Emma Lwaitama Nyerere: Kisababishi kilichojificha katika sakata la Madaraka na Steve Nyerere?

Tarishi

Senior Member
Joined
May 9, 2008
Posts
105
Reaction score
150
Vyombo vya habari vya Tanzania vinaonekana kuifuta mipaka kati ya uandishi wa habari na hadithi za mitaani, kwa ku-copy na ku-paste kila habari wanayopata bila kuchimba zaidi kutafuta ukweli.

Drama ya hivi karibuni inayowahusisha Madaraka Nyerere, mtoto wa Baba wa Taifa, na Steve Mengele, anayejulikana kwa jina maarufu la Steve Nyerere, ni mfano halisi wa uvivu huu wa wanahabari. Badala ya kufanya kazi yao na kuchunguza kwa nini ghafla Madaraka ameamua kumwambia Steve aache kutumia jina la Nyerere, ilhali amekuwa akilitumia kwa miaka mingi, wanahabari wamekopi tu habari kama ilivyo bila kuuliza maswali ya msingi ama kuchunguza nini chanzo halisi ama kisababishi?

Ngoja niwasaidie wanahabari, kwa sababu baada ya kuwafanyia kazi yao ya kiuchunguzi, hatimaye nimegundua kiini cha sakata hili. Hapa kuna siri nzito ambayo inaweza kueleza vurugu hii. Na sio kwamba Steve anaiga sauti ya Mwalimu au anapenda sifa za kuiwa na jina la Nyerere.

Tatizo halisi linamhusisha Emma Lwaitama Nyerere, mwanaharakati maarufu na binti wa mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dr. Azavery Lwaitama, ambaye pia amekuwa akitumia jina la Nyerere kwa muda mrefu sasa. Emma si mwanaharakati wa kawaida; kwa miaka kadhaa amekuwa akidai kuwa ni binti wa Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jambo ambalo si kweli. Rekodi zinaonesha amekuwa hata akikaribishwa majumbani ama Ikulu kwa viongozi wanaompenda na kumthamini Mwalimu Nyerere. Kwao wao kuwa na “binti” wa Mwalimu ilikuwa furaha na fahari ilioje.

Awali alikuwa akijitambulisha kama mtoto wa Mama Maria, baada ya kuhitimu utamu wa jina na kuonja faida zake, akawa “binti” wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Soma Pia: Kumbukizi ya Nyerere: Familia ya Mwalimu Nyerere yawataka wasanii kuacha kutumia jina la Baba wa Taifa kama ubin wao

Sasa, hapa ndipo ulipo mwiba wenyewe, ambao hata Madaraka anaonekana kuuogopa usimchome: Emma amezaa mtoto na Kambarage Joseph Nyerere, ambaye ni mtoto wa kambo mdogo wa Mwalimu, Joseph Nyerere! Kimsingi, Emma angekuwa na haki kabisa ya kutumia jina la Nyerere iwapo wangekuwa wameoana, lakini hawajaoana bado.

Hivyo basi, uhusiano wa Emma na jina la Nyerere ni wa kulazimisha. Au angalau asingekuwa anafanya haya yafuatayo.

Sasa, mambo yalianza kuchafuka pale Emma alipoanza kujitokeza kwenye majukwaa ya kitaifa na kimataifa, akipigia debe ajenda zake za kisiasa, ikiwa ni pamoja na kuunga mkono taifa la Palestina huku akilaani vikali vitendo vya Israel.

Sio siri kwamba msimamo wake huu wa wazi kuhusu Palestina, hasa kwenye majukwaa ya kimataifa, umechokoza hisia za baadhi ya mataifa ya Magharibi.

Mataifa haya yanaona kama ni fedheha ya kidiplomasia kwamba mtu wa familia ya Nyerere anazua kasheshe kwenye masuala nyeti ya kimataifa.

Tuseme tu, "wakubwa" hawajaridhika kabisa. Na kutokana na diplomasia nyeti ya Tanzania ya kutofungamana na upande wowote, kuna dalili kwamba shinikizo limetolewa chini kwa chini. Na hapa ndipo hadithi inakuwa tamu.

Vyanzo vya ndani vinaashiria kwamba msimamo wa Emma kuhusu Palestina, unaoendelea kuakisi msimamo wa zamani wa Julius Nyerere aliyewaunga mkono Wapalestina waziwazi, umewaudhi "wakubwa.” wa magharibi.

