Endapo hatutokusanya kodi kwa wingi, tutapata wapi fedha za kuendeshea nchi?

Endapo hatutokusanya kodi kwa wingi, tutapata wapi fedha za kuendeshea nchi?

Hashimu lwenje

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2017
Posts
415
Reaction score
361
Endapo hatutokusanya kodi kwa wingi Je tutapata wapi fedha za kuendeshea nchi?

Mfano naomba mnisaidie maswali haya:

1. Tutapata wapi fedha za kuwalipa wafanyakazi mishahara kila mwezi?

2. Tutapata wapi fedha za kuwakopesha wanafunzi wa vyuo vikuu mikopo ya elimu?

3. Tutapata wapi fedha za miradi? Miradi ya maji, barabara, umeme, shule na hospitali.

4. Tutapata wapi fedha za kununulia vifaa na madawa ya hospitalini.

Naombeni majibu ya haya maswali. Tiririka majibu yako kadri uwezavyo.
 
Duniani kote pale mheshimiwa rais nchi ili iweze kujiendesha lazima ikusanye kodi kwanamna yoyote ile kodi ilikuwepo tangu zama za mitume.

Hakuna mfanyabiashara yoyote yule atakuwa anautayari kulipa kodi bila kumuwekea sheria na utaratibu na aisipo ufuata sheria itachukua mkondo wake na akisema anafunga kwakuwa ananyanyasika sawa na aende tu...Nibora ukawa na wafanyabiashara kumi wanolipa kodi kuliko kuwa na wafanya biashara mia wasiolipa kodi.

kuna mambo jana uliyaongea mpaka unashangaa hivi mama samia kaamua kuwa upande wa matajiri na wafanya biashara angalia haya kwa uchache:-

KODI ZA DHULUMA HUTAKI
Yani maana yake nikwamba Magufuli alikuwa anadhulumu wafanyabiashara kiasi kwamba walikuwa wanafunga biashara zao.

Mama kudai kilichochako nidhuluma na hiyo dhuluma unayoisema kwa msingi wako kuwa wanatishiwa siyo kweli.

WAFANYABIASHARA WENGI WAMEFUNGA BIASHARA
Wengi waliofunga walikuwa hawalipi kodi na wezi na wengine walikuwa ni wauza unga lazima watafunga tu.

Mbona bakhresa yupo hajafunga mo yupo hajafunga sayona wapo peps wapo coka wapo n.k mbona hawa wajafunga au wao siyo wafanya biashara ni mainjinia.

Hao wengi ndiyo wale waliokuwa wameuwa flow meter,ndiyo hao walikuwa hawatoi risiti,ndiyo hao walikuwa hawalipi kodi bandarini sasa watafunga tu kwa msimamo wa magufuli.

Sasa kwa huo uamuzi wako tutawarudisha tena wezi.

TUTAYUMBA
Umekiri kwakusema kwa uamuzi uliochukua ndani ya miezi mitatu tutayumba ila tutakuja kukaa sawa.

Jamani mama hiyo unacheza kamali isipokaa sawa yaani inamaana ndani ya miezi mitatu tutakuwa tunakusanya kodi ndogo ili kubembeleza wafanyabiashara.

Mie yangu macho waziri wako hana muda utamtumbua maana hapo umetoa uhuru watu kukumbia leo tumepata mia mbilinkumbe alipata elfu nyengine kabania.

NIBORA UKAWA NA WALIPAKODI WATATU WANAOKULIPA VIZURI KULIKO KUWA NA NA MIA WASIO NA FAIDA.

Hicho kipindi wafanyabiashara wanakimbia wanafungabishara tuliona ndege,barabara , elimu bure, madaraja sasa ngoja tuone ila nakuapia mpaka unaondoka madara hutaleta kitu kipya...Na siku ukiacha madaraka tu hao hao wataanza kukuponda ngoja muda uongee.
 
Kama umegundua Tz ikiombewa mabaya hua hayatokei.

Alianza Lisu.

Wakaja netizens.

Wote wanatabiri nchi kupotea na maandamano na hayajawa.

Sijasikia sehemu kasema TRA iache kukusanya kodi. Huu uhuru wa kuandika kila mnachojisikia mngeweza kumkosoa JPM?

Una nyuzi ngapi za kumkosoa JPM?
 
Kipindi cha utemi utemi kimeisha, mama piga kazi watu wapumue - mnakamua ngombe hadi atoke damu laahh

Kodi kodi hadi mnaingia kwenye acc ya watu bila aibu...!! mnaanza kunyofoa hela loooh
 
Back
Top Bottom