Emma Lwaitama Nyerere: Kisababishi kilichojificha katika sakata la Madaraka na Steve Nyerere?

Emma Lwaitama Nyerere: Kisababishi kilichojificha katika sakata la Madaraka na Steve Nyerere?

Yaani mtu akiwa radical anageuka anaitwa mwehu? Mara nyingi watu wenye akili nyingi sana na wakawa radicals wanakuwa wanaonekana kama wehu mfano Huyu Tundu Lissu.
Unapokuwa na akili nyingi jamii wakati mwingine haikuelewi na ndio maana wana falsafa wengi wanapokufa ndio baadae watu wanawaelewa mfano Plato na Aristotle.
Hivi unajua hata yule nanilino aliyetangulia mbele za haki alikuwa kidogo na wehu na ndio maana alikuwa na akili nyingi kupindukia.
"Ukiona mtaa unaoishi hakuna mwehu jitathimini huenda unaweza kuwa wewe".....mwisho wa kunukuu
Hii nukuu sikuambii wewe nimeichukua kutoka kwa Signature ya mmoja wa member wetu wa JF naikubali sana hii signature
Naunga mkono hoja
 
Halafu mboni umeuliza kwa nia njema ukajibiwa vizuri ila umekuja kwa jaziba, Yeriko anaitwa Yeriko Yohanesy ila mwishoni kaongeza Nyerere Yeriko ni mzaliwa wa Iringa sio Butiama kwa hio hawezi kua na ubini wa Nyerere yeye sio Mzanaki ni aidha Mbena au Mhehe
Kwahiyo hilo jina la Nyerere ni Wazanaki tu ndiyo wenye Hakimiliki nalo? Mbona kuna majina kibao utayakuta yakitumika maeneo tofauti tofauti? Halafu ebu onesha wapi kwenye comment yangu kuna jazba au ulitaka nikubaliane tu na ulichokiandika!
 
Sio ngonjera waambie hao wanaotumia Jina la Nyerere km ubini wao kupiga Pesa wafute huo ubini watumie ubini wao, sijui unaelewa?
Sijawataja 'hao" nimekuuliza unajua jina halisi la ubini wa Yeriko hadi unasema naye anatumia jina la huyo Nyerere wa Butiama? Ndiyo lilikuwa swali langu kwahiyo usichomeke watu wengine ambao sikukuuliza.
 
Jina Nyerere sio Brand na wala halina hiyo unayoita 'hatimiliki'.

Kuna watu huwapa watoto wao majina ya watawala au matukio makubwa ya wakati huo, kuna kina Nyerere wengi tu waliozaliwa kipindi cha uhuru.

Makongoro Nyerere naye alipie hilo jina?
Yes, mbona wako wengi wa akina Nyerere, Mandera, Rugambwa, Sadam Hussein, Gadaf. Kosa itakuwa kuongeza sifa isiyokuwepo (tuseme kujiongezea mtoto wa baba wa taifa). Waandishi wengine ndio wanaongeza sifa hiyo, wakisia Nyerere wao wataongeza mtoto wa ......
 
Kiongozi wa taifa ni mali ya taifa.
Mkuu hapo kinachofikirisha sana sio jina, bali ni matumizi yake..... kwa mfano hapo juu kwenye profile ya huyo Dada kajiita kabisa Daughter of Late Julius K. Nyerere.
 
Na wale wanaotumia lile jina linaloanza na "J" mbona sijaona tamko lolote? Waendelee kulitumia au wavuliwe hilo jina?
 
Kwa upande wa hao kina Steve Mengere inajulikana kabisa kuwa ni utani tu, yaani usanii..... na ndo maana hawachukuliwi siriazi.

Tatizo huyo binti anayejiita Daughter of Late Julius K. Nyerere, kama ni kweli anajiita hivyo au waandishi tu wamemwita.
 
Sheria za hati miliki zinataka kuandika na kutamka kusichanganye watu

Hivyo ukijiita Nyelele utaambiwa tamka ukitamka Nyelele wanakwambia umevunja hati miliki matamshi yanafanana

Watumie majina ya ubini wao wayakuze na wao yawe makubwa kama la Nyerere

Ni aibu kwa wazazi wao na koo zao kuparamia majina ya ubini wa koo zingine

Wajenge brand ya ubini wa koo zao

Vikao vya koo za baba zao wakae nao wawaambie mnatia aibu na kudhalilisha ubini wetu.

Kama mtu ana kitu hqya akitumia ubini wake watu watamtambua tu

Naungana na madaraka waachane na jina la Nyerere wajenge brand name zao za ubini wa kwao
Umeandika ushuzi. Steve ni msanii kwahiyo lazima awe na jina la kisanii. Hilo la Nyerere ndo limemkaa na kukubalika. Ungeenda DRC ndo ungechanganyikiwa hayo majina hayo. Huko kuna Bill Clinton, Saddam Hussein, Ibrahimovic, Anelka, na mengine mengi. Koffi Olomide alitaka kujiita Benedict wa 17 ikabidi kanisa liingilie kati na kumkataza.
 
