Eng Hersi Said Simamia Misingi ya Kanuni na Sheria za Mpira. Mshauri Rais Samia asivuke Mipaka

Eng Hersi Said Simamia Misingi ya Kanuni na Sheria za Mpira. Mshauri Rais Samia asivuke Mipaka

Siyo born town wa msoga wala GSM mwenye ubavu wa kutunishiana misuli na Rais ..kwa bara la Africa Rais ndio kila kitu amna wa kumpinga
 
Rais Samia amesema "ANAOMBA" wakalimalize swala la Feisal, hapendezwi na ugomvi. Hajasema kama kuwalazimisha au kama amri. Ni "OMBI" ametoa ambalo linaweza likakubaliwa au kukataliwa na hao viongozi wa yanga!!!

Kosa lake ni nini hapo? Mipaka gani achunge?
Ombi la rais ni sheria.
 
Ndiyo muelewe kwa nini FIFA inakataza serikali kuingilia mambo ya mpira wa miguu. Mlikata miuno kupewa ndege,mamilioni ya magoli na kualikwa kwenda kufakamia pilau la ikulu. There is no free dinner.
FIFA haikatai pesa za hamasa wala klabu kusafirishwa kwandege za hisani.

FIFA inakataza serikali kuingilia au kuathiri maamuzi ya sokaa.
 
Mtu anatoa ombi halafu anataka na mrejesho wa mtakapofikia kama una akili timamu lazima ujiongeze.

Huyo mpemba akisaini Simba hii dinner watailaani sana waliokuwa wamedhamiria kumkomoa.

Halafu tuhuma zake alizotoa juzi hazitojibiwa tena hivyo kuaminika ni za kweli.
Inashagaza sana.

Ni ujinga ulio pitiliza yaani.
 
🫱🏼‍🫲🏽🫱🏼‍🫲🏽🫱🏼‍🫲🏽🫱🏼‍🫲🏽🫱🏼‍🫲🏽 kuna mijitu mijinga sana muulize gharama ya ndege kwenda Algeria na kurudivna kwenda Mbeya apige hesabu ya nauli ya watu 250×2 Tz -Algeria
Ndio hapo sasa wanakuja kulia lia hapa.
 
Yanga ni waoga Sana Kama FEI Toto hawataki walitakiwa kutangaza Bei ya kumuuza,, lkn wao wamebaki na aje tukae mezani tumalizane au timu inayomtaka iende ikaonanenao??suala Kama Hili halikuhitaji watu wakae mezani wanywe KaHawa.. ilikuwa ni biashara FEI anauzwa ml 500..timu inayomtaka ije ilipe biashara ifanyikeee..ohh turudi mezani.. kuna chakula umeandaa??
 
Mualiko wa ikulu umekua mchunguu, pilau limegeuka boko boko.

Sahivi ndo mnajua serikali haitakiwi kujihusisha na masuala ya soka? Alipokua anatoa ndege ya serikali buree? Na gharama zote zile? Mbna mlikua hamu muambii hilo??

Tulieni dawa iwaingie vizuriii, na ameshasema hivyoo, kinachotakiwa ni utekelezaji tyuuh.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] patamu hapoooo.
Mhhh kwahyo itakuaje sasa na dogo hamtaki herisi saidi
 
Yan
Yanga ni waoga Sana Kama FEI Toto hawataki walitakiwa kutangaza Bei ya kumuuza,, lkn wao wamebaki na aje tukae mezani tumalizane au timu inayomtaka iende ikaonanenao??suala Kama Hili halikuhitaji watu wakae mezani wanywe KaHawa.. ilikuwa ni biashara FEI anauzwa ml 500..timu inayomtaka ije ilipe biashara ifanyikeee..ohh turudi mezani.. kuna chakula umeandaa??
Yanga kiuhalisia hawakua na mpango wa kumuachia dogo walikua wanataka kipaji kipotee na wamchafue dogo. Hayo yote walikua wanaelewa utaratibu mzima na kwann wasikae nae toka sakata limeanza? Yaani bongo bado kwenye mpira tuna kaujing aka kuwekana chini kisa mambo ya ajabu ajabu tu
 
Kwani nani alimuomba atupatie ndege?
Kwani nani alimuomba incentives za magoli?

Hawezi kulaghai taasisi kwa dinner ya Milioni 200.
Yale mabango ya "Asante mama" yaliyojaa uwanjani siku ya fainali kwa mkapa ni ishara ya kwamba mlikuwa mnaunga mkono siasa kwenye michezo, kwasasa mnajifanya kupinga kwasababu limeng'ata upande wenu sio?


Sioni wa kuuendeleza huo mgogoro baada ya hiyo kauli ya Rais, kama kweli Hersi ana huo uwezo unaojaribu kusema hapa, itokee interview yoyote uone kama atalizungumzia swala la FEI kwa ngebe kama zamani.
 
FIFA haikatai pesa za hamasa wala klabu kusafirishwa kwandege za hisani.

FIFA inakataza serikali kuingilia au kuathiri maamuzi ya sokaa
Unahangaika ukiwa wapi?? Kwani hako si maombi tu kunasehem ameforce...ila tupo hpa nyumbani karib mtupe mrejessho...
 

Attachments

  • 20230519_223139.jpg
    20230519_223139.jpg
    1.5 MB · Views: 1
Habari wanajamvi.

Leo amesikika Rais wa Tanzania Akimdadavulia Rais wa Yanga SC Bw Eng Hersi Said kwa lengo la
kumuhimiza ahakikishe Mchezaji Feisal Salum anapata haki yake.

