuwa na bifu naye, rap God

sio mkali kiivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
Eminem ukali wake umepitiliza mzee, kwangu pac alikuwa bora kabla sijamfahamu huyu mwamba, ili nilipoisikia my name is... nikasema huyu mwamba fundi ila nimpe muda baada ya hapo alitoa vitu hadi nikakoma, Pac alikuwa bora ila alikaa kwenye game kwa muda mfupi na kwenye umri mdogo
 
Sometimes huwaga narudia kumtazama mara mbilimbili,najiulizags kwamba huyu mwamba ni mzungu au mweusi,ana punch lines kali sana
 
kuna interview Dre alisema alikua ana jua Eminem ni black kipindi bado hawajaonana walikua wakiwasiliana kwa simu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nna uhakika hata 2Pac haingizi mguu kwa Eminem[emoji124][emoji124]

Sina uhakika kwa hili aisee maana pac kajifia kitambo, kajifia wakati yupo kwenye peak, no one knows peak yake ingedumu kwa muda gani enzi za uhai wake, ni kama vile messi angekufa 2009 au 2011, ama pele angekufa 1963.

Kama vile eminem angekufa 2004/05 hivi tungekosa vingi mnooo.

Kwa mimi pac huwa namuweka mbele zaidi! Katika umri wa miaka 25 alikuwa kaishafanya mabala sijui angekuwa hai mpaka 41 hivi ingekuwaje.

Eminem namkubali tena namuelewa saana! Ila sijawahi fikiria kumshindanisha na pac kwa sababu zangu hapo juu.

Ngoja nikasikilize mockingbird kisha nisikilize untill the end of time, nigonge cleanin’ out my closet kisha nisikilize i aint mad at cha, nipige loose yourself kisha nimsikilize dear mama, nile utamu wa no love, ninogeshe na keap ya head up, niisikilize my name kisha nile utamu wa do for love , nisikilize stan na the real slim shady nimalizie na so many tears, me against the world.


Kwa leo itakuwa inatosha nitakuwa nimesikiliza muziki baada ya mida mrefu mnoo kupita.
 
Hakika wewe ni mtu wa Hip Hop.
Pia nimependa hoja yako ulivyoiweka kuhusu kuwashindanisha Em na Pac.
Salute Broh!
 
Huwezi kueleweka na wasiojua mziki. Post yako ni killer kwenye hii thread.

Eminem ana pumzi,verse ndefu na rhythm ndio maana Akirap anakuwa kwenye pattern ileile beat inamfuata baadae.

Lakini huyu Rap cartoon wala sio lyricist.

But I remain a fanatic fan just like "Stan"

Melvine
 
Sawa mkuu ila Eminem🙌
 
Eminem ana pumzi,verse ndefu na rhythm ndio maana Akirap anakuwa kwenye pattern ileile beat inamfuata baadae.

Lakini huyu Rap cartoon wala sio lyricist.
Boss, hapo nilipobold ulikuwa na maana gani yaani?
 
You're right, ila Eminem ana upekee kidogo sijui tuseme yupo gifted akiongea ni kama ana Rap yaan mda wote ni full sanaa jaribu kuangalia interview zake huchoki kumsikiliza
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo yule mwenyekiti wa Nanjilinji?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli mkuu...muda mwingine so lazima kufananisha vitu.
Nakumbuka J Cole alishawahi kuulizwa kati ya Michael Jordan na Kobe Bryant nani mkali was muda wrote kwenye kikapu?
Cole akajibu....Ninachojua Jordan amecheza kwa ubora kwenye kipindi chake pia Kobe amefanya hivyo kwenye kipindi chake ila siwezi sema nani no bora kuliko mwenzie.
Mimi huishi hivyo mfano namkubali Nas pia Jay Z kila mmoja kwa nafasi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…