Mabulangati
JF-Expert Member
- Dec 29, 2010
- 796
- 167
Wandugu jana nilienda kumpokea mgeni wangu toka Sri Lanka pale Julius Nyerere international Airort (Dar es Salaam). Saa 9.06 mchana Ndege ya shirika maarufu duniani Emirates iliwasili lakini ilipokanyaga ardhi tu ikapaa tena kurudi angani na kutua rasmi baada ya dakika kama 38 hivi. Sijui kilichotokea au ni kikwazo gani kilileteleza ndege hiyo kurudi angani ia mgeni aliposhuka alinieleza kuwa rubani aliomba radhi kwa kuchelewa kutua ila hakusema sababu za kutua na kupaa kwa haraka kiasi kile.
Jamani wenye taarifa zaidi za tukio hili hasa wa mamlaka ya viwanja vya ndege watujuze. Maana tumezoea mambo hayo yakifanywa na ndege za kijeshi siyo za abiria.
Journalists may wish to consult Emirates officers or TAA for elaborations on this.