End of the World: Nostradamus 2012, December 21 - Mayan Prophecy

End of the World: Nostradamus 2012, December 21 - Mayan Prophecy

Kwa wale wanaofuatilia mambo ya utabiri wa Nostradamus na hata wa watu wa Mayan kule South America wanasema Dunia inaweza kufika kikomo mwaka 2012 karibu na tarehe 21 Dec. Kumekuwa na documentaries nyingi kutoka History channel zikielezea matukio mbalimbali yanayoashiria ujio wa tukio hilo. Je wewe binafsi unaamini huo ndio utakuwa mwisho wa dunia au waliotafsiri maandiko ya Nostradamus na Mayan wameshindwa kung'amua ukweli? Kumbuka kuna utabiri wa matukio mbalimbali ambao ulifanywa na hawa watu ukiwa na ukweli ndani yake na hayo matukio yalitokea kweli.

Geeque-nashukuru kwa kutupa updates za kinachoendelea katika ulimwengu huu wa giza la ufahamu. Nimesoma posts za wadau wengi hapa nao wanaonekana suala la kuwapo au kutokuwapo kwa mwisho wa dunia kana kwamba ni jambo la hisia za mtu binafsi. Yaani mtu anajisikilizia msisimko wake unamwambia nini kisha anasema, "mwisho wa dunia haupo..."

Mimi ni Mkristo na ninaamini kwamba kuna mwisho wa Dunia kwa mujibu wa Biblia. Na Biblia inaweka wazi utangulizi wa matukio ambayo hayana budi kutokea kabla ya ujio wa Yesu Kristo, Mungu na Mfalme wa Wafalme. Katika kitabu cha 2 Wathethalonike 2 anaelezea kwa urefu mambo ambayo nilazima yatimie kabla Yesu hajarudi mara ya pili, na tukio kubwa ni Upapa kuchukua mamlaka ya kidini na kisiasa ulimwenguni, na baada ya hapo kuwatesa wakristo wanaoshika sheria na ushuhuda wa Yesu.

Nina watakaofanikisha Papa kuchukua utawala wa Ulimwengu huu? Ni Marekani, vikundi vya siri (secret societies), na Jesuits. Sasa nitakwenda kueleza kwa kifupi Utabiri wa Nostradamus wa mwisho wa Dunia, na Movies nyingi pamoja na documentaries ambazo zinaonesha kwamba December 21, 2012 ndio mwisho wa dunia.

Kimsingi kuna kundi la waabudu shetani ambao wanapanga mikakati ya hali ya juu kuhusu kuuendesha ulimwengu huu. Kundi hili linaundwa na watu kama Illuminat na Freemasons. Mfano katika upande wa Movies kuna makampuni 12 ndani ya HOLLYHOOD ambayo yanaendeshwa na Freemasons wa degree za juu ambao wanatumia music na film industry kufikisha ujumbe kwa dunia ambao mwishowe unatoa maandalizi ya kiakili kupokea tukio ambalo watalifanya wao wenyewe. Nitakupa mfano kido, Movie ya Terminator ilitoka miaka mingi kabla ya Sept 11 incedence lakini kuna scene ambayo inaonesha maneno haya "WARNING SEPTEMBER 11", na mengine mengi ambayo yanashadadia kwamba watabiri na watekelezaji wa unabii na walewale. Yaani sawa na mini niseme Kesho G atakufa alafu nimvizie nimpige risasi mwenyewe!

Kimsingi tarehe 21 December 2012 ninachofahamu mimi ni kwamba nitarehe ambayo kuna tukio linajulikana au wanaita "OMEGA POINT". Omega Point ni jambo au tukio ambalo linakuwa limepangwa na waabudu shetani kwa kusudi la kupeleka ujumbe mzito au kuanzisha mipango mikubwa kueleke "NEW WORLD ORDER". Mfano wa tukio hilo ni Sep 11. 21 December 2012 David Cameroon anatarajiwa kutoa tamka lenye agenda ya kishetani yaani NWO kuhusiana na suala la usimamizi wa kidunia wa Mazingira. Tukio hilo litapelekea kama ilivyokuwa kwa Sept 11 nchi nyingi zilidhie kutoa sovereignity juu ya kundi la watu wachache ambao wana agenda ya kuutawala ulimwengu. Kwahiy Nastro, Documentaries na Movie kama ile ya 2012 zoote zinatuandaa kwaajili hiyo.

Napenda nimaliza kwa hekima kama alivyoshauri Mzee wa Upako, japo simuamini ikija kwa misingi ya imani, yeye anasema hakuna haha ya kumpaisha shetani kwa kusema kazi zake bila kuzungumza kwamba mwisho wake unakuja kwa haraka na wale wanaomwamini Yesu watapata Ushindi.

