Emirates yafanya maajabu uwanja wa ndege dar es salaam

Emirates yafanya maajabu uwanja wa ndege dar es salaam

Si kitu cha ajabu wala si kitu cha kawaida sana, lakini huwa kinatokea mara kadhaa. Binafsi kimewahi kunitokea mara nne (4); 2 hapo DIA, moja Nairobi (JKIA) na Oman-Muscat Int. Airport, ila presha yake si mchezo. Kwa Dar huwa inatokea sana ndege zinapotua south-north direction. Yaani zinapotua kutokea upande wa kusini wa uwanja (sijui kesi yako ilikuwa ikitua vipi siku hiyo). Na vilevile Dar Airport kuna kiupepo flani kikorofi sana.

Mbali na sababu walizozitoa wana JF ambazo nyingi ni possible reason, sababu nyingine ni missed direction. Ndege huwa haikati kona inapokuwa kwenye ground speed ya kutua, hivyo ni wajibu wa rubani kuhakikisha kwamba anaiweka kwenye straight line at the ground level wakati wa kutua. Kwani akiikosa itabidi afuate direction husika ambayo huenda ikamtoa kwenye lami na kumpeleka kwenye majani na hatimaye dhahama kutokea. Hivyo akigundua kwamba hayuko kwenye straight line hana budi kuruka tena na kuanza mzunguko mpya (Kumbuka rubani wanaona chini ya ndege, teknolojia ambayo imeshawekwa kwenye magari mengi hivi sasa). Na huenda mbali kidogo ili kuwaondoa abiria na presha waliyoipata wakati wa kuruka ghafla na kuruhusu logistic nyingine uwanjani kama hazijabadilika/kuanza upya. Ya Nairobi ambayo hii ilikuwa kitambo kidogo (six years ago) ilisababishwa na ukungu ambayo ilimkosesha rubani kuuona kwa usahihi huo 'straight line at the ground', hivyo naye alipaa tena na alienda kutua Mombasa.
 
Wandugu jana nilienda kumpokea mgeni wangu toka Sri Lanka pale Julius Nyerere international Airort (Dar es Salaam). Saa 9.06 mchana Ndege ya shirika maarufu duniani Emirates iliwasili lakini ilipokanyaga ardhi tu ikapaa tena kurudi angani na kutua rasmi baada ya dakika kama 38 hivi. Sijui kilichotokea au ni kikwazo gani kilileteleza ndege hiyo kurudi angani ia mgeni aliposhuka alinieleza kuwa rubani aliomba radhi kwa kuchelewa kutua ila hakusema sababu za kutua na kupaa kwa haraka kiasi kile. Jamani wenye taarifa zaidi za tukio hili hasa wa mamlaka ya viwanja vya ndege watujuze. Maana tumezoea mambo hayo yakifanywa na ndege za kijeshi siyo za abiria. Journalists may wish to consult Emirates officers or TAA for elaborations on this.

Uko sahihi sana na ulichokishangaa, ni ajabu na ni jambo la hatari sana hasa kwa ndege ya abiria. Rubani lazima ajieleze na atoe maelezo hayo si kwa abiria tu bali na kwa wataalamu ili wapime ulazima wa kufanya hivyo. Kimsingi mimi na mashaka sana na uwezo wa rubani huyo!
 
Rubani alisikia Mwakyembe yupo Uwanjani kwa Ukaguzi... Rizmoko alimpigia simu na kumuambia ni Kovvva usiwe na wasiwasi wewe tua tu
 
Sisi wataalamu tunaita MISSED APPROACH
is a procedure followed by a pilot when an instrument approach cannot be completed to a full-stop landing.

Mkuu afadhali wewe umeongea kitaalam, watu wanasema ni jambo la kawaida sana, lakini mimi napingana nao. Ndege haiwezi kutaka kutua kisha gafla iruke tena juu na ukaendelea kusema kwamba ni jambo la kawaida. Kuna kitu hakipo sawa!
 
Ndege hz zina mambo jana kuna mtu nusura aachwe tiketi imeandikwa reporting time 6:00 night akajua ni ijumaa kumbe ni alhamis na watu weng waliachwa hv kweli hyo reporting time alieset hvyo kweli anawazaje kichwani mwake.
 
kwa maelezo haya nimejifunza kitu

1] kutii maelezo ya wahudumu wa ndege wanaposema, tulieni kwenye viti na mkiwa mmefunga mikanda hadi ndege itakaposimama kabisa, kwa bahati mbaya sikufahamu kuwa ndege inaweza kutua hadi ardhini na kurudi tena juu.kusema kweli linapotokea hili jambo huwa kuna mkanganyiko mkubwa Sana. Mara nyingi kuna wasafiri ndege inapotua chini haraka wanafungua mikanda na kukimbilia kuchukua mizigo, ni hatari sana.

