PakaJimmy
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 16,199
- 8,761
Ni kweli mkuu, mimi pale kwenye post yangu sikusema kwamba haiwezekani, inawezekana,lakini ni risk kubwa ajabu kufanya kitendo hicho! Shukuruni Mungu hiyo touch n' go ilifanikiwa. Inataka pilot awe na sababu very serious kucheza mchezo huo huku akiwa na abiria 250 au 300 onboard!Mimi nilipanda Quntas Boeing 747 Hongkong-Brisane kupitia Manila. Pale Manila ndege ikitua ilikanyaga runway na baadaye kupaa papo hapo! Tuliambiwa kulikuwa na foreign object 400 meters away na ikalazimisha kurudi hewani. Tulishuka baadaye after 2 hours
Pia nilisema kuwa makosa mengi kwenye ajali za ndege hutokea kwenye kitendo cha kutua au kunyanyuka pale kiwanjani, mojawapo ni condition ya namna hiyo. Inataka Pilot makini sana kuactivate harakaharaka tena ndege ambayo aliiandaa kwa kutua na kusimama.
Labda nisema kuwa mara nyingi sana ndege huwa zina'generate snags zikiwa hewani, lakini kutokana na ndege ilivyotengenezwa kwa umakini huwa zinaweza kutembea tu angani na snags hizo, hadi itakapotua, na ndipo baada ya hapo itadai matengenezo kwa lazima kwa kudisplay kwenye dashboard kuwa haiondoki hadi itengenezwe.
Sasa kwa ndege ambayo iligenerate snag ikiwa enroute, halafu pilot anatua, ghafla anaanza kupaa bila kumaliza cycle ya kutua, ujue anaandaa msala utakaotangazwa kwenye TVs za dunia nzima, na wauza magazeti watafanya biashara iliyotukuka!