Kashi
JF-Expert Member
- Jan 6, 2013
- 897
- 745
Wote mmejitahidi sn kutoa majibu ambayo yanaelekeana na ukweli.
Lakini kwa kufupisha mambo, kuna sbb nyingi zinazoweza kupelekea ndege kuoveshoot km ifuatavyo:
1.Uwepo wa mnyama au ndege kwny njia ya kutua na kuruka ndege(wenyewe wanaita Wildlife Hazard).
2. Kuwepo kwa foreign object au debri yoyote kwenye njia hiyo.
3.Mabadiliko ya ghafla ya upepo. Kawaida kila bada ya dakika 30 mtu wa Met anatakiwa kupeleka weather report inayoitwa 'meter'kwa air traffic controllers ili nao wawasomee marubani. Lakini within 30min kunaweza kutokea sudden change zitakazosababisha crosswind kali hadi kumfanya pilot arudi juu ili akaistabilize ndege kwa buttons za ziada.
Pia hapa kuna kipimo sensitive sana cha mgandamizo wa hewa ambacho ndicho kinaifanya ndege inayotua ijue iko umbali gani toka tairi lake hadi kwenye lami. Ni mambo mengi complex kidogo hapa.
4.Priority- huwa kuna Priority ya kutua nyakati fulani. Imagine ndege ya kawaida km Emirates inaongozana na Tanzania One ya Kikwete, huku ya JK ikiwa nyuma, kwa sheria za Aviation lazima VIP wa level ya Rais apewe priority kwanza kabla ya raia mwingine.
Pia kuna Priority inayotolewa kwa ndege kubwa vs ndogo kwenye kutua, coz the larger the equipment the larger the risk associated.
5.Ni mara nyingi tu ambapo pilot akihisi ana pancha kwenye tairi atashusha ndege hadi kwenye level ya jengo la control tower ili wamsaidie kuangalia, then anaovershoot.
5. N.kadhalika.
Ila nina shaka kidogo na mleta mada kama ni ukweli kuwa ndege hiyo ilishuka hadi kugusa pavement ya runway. Hakuna kitu cha hivo.
Ndege kubwa jamii ya Boeing au Airbus haiwezi kabisa kugusa runway na kunyenyuka ikiwa salama kutokana na uzito wake. Kitendo cha kugusa tu ile njia kinapunguza sana kasi ya ndege na haiwezi kunyenyuka ghafla.
Ntakubali km atasema ilishuka chini sn, lkn si touchdown.
Pia naomba nimrekebishe mdau mmoja aliyesema kuwa huenda pilot hakuiweka ndege sawasawa kwenye center-line ya runway.
Kwa kiwanja kikubwa kama Jnia kina maneno inaitwa Instrument Landing System(ILS) ambapo pilot akifika umbali fulani jirani na kiwanja anawasha radios fulani ndani ya ndege ambazo zinawasiliana na antenna zilizopo mwanzoni mwa njia ya kutua(localizer), na ndizo zinazoiposition ndege itue kwenye msitari wake tu, bila kosa hata la mm 1!
Ni mambo mengi lakini kwa ufupi hatuwezi kujua ninini kilimfanya rubani wa ndege hiyo airudishe ndege juu, lakini lazima aliwasiliana na tower, maana hawezi kufanya jambo la hatari hivyo bila reporting, ambapo hata controller aliyepo zamu analog incidence hiyo kwenye logbooks zake.
Huenda maelezo yangu yatawasaidia baadhi ya watu wanaosema ni kitendo cha kawaida' tu! Kitaalamu tunasema kuwa 90% ya ajali za ndege hutokea ndani au jirani kabisa ya kiwanja(within,or in the vicinity of the Airport), kwa maana kwamba uwezekano wa rubani kufanya makosa zaidi upo kwenye kitendo cha kuruka na kutua.
Kupandisha juu ndege iliyokuwa inatua inamaanisha kuactivate kwa ghafla systems zote zilizokuwa tayari zinaslow down, kwahiyo ndege inaweza kukubali au kukataa.
Mimi najua kuwa si kawaida unless kama pilots wako mafunzoni, but si ndege ikiwa na abiria 300, over the dead body!!!
Duh! Mkuu nimekukubali kwa shule nzuri.Hongera sana!