Ukweli ni kwamba NWO inakuja lakini tumaini lipo katika Kristo Yesu ambaye atawaokoa waliomuamini na wanaozishika amri zake na ushuhuda wake. Yaana anaandika uwe mwamifua hata kufa nami nitakupa taji ya uzima. Hilo ndilo tumaini letu katika kipindi cha NWO ambacho ni mahususi kwaajili ya kufutilia mbali watoto wa Mungu. Chagua sasa kuwa upande wa Mungu kabla hakijaja kipindi kibaya.....
 
Hakuna mwisho wa dunia kama ule tunaoufikiria -
Kwanini unadhani kwamba hakuna mwisho wa dunia...

ila mwisho wetu na mwisho wa kila kiumbe. Kwani dunia ikiisha kutakuwa na nini, uumbaji mwingine au?
Maswali mazuri, Biblia inatoa majibu kwa usahihi sana jitahi kusoma kitabu cha Ufunuo sura ya 13 mpaka ya 22 inatoa majibu ya maswali yako yote.
Ninachoamini ni kwamba wewe na mimi tutakufa lakini watu wengine na viumbe vingine wataendelea/vitaendelea kuzaliwa na hivyo ndivyo itakavyokuwa muda wote.
Imani yako inaonekana kuwa ni nzuri sana isipokuwa imejikita katika hisia zako binafsi. Kuna Mungu aliyefanya mbingu na nchi ambaye anaiongoza historia ya ulimwengu huu na yeye ndiye anayezuia machafuko yasitokee juu ya nchi. Jaribu kusoma Biblia katika kitabu cha ufunuo utapata Jibu, ukikwam ni PM tusaidiane.
 
Kama dunia haikufika kikomo mwaka 2000 na 'Y2K', basi kwa sasa na subiri mwisho wa dunia ulioandikwa ktk vitabu vitakatifu tu.
 
Kama dunia haikufika kikomo mwaka 2000 na 'Y2K', basi kwa sasa na subiri mwisho wa dunia ulioandikwa ktk vitabu vitakatifu tu.

Kitu gani kilikufanya uamini kuwa mwisho wa dunia ingekuwa mwaka 2000?
 
Hakuna mwisho wa dunia kama ule tunaoufikiria - ila mwisho wetu na mwisho wa kila kiumbe. Kwani dunia ikiisha kutakuwa na nini, uumbaji mwingine au? Ninachoamini ni kwamba wewe na mimi tutakufa lakini watu wengine na viumbe vingine wataendelea/vitaendelea kuzaliwa na hivyo ndivyo itakavyokuwa muda wote.

wewe umenena
 
Napenda niseme kwamba utabiri huu ni uzushi kwa mujibu wa Biblia. Katika MATHAYO 24 yote Yesu alieleza juu ya mwisho wa dunia kwa maana ya kuja kwake mara ya pili lakini mstari wa 36-49, anasema yeye Yesu mwenyewe hajui, malaika hawajui ila baba peke yake. Ni kama wakati wa Nuhu. Pia, mstari wa 42-44 alisema hata wanafunzi wake hawatajua siku ya kuja kwake kwa hiyo wakeshe wakati wote na kujiweka tayari. Sisi wanadamu tumepewa kujua majira kwamba yamekaribia lakini siyo tarehe. Kwa ujumla hakuna dalili au ishara ambazo zimesalia.Ambaye bado hajajiandaa ajiweke tayari kuonana na Mungu ( AMOSI 4:12) maana atakuaj kama mwivi KWA WALE WASIOJIANDAA( MATHAYO 24:42-44), (MATHAYO25:13). Wakati wanaposema kuna aman ndipo anapokujai! (1WATHESALINIKE 5:1-11) Je wewe uko kundi lipi?
 
Mambo mengi yatatabiliwa na yatatimia lakini hili la mwisho wa Dunia ni Siri ya Mungu. Mambo mengine husababishwa na Shetani na mawakala wake, hivyo hutumia watumwa wake kudokeza mipango aliyoiweka. Hili la Mwisho wa Dunia piga ua galagaza hakuna ajuaye bali MUNGU pekee!
 
fafaanua mwisho wa dunia utakuwaje yani dunia itagawanyika au kutakuwa na tukio lipi litakalo ashilia kuwa sasa ni mwisho wa dunia
 
swala ni kwamba mwaka huu kutakuwa na tukio kubwa linalohusiana na new world order
 