Hakika jf ni darasa lenye upeo uliotukuka.
 
Kuna ng,ombe walikuwa malisho hapo airport ,akaogopa kuwagonga
 
Labda alikuja too fast,na aliogopa kufanya overshoot ya runway,kwa hiyo akarudi angani. Kuchelewa 38 minutes,hiyo labda ilikuwa sababu tu ya kupisha ndege nyingine.
 
Mdau Mabulangati, hilo ni jambo la kawaida, hata mimi limeshawahi nitokea na rubani alisema ni tatizo la upepo. Ndege zina kifaa cha kupimia upepo wa chini (ground wind flow) ila sometimes due to several reasons hua hakipimi sawasawa mpaka pale ndege inapofika chini ndio rubani anagundua upepo ni mkali na si salama kwa ndege kutua in that direction so hua wanarudi angani na kubadilisha direction ya kutua then wanatua in different direction ila pia inategemeana na uzito wa ndege wakati huo.

kati ya majibu yote nimependa wewe ulivyojibu na kuelewesha umati...bila shari wala kumcheka mtu, sio kila mtu anajua kila kitu,just bcoz mtu kazoea kupanda ndege daznt mean anajua
 
kwa maelezo haya nimejifunza kitu

1] kutii maelezo ya wahudumu wa ndege wanaposema, tulieni kwenye viti na mkiwa mmefunga mikanda hadi ndege itakaposimama kabisa, kwa bahati mbaya sikufahamu kuwa ndege inaweza kutua hadi ardhini na kurudi tena juu.kusema kweli linapotokea hili jambo huwa kuna mkanganyiko mkubwa Sana. Mara nyingi kuna wasafiri ndege inapotua chini haraka wanafungua mikanda na kukimbilia kuchukua mizigo, ni hatari sana.

Hakika jf ni darasa lenye upeo uliotukuka.

Duh! Mimi ni mmojawapo wa hao uliowasema (kufungua mikanda na kusimama kabla ndege haijatulia kabisa), lakini kwa tukio hili, ni hadi pale ndege itakapokuwa imesimama kabisa ndo nitafungua mkanda!
 
usafiri wa ndege kwa wa tz wengi ni anasa

hakika,kuna siku npo na rafiki yangu mmoja namwambia kuwa nakwenda kufanya booking ya ticket ya ndege kutoka mwanza -dar anashangaa "unakwenda kukata tiketi ya ndege wewe? Acha kutuzingua"kiukwel nlikuwa so disapointed na nkaona kweli watanzania usafir wa ndege ni anasa.
 
Wote mmejitahidi sn kutoa majibu ambayo yanaelekeana na ukweli.
Lakini kwa kufupisha mambo, kuna sbb nyingi zinazoweza kupelekea ndege kuoveshoot km ifuatavyo:
1.Uwepo wa mnyama au ndege kwny njia ya kutua na kuruka ndege(wenyewe wanaita Wildlife Hazard).

2. Kuwepo kwa foreign object au debri yoyote kwenye njia hiyo.

3.Mabadiliko ya ghafla ya upepo. Kawaida kila bada ya dakika 30 mtu wa Met anatakiwa kupeleka weather report inayoitwa 'meter'kwa air traffic controllers ili nao wawasomee marubani. Lakini within 30min kunaweza kutokea sudden change zitakazosababisha crosswind kali hadi kumfanya pilot arudi juu ili akaistabilize ndege kwa buttons za ziada.
Pia hapa kuna kipimo sensitive sana cha mgandamizo wa hewa ambacho ndicho kinaifanya ndege inayotua ijue iko umbali gani toka tairi lake hadi kwenye lami. Ni mambo mengi complex kidogo hapa.

4.Priority- huwa kuna Priority ya kutua nyakati fulani. Imagine ndege ya kawaida km Emirates inaongozana na Tanzania One ya Kikwete, huku ya JK ikiwa nyuma, kwa sheria za Aviation lazima VIP wa level ya Rais apewe priority kwanza kabla ya raia mwingine.
Pia kuna Priority inayotolewa kwa ndege kubwa vs ndogo kwenye kutua, coz the larger the equipment the larger the risk associated.

5.Ni mara nyingi tu ambapo pilot akihisi ana pancha kwenye tairi atashusha ndege hadi kwenye level ya jengo la control tower ili wamsaidie kuangalia, then anaovershoot.