Wazungu wakipiga marufuku msitumie majina yao wengi humu mtabaki jina la " wemtu" au "we tall, au short, au bonge".
Wazungu na warabu wenye koo zao huko wakataze majina yao yasitumike na watu wasio koo zao.
Nataka nipime umburula hapa.
Kuna mfanyakazi mwenzangu anaitwa Mackenzie kwa hiyo ile familia ya mmojawapo wa mawaziri wa Jomo Kenyatta mzungu Bruce Mackenziei familia yake wanaweza zuka huku kudai jina lao lisitumiwe.
Acheni ubinafsi nyie watoto wa J K Nyerere hata wajiiteje hakuna atakayekuwa baba wa taifa au kuwa kama yeye.
 
Hii ni ngumu! Hivi siwezi kuzaa mtoto nikamwita Julius Nyerere? Hivi senior counsel Prof PLO Lumumba anauhusiano wowote na Patrice Lumumba wa Congo zamani Zaire?
 
Kwahiyo hilo jina la Nyerere ni Wazanaki tu ndiyo wenye Hakimiliki nalo? Mbona kuna majina kibao utayakuta yakitumika maeneo tofauti tofauti? Halafu ebu onesha wapi kwenye comment yangu kuna jazba au ulitaka nikubaliane tu na ulichokiandika!
Una jazba saana haya onyesha kwa Wabena na Wahehe nionyeshe ubini wa Nyerere nionyeshe Mbena mwenye ubini wa Nyerere, acheni hizo halafu mnatafuta sympathy za kijinga kutaka muonewe huruma kwani ni lazima mtumie jina la Nyerere wakati hamhusiki nae namaanisha kuhusika nae kifamilia watoto na ndugu wa chimbuko lake yeye, hapa nazungumzia ubini as if Nyerere ni Baba aliewazaa wakati Nyerere ana watoto wake na wajukuu wake na vitukuu, sasa inaleta contradiction sababu nyinyi mnalitumia jina la Nyerere kibiashara kupiga Pesa kutengeneza deals n some sort like sasa kwanini msitafute majina mengine kwanini mtumie mtelezo wa Jina Nyerere kujitengenezea Pesa? Mkipigiwa simu hampokei
 
Sijawataja 'hao" nimekuuliza unajua jina halisi la ubini wa Yeriko hadi unasema naye anatumia jina la huyo Nyerere wa Butiama? Ndiyo lilikuwa swali langu kwahiyo usichomeke watu wengine ambao sikukuuliza.
Ndio nimekwambia watafute majina yao ya ukoo sio kuchomeka ubini wa Nyerere, Steve Machele atumie Machele km ubini wake Yeriko Mwambele atumie Mwambele km ubini wake waache kulitumia jina la Nyerere kibiashara wanatengeneza Pesa kupitia Jina la Nyerere wenyewe hawataki sasa, kuna yule Jamaa anaemuiga JK jina lake anajiita JK Comedian unaelewa vizuri ila ana jina lake hajiiti Justin Kikwete au Jackson Kikwete unanielewa vizuri lakini?
 
Una jazba saana haya onyesha kwa Wabena na Wahehe nionyeshe ubini wa Nyerere nionyeshe Mbena mwenye ubini wa Nyerere, acheni hizo halafu mnatafuta sympathy za kijinga kutaka muonewe huruma kwani ni lazima mtumie jina la Nyerere wakati hamhusiki nae namaanisha kuhusika nae kifamilia watoto na ndugu wa chimbuko lake yeye, hapa nazungumzia ubini as if Nyerere ni Baba aliewazaa wakati Nyerere ana watoto wake na wajukuu wake na vitukuu, sasa inaleta contradiction sababu nyinyi mnalitumia jina la Nyerere kibiashara kupiga Pesa kutengeneza deals n some sort like sasa kwanini msitafute majina mengine kwanini mtumie mtelezo wa Jina Nyerere kujitengenezea Pesa? Mkipigiwa simu hampokei
Unaendeleza ngonjera tu,nimekuuliza swali ambalo umeshindwa kulijibu sasa umeona ubwekebweke kama mbweha tu,eti nitumie jina la Nyerere! Nyerere kwangu si lolote si chochote kwahiyo sina sababu hata moja ya kutumia jina lake na haiwezi kutokea nikajinasibisha naye kwa lolote labda wewe na wapumbavu wenzako mnayetamani kumuabudu kwa kumuona ndiye mungu wenu.
Sitoendelea kujibishana na wewe maana labda naongea na kichaa bila kujua,ugua pole.
 
Ndio nimekwambia watafute majina yao ya ukoo sio kuchomeka ubini wa Nyerere, Steve Machele atumie Machele km ubini wake Yeriko Mwambele atumie Mwambele km ubini wake waache kulitumia jina la Nyerere kibiashara wanatengeneza Pesa kupitia Jina la Nyerere wenyewe hawataki sasa, kuna yule Jamaa anaemuiga JK jina lake anajiita JK Comedian unaelewa vizuri ila ana jina lake hajiiti Justin Kikwete au Jackson Kikwete unanielewa vizuri lakini?
Siwezi kumuelewa kichaa sina kipaji hicho.
 
Back
Top Bottom