robert sendabishaka
JF-Expert Member
- Dec 11, 2015
- 3,111
- 3,294
Lakini kwenye gemu waliotunukiwa medali ikibainika kulikuwa na 'namna' wananyang'anywa/vuliwa.Huyu dogo katupiga za chembe kaka... refa naye kakimbilia kuhesa hadi 10 kabla hatujaanguka...game kaputi....
Kilichotakiwa kufanyika:
Ingesubiriwa ripoti maalumu ya jopo la wachunguzi wa masuala ya ndege waliotoka kwa watengenezaji. Wakishapata taarifa za chanzo cha ajali na mawasiliano ya rubani na mamlaka; kama zilivyonaswa na Black box ndio tuje na concrete conclusion tuwatambue wote walioshiriki kuokoa na kuopoa, wa kupewa tuzo/mafunzo, wa kuorodheshwa miongoni mwa mashujaa wa taifa watambuliwe na waliolala mauti wapewe heshima/fidia inayostahili kama wale wa mv. Bukoba. Lakini KUBWA zaidi watakaobainika kuchangia uzembe pia wawajibishwe.
Naamini ripoti ya mtengeneza ndege haiwezi kuchakachuliwa wala kufumbia macho makandokando ya ndani ili kulinda hadhi na jina la biashara zao.
Shida kubwa katika ulimwengu wa tatu ni utovu wa uwajibikaji. Kiongozi yuko tayari aunde zengwe na filamu kwa gharama yoyote ili tu kukwepa uwajibikaji tofauti na wenzetu ulimwengu wa kwanza kashfa moja tu inatosha kumuondoa kwenye nafasi yake.
Mpaka sasa hadithi zimekuwa nyingi utadhani ajali ilitokea usiku wa giza hadi imekuwa kitendawili kubaini Walioshiriki kuvunja mlango na kuwezesha uokozi/uopoaji. Je, ni Majaliwa? Wahudumu? Mhandisi? Kesho tunaweza kutajiwa kikosi cha zimamoto[emoji2960]
Japo hizi ngonjera hazisaidii kurejesha uhai na hasara iliyotokea lakini kwa faida ya kuweka rekodi sawa basi tupate picha sahihi ya pamoja.