5. N.kadhalika.

Ila nina shaka kidogo na mleta mada kama ni ukweli kuwa ndege hiyo ilishuka hadi kugusa pavement ya runway. Hakuna kitu cha hivo.
Ndege kubwa jamii ya Boeing au Airbus haiwezi kabisa kugusa runway na kunyenyuka ikiwa salama kutokana na uzito wake. Kitendo cha kugusa tu ile njia kinapunguza sana kasi ya ndege na haiwezi kunyenyuka ghafla.
Ntakubali km atasema ilishuka chini sn, lkn si touchdown.

Pia naomba nimrekebishe mdau mmoja aliyesema kuwa huenda pilot hakuiweka ndege sawasawa kwenye center-line ya runway.
Kwa kiwanja kikubwa kama Jnia kina maneno inaitwa Instrument Landing System(ILS) ambapo pilot akifika umbali fulani jirani na kiwanja anawasha radios fulani ndani ya ndege ambazo zinawasiliana na antenna zilizopo mwanzoni mwa njia ya kutua(localizer), na ndizo zinazoiposition ndege itue kwenye msitari wake tu, bila kosa hata la mm 1!

Ni mambo mengi lakini kwa ufupi hatuwezi kujua ninini kilimfanya rubani wa ndege hiyo airudishe ndege juu, lakini lazima aliwasiliana na tower, maana hawezi kufanya jambo la hatari hivyo bila reporting, ambapo hata controller aliyepo zamu analog incidence hiyo kwenye logbooks zake.

Huenda maelezo yangu yatawasaidia baadhi ya watu wanaosema ni kitendo cha kawaida' tu! Kitaalamu tunasema kuwa 90% ya ajali za ndege hutokea ndani au jirani kabisa ya kiwanja(within,or in the vicinity of the Airport), kwa maana kwamba uwezekano wa rubani kufanya makosa zaidi upo kwenye kitendo cha kuruka na kutua.
Kupandisha juu ndege iliyokuwa inatua inamaanisha kuactivate kwa ghafla systems zote zilizokuwa tayari zinaslow down, kwahiyo ndege inaweza kukubali au kukataa.

Mimi najua kuwa si kawaida unless kama pilots wako mafunzoni, but si ndege ikiwa na abiria 300, over the dead body!!!
 
Mabulangati;7148074]Nashukuru nimeekewa. Lakini kwa mujibu wa mgeni wangu, hakukua na maelezo yoyote kuhusu hilo hivyo kwangu ilikua maajaby
Mkuu ulichokiona si cha ajabu ingawaje kinatisha!
Mimi kimeshanitokra pale uwanja wa ndege Dubai mwaka 2006, tulipokuwa tunatua na ndege ya Africa One.

Ndege ilianza kutua na kabla kufika ardhini kama mita 10 hivi rubani akavuta mafuta na ndege ilikuwa kama inasota kanla ya kupaa tena.
Mama mmoja wa jirani akaenda haja.
Tukazunguka tena kama nusu saa na tukatua salama kabisa.

Hatukuelezwa kwa nini rubani ali abort landing, na yule mama alikuwa wa mwisho kishuka.
 
hakika,kuna siku npo na rafiki yangu mmoja namwambia kuwa nakwenda kufanya booking ya ticket ya ndege kutoka mwanza -dar anashangaa "unakwenda kukata tiketi ya ndege wewe? Acha kutuzingua"kiukwel nlikuwa so disapointed na nkaona kweli watanzania usafir wa ndege ni anasa.

hiyo kawaida tu. nilikuwa mkoa fulani nikawa na safari ya kwenda dar, nikamwambia mtu nakwenda dar, akaniambia hebu acha uongo wewe unaweza kwenda dar wewe. Nilishindwa hata kuendelea kuongea nae nikaondoka zangu.
 
Kama alivyosema mdau mmoja hapo...si rahisi kwamba hiyo ndege ilitua mpaka chini(touchdown)...ni lazima rubani ali-overshoot,mana kwa sasa Emirates Tz wanaleta Boeing777-200/300...sasa kwa aina hii ya ndege huwezi ishusha chini na kuirusha tena kwa ghafla kutokana na uzito wake
Kuna mambo kadhaa husababisha "overshooting"
(1)Kuzima kwa taa za runway/Approach lights
Maarufu kama PAPI
(2)kuwepo kwa ndege "birds hazards" na FOD
i.e foreign object demage kama nuts,mawe,
Vyuma n.k vinavyoweza kuwa sucked na jet
Engine na kuleta madhara..
(3)Runway Obscurity...poor visibility ya runway..
Hii inamfanya rubani a-overshoot kabla ya
Kutua..
Kitendo hichi si cha kawaida...ni lazima rubani atoe maelekezo,wakati mwingine uwanja wetu mbwa na mbweha huingia ktk runway..rubani anaweza kutahaamaki mbwa huyu hapa...hawezi kutua...so sio jambo dogo
 
Back
Top Bottom