Inaonekana wameishinikiza familia ya Nyerere kumvuta Emma chini, wakitaka jina hilo lisihusishwe kabisa na siasa hizo za kimataifa, huku wakipigwa mkwara wa “Hiyo ilikuwa zamani, sasa mchezo umebadilika. Kwa hiyo, mnyamazisheni! Vinginevyo…”

Sasa familia ya Nyerere inafanyaje? Badala ya kumkemea Emma moja kwa moja, wanamtuma Madaraka, msemaji wa familia. Lakini yeye, badala ya kukabiliana na chanzo halisi—Emma kutumia jina la Nyerere kwenye majukwaa ya kimataifa—wanaamua kumshambulia Steve Nyerere, ambaye utaamua mwenyewe kama ana ama hana hatia ya kupewa jina hilo na mashabiki wake kwa kuiga sauti ya Mwalimu.

Steve anakula za uso huku watu wengine wanaotumia jina la Nyerere.Mfano mwingine ni kama huyu Yericko Nyerere, anayejinasibu yu mtaalamu bingwa wa masuala ya ujasusi na dilomasia na uchumi na mwandishi wa vitabu vya masuala ya ujasusi ambao wanaendelea kula bata kwa jina la Mwalimu.

Yericko, ambaye anatokea Iringa (kama Steve), sii Mzanaki na hana uhusiano kabisa na Mwalimu. Lakini Madaraka kammezea!

Kuna dhana kwamba huenda kutoikana na umaarufu alio nao, imeonekana ujumbe utafika haraka zaidi endapo kama watamtumia Steve kama mbuzi wa kafara.

Wengine watamalizana nao baadae mmoja mmoja. Sasa basi, sina haja ya kuwatafunia kila kitu enyi wanahabari, habari ndiyo hiyo. Tafuteni ukweli. Muulizeni Madaraka yote haya. Na kwa upendo wa Mungu, acheni ku-copy na ku-paste! Jifunzeni kuchunguza mambo kama nilivyoiwasaidia hapa!

Alamsiki

Screenshot 2024-10-15 at 12.12.27 AM.png
99b340e5-9fc2-4660-844e-a10865fd4e85.JPG
 
Nimekuelewa sasa huyo Steve na Mwenzie yule Engineer mwandika vitabu bwana Yericko Nyerere nao wajitathmini wakiweza wajivue huo ubini haraka watumie ubini wao kwani lazima kutumia ubini usiowahusu mboni ni jambo dogo tu, Madaraka msemaji wa familia kasema wajivue ubini basi wajivue si wakipigiwa simu hawapokei haya vueni ubini huo haraka
 
Waanze kujiita Nyelele badara ya Nyerere.
Waende mbali zaidi kwa kuliongeza Hilo jina kwa kufanya deedpoll kabisa.

Ukishakuwa kiongozi wa nyadhifa kubwa kabisa kitaifa basi unakuwa Mali ya kila mtu kwa watakao jivunia, kukuponda, kuku enzi na kujisifia.
 
Kama Yeriko Nyerere anatumia jina Mwalimu ebu tutajie ubini wake halisi unaoujua wewe.
 
Nimekuelewa sasa huyo Steve na Mwenzie yule Engineer mwandika vitabu bwana Yericko Nyerere nao wajitathmini wakiweza wajivue huo ubini haraka watumie ubini wao kwani lazima kutumia ubini usiowahusu mboni ni jambo dogo tu, Madaraka msemaji wa familia kasema wajivue ubini basi wajivue si wakipigiwa simu hawapokei haya vueni ubini huo haraka
Siyo rahisi kihivyo maana wanafaidika na hilo jinq.
 
Waanze kujiita Nyelele badara ya Nyerere.
Waende mbali zaidi kwa kuliongeza Hilo jina kwa kufanya deedpoll kabisa.
Sheria za hati miliki zinataka kuandika na kutamka kusichanganye watu

Hivyo ukijiita Nyelele utaambiwa tamka ukitamka Nyelele wanakwambia umevunja hati miliki matamshi yanafanana

Watumie majina ya ubini wao wayakuze na wao yawe makubwa kama la Nyerere

Ni aibu kwa wazazi wao na koo zao kuparamia majina ya ubini wa koo zingine

Wajenge brand ya ubini wa koo zao

Vikao vya koo za baba zao wakae nao wawaambie mnatia aibu na kudhalilisha ubini wetu.

Kama mtu ana kitu hqya akitumia ubini wake watu watamtambua tu

Naungana na madaraka waachane na jina la Nyerere wajenge brand name zao za ubini wa kwao
 
Yaani Emma hadi anaogopa kutumia jina la ubini la Lwaitama

Mzee Lwaitama ajitathmini .Mimi huwa nikimsikiliza huwa naona kama yule mzee mwehu

Nafikiri Emma asaidiwe tu kisaikolojia kuwa atumie tu huo ubini baba yake mwehu lakini ndio hivyo tena hawezi kuwa na baba mwingine huyo ndie baba yake atumie tu ubini wa Lwaitama hivyo hivyo itasaidia pia jamii kujua kuwa sio akina Lwaitama wote wehu yeye zimo kichwani.Itasaidia kusafisha jina bovu la Lwaitama
 