Ninacho fahamu kuwa Mama Samia hana ufahamu sahihi wa kinacho endelea baina ya mgogoro uliopo kati ya Yanga SC na Mchezaji husika. Hisia zake kama Mzanzibar ndizo zimempelekea kusukumwa kutoa mapendekezo yake pasi na kuhitaji kulifahamu zaidi swala hilo.

Ndugu Hersi Said, unapaswa kucheza karata zako makini mno kwenye hilo. Kumbuka Mama Samia ametumia gharama kiduchu sana kwenye kampeni ya zawadi za kila goli, Dinner la Ikulu pampja na usafiri wa ndege. Kumbuka hajafanya haya si kwa mapenzi ya dhati na masuala ya michezo, bali alilenga zaidi kuilaghai taasisi ya michezo ili iache kusimamia misingi ya kisheria na kikanuni ya michezo.

Kwa kawaida, ni muhimu kwa Rais wa nchi kuzingatia majukumu yake kikatiba na kutofautisha majukumu ya mamlaka nyingine za kiserikali na taasisi mbalimbali. Mgogoro kati ya klabu na mchezaji ni suala la kisheria ambalo linapaswa kusuluhishwa na mamlaka husika za sheria na kanuni za michezo.

Rais Samia Anahitaji Elimu zaidi.

Kwa hiyo Rais wa nchi kuingilia kati ktk mgogoro kama huo unaweza kusababisha mchanganyiko wa majukumu na kuingilia uhuru wa mamlaka nyingine. Ni muhimu kwamba kila mamlaka ifanye kazi yake. Kitendo cha Rais kuwapa Incentives mbalimbali basi isiwe sababu ya kuhalalisha kuingiliana ki mamlaka katika mihimili inayo jitegemea kiutendaji.

Rais Samia anahitaji mrejesho, Basi ni wasaa sahihi kuhakikisha anaandikiwa mrejesho wa kumuelimisha kuwa masuala ya migogoro ya kisoka/kimpira yana namna yake ya kutatuliwa. Muelewesheni kuwa zipo sababu za msingi kwanini hili suala linakawia kufikiwa tamati.

Ni vyema akafahamu kuwa uvunjwaji wa taratibu na mchezaji yeyote wa klabu ni lazima kuadhibiwe pasi na kujali kama huyu ni mchezaji wa kizanzibar, wa bara au wa kimataifa. Na hukumu kwa mchezaji wa namna hiyo hautotokwa kwa upendelea wa kibusara eti kwa kisingizio kuwa mchezaji ni mzawa au la.

Mshaurini Rais kuwa licha ya kuyafurahia mafanikio haya madogo ya klabu, kuna watu nyuma ya pazia ambao wanawekeza pesa zao na wasingependa kuona wanapata hasara ktk biashara ya mauzo ya wachezaji. Tukiruhusu kuingilia maamuzi ya taasisi huru ambazo zina sheria zake za usuluhishi basi tunajiweka katika nafasi ya kuwafukuza wawekezaji aina ya wakina GSM na Mo Dewji katika mpira wa Tanzania.

Kuna madhara makubwa sana endapo klabu kama klabu itashindwa kusimamia misingi ya taratibu zake na kusuluhisha migogoro na kesi za kimpira kwa kutumia tu mapendekezo ya wana siasa. Je Mama Samia anatoa ushauri kama nani? Je ni kama mtu mwenye ufahamu wa kanuni na taratibu za uendeshaji wa mpira? au Kama

Sasa endelea kubishana na Mamlaka ya nchi. Maana wabongo huwa mnaubishi wa ujuaji mwingi.

Sio kila misingi ni lazima isimamiwe, ndio maana umepewa brain......thinking na busara ni muhimu.

Rais ametoa MAELEKEZO, hupaswi kujadili maagizo ya Rais, Bali anatakiwa kutafuta njia bora ya kuyatekeleza in mutual understanding.

Otherwise, aendele kupuuza na kubaki kwenye misingi yake.
 
Ukila vya mbwa uwe na mbio kama huna mbio utaliwa tuu, huyo jamaa hana pa kutokea kwenye hilo lazima afuate maelekezo, yule dogo anarudi utopoloni
 
Hili liwe fundisho kwa mawakala wa wachezaji.
Lazima kuwa na kipengele katika mkataba kinachoonesha.

1. Timu ikitaka kuvunja mkataba wa mchezaji muda wowote ifate kanuni gani.

Kuna wakati mchezaji anabadilikia kutabia au anaisaliti timu na anatakiwa kuachwa lazima kuwa na kipengele cha namna ya kumwacha.

.

Ko wachezaji wote hivi sasa kwenye mikataba yao wawe nakipengele hiko ili wakiona hawataki kuendelea na klabu zao basi wabadilishe TABIA au WAISALITI timu ili waachiwe huru kirahisi..?


[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Na umshauri aache kuomba eneo la uwanja pale jangwani ,akanunue eneo Kama Simba walivyonunua Bunju
 
Sasa endelea kubishana na Mamlaka ya nchi. Maana wabongo huwa mnaubishi wa ujuaji mwingi.

Sio kila misingi ni lazima isimamiwe, ndio maana umepewa brain......thinking na busara ni muhimu.

Rais ametoa MAELEKEZO, hupaswi kujadili maagizo ya Rais, Bali anatakiwa kutafuta njia bora ya kuyatekeleza in mutual understanding.

Otherwise, aendele kupuuza na kubaki kwenye misingi yake.
Achana nao mkuu GSM akiambiwa achague kati ya biashara zake na Fei toto unafikiri atachagua nini?
 
Usiseme; "Rais hana ufahamu wa kinachoendelea baina ya mgogoro uliopo kati ya Yanga na Faisal"

Rais ni taasisi,anapata information zote,mpaka kufikia kuliongelea hilo,ujue anazo info zote.
 
Back
Top Bottom