Endesha kwa Umeme, Nishati Safi na Nafuu zaidi Barabarani.

Endesha kwa Umeme, Nishati Safi na Nafuu zaidi Barabarani.

Tanesko punguzeni bei ya umeme bwawa lina zalisha umeme wa kutosha mnafeli wapi?
Sera za ccm, ndio zinaleta yote haya, kwa hili nawatetea Tanesco. Hii ipo deep, tuwalaumu hawa wanasiasa wanaobadirishana viti vya madaraka kila miaka 5, kila mtu anakuja na lake ni mkanganyo
 
Habari ndugu mteja, asante kwa kuwasiliana nasi.

Suala la bei za umeme linasimamiwa na EWURA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Mchakato huo ni endelevu, na umma utajulishwa kuhusu mabadiliko yoyote pindi utakapofika wakati muafaka.

Asante. ^FL
Lini mliwahi kupandisha bei halafu mkashusha?
Ewura ni wanufaika wa bei ya umeme wana mgao wao, hii nchi imelaaniwa.
 
Lini mliwahi kupandisha bei halafu mkashusha?
Ewura ni wanufaika wa bei ya umeme wana mgao wao, hii nchi imelaaniwa.
Bei ya sasa haijapandishwa tokea 2016 licha ya mabadiliko mbali mbali za kiuchumi, na uendeshaji.

EWURA ni mamlaka inayojitegemea yenye majukumu yake
 
Hivi nani aliwashauri Kodi ya nyumba ilipwe kupitia tanesco.wengine tumepanga lakini kila mwezi tunakatwa 1500 .
Mwenye nyumba hakai hapo hamuoni mnatutesa?
Habari ndugu mteja, asante kwa kuwasiliana nasi.

Tumepokea kama maoni na kuwasilisha idara husika kwa utekelezaji. Asante.^NI
 
Tafadhali angalia "figures" ulizoweka na pia, tunaomba maelezo ya utafauti ili tuweze kukusaidia. Nia yetu ni kukusaidia, mteja wetu. Tunaomba ushirikiano wako.

Asante. ^FL
We utakuwa Sio Mzima.
Inamaana Mimi sijui ninachokisema?????????

Umeme wa Elfu sabini
70,000 nimepewa Unit 19.6

Mita nyingine Umeme wa Elfu sabini nimepewa Unit 19.6

ACHA UBWEGE USIDHANI KILA MTU MJINGA.
 
We utakuwa Sio Mzima.
Inamaana Mimi sijui ninachokisema?????????

Umeme wa Elfu sabini
70,000 nimepewa Unit 19.6

Mita nyingine Umeme wa Elfu sabini nimepewa Unit 19.6

ACHA UBWEGE USIDHANI KILA MTU MJINGA.
Habari, ndugu mteja.

Tunaomba ututumie namba yako ya mita (kwa inbox) au katika jukwa hili tukusaidie kubaini kwanini umepokea unit hizi.

Hii ndo huduma unaitaji tukusaidie nayo?

Asante. ^FL
 
Habari, ndugu mteja.

Tunaomba ututumie namba yako ya mita (kwa inbox) au katika jukwa hili tukusaidie kubaini kwanini umepokea unit hizi.

Hii ndo huduma unaitaji kutusaidie nayo?

Asante. ^FL
Nimeisha Ibiwa.
Nimemuachia Mungu hizo Dhuruma zenu.

Mithali 29:2
“Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua".
 
Nimeisha Ibiwa.
Nimemuachia Mungu hizo Dhuruma zenu.

Mithali 29:2
“Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua".
Habari, ndugu mteja.

Tafadhali tutumie namba yako ya mita kupitia inbox ili tufanye uchunguzi na kubaini sababu za makato hayo ulizoonyesha katika jukwaa hii.

Iwapo itabainika makato hayakua sahihi, kuna utaratibu wa kurejesha uniti. Lengo letu ni kubaini chanzo cha changamoto na kuhakikisha unapata ufumbuzi stahiki.

Ningewashauri tu Msiwe Mnakata Fedha za watu kwenye manunuzi ya Unit za Umeme.

Haiwezekani Umeme wa 70,000 ninapata Unit 19.
Tena Mita Mbili.

ACHENI DHURUMA.
NIMEMALIZA.
 
Tanesco nawashashukuru changamoto yangu imepata ufumbuzi
Karibu sana, mteja wetu na tunaomba usisite kuwasiliana nasi ukipata changamoto nyingine.

Asante. ^HN
 
Back
Top Bottom