Yaani Emma hadi anaogopa kutumia jina la ubini la Lwaitama

Mzee Lwaitama ajitathmini .Mimi huwa nikimsikiliza huwa naona kama yule mzee mwehu

Nafikiri Emma asaifiwe tu kisaikolojia kuwa atumie tu huo ubini baba yake mwehu lakini ndio hivyo tena hawezi kuwa na baba mwingine huyo ndie baba yake atumie tu ubini wa Lwaitama hivyo hivyo itasaidia pia jamii kujua kuwa sio akina Lwaitama wote wehu yeye zimo kichwani.Itasaidia kusafisha jina bovu la Lwaitama
Wewe ndiye mwehu. Lwaitama ni maana halisi ya mzalendo. Hana makuu, hana tamaa ya madaraka wala mali. Mliozoea vya kunyonga lazima umuone mwehu.
 
Sheria za hati miliki zinataka kuandika na kutamka kusichanganye watu

Hivyo ukijiita Nyelele utaambiwa tamka ukitamka Nyelele wanakwambia umevunja hati miliki matamshi yanafanana

Watumie majina ya ubini wao wayakuze na wao yawe makubwa kama la Nyerere

Ni aibu kwa wazazi wao na koo zao kuparamia majina ya ubini wa koo zingine

Wajenge brand ya ubini wa koo zao

Vikao vya koo za baba zao wakae nao wawaambie mnatia aibu na kudhalilisha ubini wetu.

Kama mtu ana kitu hqya akitumia ubini wake watu watamtambua tu

Naungana na madaraka waachane na jina la Nyerere wajenge brand name zao za ubini wa kwao
Uko Sahihi kabisa, Watumie Ubini wa Wao, Wewe Yerico Nyerere na Yule Kuwadi Mkongwe Steven Nyerere Pamoja na huyu Mtoto wa Profe,, Lwaitama, Emma Lwaitama Wakatazwe Hawa Viumbe kutumia Majina Ambayo Awana Vinasaba Nawo
 
Siyo mara ya kwanza hili suala kuibuka,Andrew Nyerere naye amewahi kumzukia Yericko

Kimsingi hiyo familia wangekomaa na wanaotumia hilo jina kulaghai na kuhadaa watu kuwa na wao ni uzao wa Mwitongo.
 
Vyombo vya habari vya Tanzania vinaonekana kuifuta mipaka kati ya uandishi wa habari na hadithi za mitaani, kwa ku-copy na ku-paste kila habari wanayopata bila kuchimba zaidi kutafuta ukweli.

Drama ya hivi karibuni inayowahusisha Madaraka Nyerere, mtoto wa Baba wa Taifa, na Steve Mengele, anayejulikana kwa jina maarufu la Steve Nyerere, ni mfano halisi wa uvivu huu wa wanahabari. Badala ya kufanya kazi yao na kuchunguza kwa nini ghafla Madaraka ameamua kumwambia Steve aache kutumia jina la Nyerere, ilhali amekuwa akilitumia kwa miaka mingi, wanahabari wamekopi tu habari kama ilivyo bila kuuliza maswali ya msingi ama kuchunguza nini chanzo halisi ama kisababishi?

Ngoja niwasaidie wanahabari, kwa sababu baada ya kuwafanyia kazi yao ya kiuchunguzi, hatimaye nimegundua kiini cha sakata hili. Hapa kuna siri nzito ambayo inaweza kueleza vurugu hii. Na sio kwamba Steve anaiga sauti ya Mwalimu au anapenda sifa za kuiwa na jina la Nyerere.

Tatizo halisi linamhusisha Emma Lwaitama Nyerere, mwanaharakati maarufu na binti wa mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dr. Azavery Lwaitama, ambaye pia amekuwa akitumia jina la Nyerere kwa muda mrefu sasa. Emma si mwanaharakati wa kawaida; kwa miaka kadhaa amekuwa akidai kuwa ni binti wa Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jambo ambalo si kweli. Rekodi zinaonesha amekuwa hata akikaribishwa majumbani ama Ikulu kwa viongozi wanaompenda na kumthamini Mwalimu Nyerere. Kwao wao kuwa na “binti” wa Mwalimu ilikuwa furaha na fahari ilioje.

Awali alikuwa akijitambulisha kama mtoto wa Mama Maria, baada ya kuhitimu utamu wa jina na kuonja faida zake, akawa “binti” wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Soma Pia: Kumbukizi ya Nyerere: Familia ya Mwalimu Nyerere yawataka wasanii kuacha kutumia jina la Baba wa Taifa kama ubin wao

Sasa, hapa ndipo ulipo mwiba wenyewe, ambao hata Madaraka anaonekana kuuogopa usimchome: Emma amezaa mtoto na Kambarage Joseph Nyerere, ambaye ni mtoto wa kambo mdogo wa Mwalimu, Joseph Nyerere! Kimsingi, Emma angekuwa na haki kabisa ya kutumia jina la Nyerere iwapo wangekuwa wameoana, lakini hawajaoana bado.