Kwa wale wanaofuatilia mambo ya utabiri wa Nostradamus na hata wa watu wa Mayan kule South America wanasema Dunia inaweza kufika kikomo mwaka 2012 karibu na tarehe 21 Dec. Kumekuwa na documentaries nyingi kutoka History channel zikielezea matukio mbalimbali yanayoashiria ujio wa tukio hilo. Je wewe binafsi unaamini huo ndio utakuwa mwisho wa dunia au waliotafsiri maandiko ya Nostradamus na Mayan wameshindwa kung'amua ukweli? Kumbuka kuna utabiri wa matukio mbalimbali ambao ulifanywa na hawa watu ukiwa na ukweli ndani yake na hayo matukio yalitokea kweli.
Jamani mbona neno la MUNGU liko wazi tu, mwisho wa uovu na dunia fisadi upo ila watakatifu wote waliomwamini YESU/YAHSHUA kuwa ni MWANA wa MUNGU aliyekufa akafufuka kwa ajili ya dhambi ya ulimwengu na wanadamu hao hawana mwisho bali watakuwa katika ulimwengu mpya usio na dhambi, maumivu, wala shida ya aina yeyote, ulimwengu huu/ufalme utakuwa ni mtakatifu mno kwani MFALME wake atakuwa ni YESU mwenyewe..AMINA
 
Jamani mbona neno la MUNGU liko wazi tu, mwisho wa uovu na dunia fisadi upo ila watakatifu wote waliomwamini YESU/YAHSHUA kuwa ni MWANA wa MUNGU aliyekufa akafufuka kwa ajili ya dhambi ya ulimwengu na wanadamu hao hawana mwisho bali watakuwa katika ulimwengu mpya usio na dhambi, maumivu, wala shida ya aina yeyote, ulimwengu huu/ufalme utakuwa ni mtakatifu mno kwani MFALME wake atakuwa ni YESU mwenyewe..AMINA

Hilo ni neno la MUNGU wako, kuna wengine hawamwamini mungu wako kama wewe usivyomwamini MUNGU wao!!!!! Safari hii hata Sayansi inatetesika kuwa ngoma iko karibu...teh teh!DOOOOOM NGKAPA NGKAPAAA!
 
Hilo ni neno la MUNGU wako, kuna wengine hawamwamini mungu wako kama wewe usivyomwamini MUNGU wao!!!!! Safari hii hata Sayansi inatetesika kuwa ngoma iko karibu...teh teh!DOOOOOM NGKAPA NGKAPAAA!
Ni kweli ni MUNGU wangu wala hujakosea. Mimi namuamini yule wa Ibrahimu Isaka na Yakobo..wewe je?
 
Siku wala saa mwanadamu hatoijua..ila watu wema na wacha MUNGU watafahamu majira. Timeline ya nyakati za mwisho soma Daniel 9: 25-27 "25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa kwa amri kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba;na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki,naam,katika nyakati za taabu. 26 Na baada ya yale majuma sitini na mawili,masihi atakataliwa mbali,naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu;na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika,na hata mwisho ule vita vitakuwapo;ukiwa umekwisha kukusudiwa. 27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja;na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu;na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu;na hivyo,hata ukomo,na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu". Jambo la msingi la kuzingatia ni kuwa katika hali ya kawaida juma moja lina siku 7, kwa MUNGU (lugha ya unabii) siku moja ni mwaka mmoja, pia ki-Bibilia mwaka una siku 360. Ukimuomba YESU akuongoze na kusoma mafungu haya utagundua kuwa majuma 69 (fanya mahesabu utajua) yalikamilishwa na kujengwa YERUSALEM, Kusulubiwa kwa YESU. Sasa tuko katika gap (church age) tukisubiri miaka 7 ya mwisho na hii itaanza mara tu baada ya mpinga kristo kufunuliwa (wenye hekima za MUNGU watafahamu) atakapo fanya mkataba wa amani kati ya Israel na Parestina mkataba huu utaruhusu kujengwa tample kama lile la Mfalme Solomon lililobomolewa mahali pale pale, inasemekana sasa kuna msikiti wa Al Aqsa lakini katikati ya miaka 7 (baada ya 3.5) ataingia katika hilo hekalu na kufanya chukizo la uharibifu..vyanzo vingi vinasema atasema kuwa yeye ndo KRISTO/MUNGU hapo ndipo atakapoanza kutawala dunia kwa nguvu na hata ile 666 ndo itaanza kutumika baada ya 3.5 iliyobaki kukamilika kwa dhiki kuu, YESU KRISTO mfalme wa wafalme ataonekana mawinguni akija pamoja na jeshi lote la mbinguni, ujio wake utakuwa kama alivyoondoka na kila jicho litamwona ndipo atakapoangamiza dhambi kwa pumzi yake takatifu, shetani atafungwa kwa miaka 1000................someni mtaelewa. Cha msingi ndugu zangu ni kumuamini KRISTO wa kweli kwani ndo njia ya uzima na kweli..AMEN
 
Back
Top Bottom