Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng: Rogatus Mativila akitoa taarifa fupi ya mradi huo amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) ilitenga fedha kwa ajili ya kuboresha Barabara hiyo ikiwa ni sehemu ya Mkakati wa Serikali wa kuboresha mtandao wa Barabara nchini pamoja na kupendezesha miji yetu.
Amesema Ujenzi wa barabara hiyo umegawanyika katika Sehemu tano, Mianzini – Olemringaringa – Ngaramtoni Juu- km 12.24, Olemringaringa – Timbolo – km 2.95, Ngaramtoni Juu – Selian – km 2.15, Ngaramtoni Juu – Sokoni – km 0.52 na Barabara ya kwenda Hospitali ya Selian – km 0.18, ambapo Mradi huo wa barabara unatekelezwa na Kampuni ya STECOL Corporation ya China kwa gharama ya Shillingi Billioni 22.225 na kwamba kulingana na mkataba mradi unatakiwa kukamilika tarehe 19 Agosti 2023.
Aidha Mradi huo unahusisha ujenzi wa daraja moja kubwa kwenye mto Lekasayo lenye urefu wa mita 13, makalavati makubwa (Box Culverts) 8, makalvati madogo 45 yatajengwa pia barabara hiyo itawekwa taa za barabarani kwenye maeneo ya makazi ya watu.