Hivyo basi, uhusiano wa Emma na jina la Nyerere ni wa kulazimisha. Au angalau asingekuwa anafanya haya yafuatayo.

Sasa, mambo yalianza kuchafuka pale Emma alipoanza kujitokeza kwenye majukwaa ya kitaifa na kimataifa, akipigia debe ajenda zake za kisiasa, ikiwa ni pamoja na kuunga mkono taifa la Palestina huku akilaani vikali vitendo vya Israel.

Sio siri kwamba msimamo wake huu wa wazi kuhusu Palestina, hasa kwenye majukwaa ya kimataifa, umechokoza hisia za baadhi ya mataifa ya Magharibi.

Mataifa haya yanaona kama ni fedheha ya kidiplomasia kwamba mtu wa familia ya Nyerere anazua kasheshe kwenye masuala nyeti ya kimataifa.

Tuseme tu, "wakubwa" hawajaridhika kabisa. Na kutokana na diplomasia nyeti ya Tanzania ya kutofungamana na upande wowote, kuna dalili kwamba shinikizo limetolewa chini kwa chini. Na hapa ndipo hadithi inakuwa tamu.

Vyanzo vya ndani vinaashiria kwamba msimamo wa Emma kuhusu Palestina, unaoendelea kuakisi msimamo wa zamani wa Julius Nyerere aliyewaunga mkono Wapalestina waziwazi, umewaudhi "wakubwa.” wa magharibi.

Inaonekana wameishinikiza familia ya Nyerere kumvuta Emma chini, wakitaka jina hilo lisihusishwe kabisa na siasa hizo za kimataifa, huku wakipigwa mkwara wa “Hiyo ilikuwa zamani, sasa mchezo umebadilika. Kwa hiyo, mnyamazisheni! Vinginevyo…”

Sasa familia ya Nyerere inafanyaje? Badala ya kumkemea Emma moja kwa moja, wanamtuma Madaraka, msemaji wa familia. Lakini yeye, badala ya kukabiliana na chanzo halisi—Emma kutumia jina la Nyerere kwenye majukwaa ya kimataifa—wanaamua kumshambulia Steve Nyerere, ambaye utaamua mwenyewe kama ana ama hana hatia ya kupewa jina hilo na mashabiki wake kwa kuiga sauti ya Mwalimu.

Steve anakula za uso huku watu wengine wanaotumia jina la Nyerere.Mfano mwingine ni kama huyu Yericko Nyerere, anayejinasibu yu mtaalamu bingwa wa masuala ya ujasusi na dilomasia na uchumi na mwandishi wa vitabu vya masuala ya ujasusi ambao wanaendelea kula bata kwa jina la Mwalimu.

Yericko, ambaye anatokea Iringa (kama Steve), sii Mzanaki na hana uhusiano kabisa na Mwalimu. Lakini Madaraka kammezea!

Kuna dhana kwamba huenda kutoikana na umaarufu alio nao, imeonekana ujumbe utafika haraka zaidi endapo kama watamtumia Steve kama mbuzi wa kafara.

Wengine watamalizana nao baadae mmoja mmoja. Sasa basi, sina haja ya kuwatafunia kila kitu enyi wanahabari, habari ndiyo hiyo. Tafuteni ukweli. Muulizeni Madaraka yote haya. Na kwa upendo wa Mungu, acheni ku-copy na ku-paste! Jifunzeni kuchunguza mambo kama nilivyoiwasaidia hapa!

Alamsiki

View attachment 3127011View attachment 3127012
shida kubwa sio kwanini madaraka analalamika sasa,bali ni je ni halali mtu asiye mtoto wa nyerere kulitumia jina hilo kama ubini wake.Hoja kubwa pia ni kwamba huyo steve nyerere popote anapopiga simu kuomba msaada anapokelewa haraka na kupewa kila aina ya msaada,kwa c/o ya ubini wa nyerere wakati akipiga simu madaraka ambae ndio mtoto wa nyerere watu hao hao hawapokei simu yake.Na mama maria hawapi watoto wake hata senti tano
 
Walipie basi wawe wanapeleka pesa kwa Familia ya Nyerere
Jina Nyerere sio Brand na wala halina hiyo unayoita 'hatimiliki'.

Kuna watu huwapa watoto wao majina ya watawala au matukio makubwa ya wakati huo, kuna kina Nyerere wengi tu waliozaliwa kipindi cha uhuru.

Makongoro Nyerere naye alipie hilo jina?
 
Back
Top Bottom