Mfumo wa Uchezaji wa Mpira wa Afrika Kusini na hata katika Ligi Kuu yao ya PSL unatumika na hata katika Academies zao ni Mpira wa Kasi na Nguvu.
Pia usisahau kuwa sehemu Kubwa ya Afrika Kusini ni Baridi sana hivyo Kisayansi Mtu anayefanya Mazoezi katika Ukanda wa Baridi hulazimika kutumia Nguvu nyingi ili pia kutengeneza Joto la Mwili ili Kulibalansi hali ambayo husaidia kuongeza Kasi ya Mwili kutenda Kazi na hata Mtu Kuwajibika zaidi kuliko wale wanaoishi maeneo ya Joto Kali kama huku Kwetu Afrika Mashariki au kule Sudan.
Hivyo baada ya Vilabu vya Afrika Kusini kujua hilo na Wao Kiufundi wakiwa wanataka Kusajili Wachezaji wa Kimataifa hutumia Vigezo hivi hivi vikubwa Viwili vya kuangalia je, na Wao wanatoka katika nchi zenye Baridi na Ligi zao ni ya matumizi makubwa ya Nguvu na Kasi?
Chunguza hata hao Wachezaji wa Kigeni wa Mamelodi Sundowns FC nchi wanazotoka ni zenye Hali ya Hewa inayofanana na ya Afrika Kusini na Mfumo wa Mpira kama Wao wa Kasi na Nguvu.
Ni haya tu Mkuu wangu. Siku Njema.