Endapo hatutokusanya kodi kwa wingi, tutapata wapi fedha za kuendeshea nchi?

Endapo hatutokusanya kodi kwa wingi, tutapata wapi fedha za kuendeshea nchi?

Yes kwa miezi michache itapungua kwasabab tra kawakataza kwenda kuwafungua watu account zao na kukwapua hela, kakataza kwenda kutishia case za uhujumu uchumi ili mtu aogope na atoe hela atakama anaonewa...unahisi mama hayo ayajui ww unayajua zaidi huyu mama kawa makamu wa raisi kwa miaka 6 anajua matatizo yte na namna ilivokuwa hata zaidi yako wewe
Kwahiyo kila mwezi TRA wanafungia watu biashara na kukwapua hela. Toka wameanza kufanya hiyo kazi kwa miaka 5 bado kuna wafanyabiashara kweli? Si biashara zote zingekua zimefungwa na kungekua hakuna wakulipa kodi. Hili suala linafikirisha sana.

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Wakati wa kikwete Kodi ilikuwa haikusanywi na ilikuwa inakusanywa vipi,wakati wa mkapa je? Yani njoo nikwambie wafanyabiashara Kodi watalipa tu ila tu mfumo wakulipa Kodi uwe huru na amani wakati wa jpm kulikuwa Kuna mambo yakijinga Sana ya tra ili mradi tu wa meet target walikuwa wanakamua wananchi..sio Siri Kodi wakati wa jpm ilikuwa inapanda kwasababu almost parefu haikuwa ya halali watu wanatishia kufunguliwa case, mtu ulipewa tax clearance leo baada ya mwaka unaitwa unaambiwa unadaiwa mil 400 haha tuseme ukweli maguful hakutaka kutengeneza mfumo wa ulipaji Kodi Tanzania ila alitaka hela ipatikane kwa namna yyte ile private sector wakati wa jpm ilidrop sana
Na makusanyo yalikuaje? Kipindi cha JK na JPM? Mbona hutoi figure, tujue nani alikua anafanya vizuri.

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Kamuulize CAG atakuonyesha kodi yako inapoenda
 
Endapo hatutokusanya kodi kwa wingi Je tutapata wapi fedha za kuendeshea nchi?

Mfano naomba mnisaidie maswali haya:

1. Tutapata wapi fedha za kuwalipa wafanyakazi mishahara kila mwezi?

2. Tutapata wapi fedha za kuwakopesha wanafunzi wa vyuo vikuu mikopo ya elimu?

3. Tutapata wapi fedha za miradi? Miradi ya maji, barabara, umeme, shule na hospitali.

4. Tutapata wapi fedha za kununulia vifaa na madawa ya hospitalini.

Naombeni majibu ya haya maswali. Tiririka majibu yako kadri uwezavyo.

Nani kasema kodi isikusanywe? Isiyotakikana ni kodi ya dhuluma!

Serikali inayodhulumu pesa au maisha ina jina lisilopendeza.
 
Back
Top Bottom