Kwa wale wanaofuatilia mambo ya utabiri wa Nostradamus na hata wa watu wa Mayan kule South America wanasema Dunia inaweza kufika kikomo mwaka 2012 karibu na tarehe 21 Dec. Kumekuwa na documentaries nyingi kutoka History channel zikielezea matukio mbalimbali yanayoashiria ujio wa tukio hilo. Je wewe binafsi unaamini huo ndio utakuwa mwisho wa dunia au waliotafsiri maandiko ya Nostradamus na Mayan wameshindwa kung'amua ukweli? Kumbuka kuna utabiri wa matukio mbalimbali ambao ulifanywa na hawa watu ukiwa na ukweli ndani yake na hayo matukio yalitokea kweli.
Geeque-nashukuru kwa kutupa updates za kinachoendelea katika ulimwengu huu wa giza la ufahamu. Nimesoma posts za wadau wengi hapa nao wanaonekana suala la kuwapo au kutokuwapo kwa mwisho wa dunia kana kwamba ni jambo la hisia za mtu binafsi. Yaani mtu anajisikilizia msisimko wake unamwambia nini kisha anasema, "mwisho wa dunia haupo..."
Mimi ni Mkristo na ninaamini kwamba kuna mwisho wa Dunia kwa mujibu wa Biblia. Na Biblia inaweka wazi utangulizi wa matukio ambayo hayana budi kutokea kabla ya ujio wa Yesu Kristo, Mungu na Mfalme wa Wafalme. Katika kitabu cha 2 Wathethalonike 2 anaelezea kwa urefu mambo ambayo nilazima yatimie kabla Yesu hajarudi mara ya pili, na tukio kubwa ni Upapa kuchukua mamlaka ya kidini na kisiasa ulimwenguni, na baada ya hapo kuwatesa wakristo wanaoshika sheria na ushuhuda wa Yesu.
Nina watakaofanikisha Papa kuchukua utawala wa Ulimwengu huu? Ni Marekani, vikundi vya siri (secret societies), na Jesuits. Sasa nitakwenda kueleza kwa kifupi Utabiri wa Nostradamus wa mwisho wa Dunia, na Movies nyingi pamoja na documentaries ambazo zinaonesha kwamba December 21, 2012 ndio mwisho wa dunia.
Kimsingi kuna kundi la waabudu shetani ambao wanapanga mikakati ya hali ya juu kuhusu kuuendesha ulimwengu huu. Kundi hili linaundwa na watu kama Illuminat na Freemasons. Mfano katika upande wa Movies kuna makampuni 12 ndani ya HOLLYHOOD ambayo yanaendeshwa na Freemasons wa degree za juu ambao wanatumia music na film industry kufikisha ujumbe kwa dunia ambao mwishowe unatoa maandalizi ya kiakili kupokea tukio ambalo watalifanya wao wenyewe. Nitakupa mfano kido, Movie ya Terminator ilitoka miaka mingi kabla ya Sept 11 incedence lakini kuna scene ambayo inaonesha maneno haya "WARNING SEPTEMBER 11", na mengine mengi ambayo yanashadadia kwamba watabiri na watekelezaji wa unabii na walewale. Yaani sawa na mini niseme Kesho G atakufa alafu nimvizie nimpige risasi mwenyewe!
Kimsingi tarehe 21 December 2012 ninachofahamu mimi ni kwamba nitarehe ambayo kuna tukio linajulikana au wanaita "OMEGA POINT". Omega Point ni jambo au tukio ambalo linakuwa limepangwa na waabudu shetani kwa kusudi la kupeleka ujumbe mzito au kuanzisha mipango mikubwa kueleke "NEW WORLD ORDER". Mfano wa tukio hilo ni Sep 11. 21 December 2012 David Cameroon anatarajiwa kutoa tamka lenye agenda ya kishetani yaani NWO kuhusiana na suala la usimamizi wa kidunia wa Mazingira. Tukio hilo litapelekea kama ilivyokuwa kwa Sept 11 nchi nyingi zilidhie kutoa sovereignity juu ya kundi la watu wachache ambao wana agenda ya kuutawala ulimwengu. Kwahiy Nastro, Documentaries na Movie kama ile ya 2012 zoote zinatuandaa kwaajili hiyo.
Napenda nimaliza kwa hekima kama alivyoshauri Mzee wa Upako, japo simuamini ikija kwa misingi ya imani, yeye anasema hakuna haha ya kumpaisha shetani kwa kusema kazi zake bila kuzungumza kwamba mwisho wake unakuja kwa haraka na wale wanaomwamini Yesu watapata Ushindi.
Ukweli ni kwamba NWO inakuja lakini tumaini lipo katika Kristo Yesu ambaye atawaokoa waliomuamini na wanaozishika amri zake na ushuhuda wake. Yaana anaandika uwe mwamifua hata kufa nami nitakupa taji ya uzima. Hilo ndilo tumaini letu katika kipindi cha NWO ambacho ni mahususi kwaajili ya kufutilia mbali watoto wa Mungu. Chagua sasa kuwa upande wa Mungu kabla hakijaja kipindi kibaya.....