Endapo hatutokusanya kodi kwa wingi, tutapata wapi fedha za kuendeshea nchi?

Endapo hatutokusanya kodi kwa wingi, tutapata wapi fedha za kuendeshea nchi?

Kukusanya kodi kweli ulikuwepo tangu enzi
Ila ukusanyaji umebadilika sana kwani hata waliotutangilia sana pia walipitia ukusanyaji wa kibabe na dhulma

Lakini walibadilika taratibu na kubadili mifumo ya ukusanyaji wa kodi
Tunahitaji elimu sana kuhusu kodi na pia kuongeza wigo la ukusanyaji ila kumtoza faini mfanyabiashara 3m kisa hajatoa risiti ni mtihani na unafungua ulaji kuwa mkubwa pia
 
Ashakum si matusi na wala sitaki kuubagaza utu wako ila ni uzi wa ajabu kuwahi kuusoma hapa duniani.

Kodi ambazo zinatokana na ubabe si halali kama ulimpa mtu Tax clearance certifaces za miaka yote huko nyuma then unakuja unamuambia kuna kodi hakulipa ya billions of money ni sawa hiyo? Tupo na MTU WA DINI HASWAA hahitaji kumuita Mufti tujue yeye ni mcha Mungu just ongea yake na fikra zake tu zinatosha.
 
Endapo hatutokusanya kodi kwa wingi Je tutapata wapi fedha za kuendeshea nchi?
Tusipotoshe alichoongea Mama Samia, amesema ikusanywe kodi ya haki, sasa unakwenda kumkaba mtu unampora then anafunga biasahara. hio kodi utaipata wapi next time? Ukienda TRA kaangalie idadi ya biashaar zilizofungwa VS idadi ya biashara zilizofunguliwa
 
Tuliza wenge ,ni wapi mama alisema hakusanyi kodi? Ile clip yake aliyowapa kina lameck madelu(Mwigulu) target ya makusanyo ya trilioni 2 kwa mwezi ni nini ile? mama hataki fedha za dhuluma ambazo kikundi cha kina bashite(task force) kilikuwa kinakusanya.
 
Hakuna aliyesema kodi isikusanywe kwa wingi. Ikusanywe kwa AKILI/WELEDI na si MAGUVU.

Kaa na watu, panga nao jinsi watakavyolipa madeni yao ya kodi si kufunga biashara na kunyang'anya bidhaa na pesa kwenye account. Nani kesho atakulipa kodi?

Weka mifumo rafiki, halisia na ya haki. Utapata kodi yako na zaidi ya hiyo ya kutumia maguvu na kuumiza watu.
 
Tusipotoshe alichoongea Mama Samia, amesema ikusanywe kodi ya haki, sasa unakwenda kumkaba mtu unampora then anafunga biasahara. hio kodi utaipata wapi next time? Ukienda TRA kaangalie idadi ya biashaar zilizofungwa VS idadi ya biashara zilizofunguliwa
MATAGA na SUKUMA-GANG wanatafuta pa kutokea, kwani nyerere na hao wote waliopita kodi zilikuwa hazikusanywi? huyu "mwendazake" kaja na staili ya "kupora kodi" na si kukusanya!
 
Nyie mashetani mlimnyang'anya Shayo bilioni 2 zote kwenye akaunti yake akajiua.

Watu wa Tabata hadi leo wanamkumbuka sana jirani yao.

Dhuluma sio nzuri, hivi sasa Magu kakutana uso kwa uso na Shayo kuzimu.
 
Back
Top Bottom