Eng Victor: Namshukuru Mungu kwa Ujasiri alionipa wa kujiokoa na kuokoa wengine kwenye Ndege, naelekea Muhimbili kwa matibabu zaidi

Huyu dogo katupiga za chembe kaka... refa naye kakimbilia kuhesa hadi 10 kabla hatujaanguka...game kaputi....
Lakini kwenye gemu waliotunukiwa medali ikibainika kulikuwa na 'namna' wananyang'anywa/vuliwa.

Kilichotakiwa kufanyika:
Ingesubiriwa ripoti maalumu ya jopo la wachunguzi wa masuala ya ndege waliotoka kwa watengenezaji. Wakishapata taarifa za chanzo cha ajali na mawasiliano ya rubani na mamlaka; kama zilivyonaswa na Black box ndio tuje na concrete conclusion tuwatambue wote walioshiriki kuokoa na kuopoa, wa kupewa tuzo/mafunzo, wa kuorodheshwa miongoni mwa mashujaa wa taifa watambuliwe na waliolala mauti wapewe heshima/fidia inayostahili kama wale wa mv. Bukoba. Lakini KUBWA zaidi watakaobainika kuchangia uzembe pia wawajibishwe.

Naamini ripoti ya mtengeneza ndege haiwezi kuchakachuliwa wala kufumbia macho makandokando ya ndani ili kulinda hadhi na jina la biashara zao.

Shida kubwa katika ulimwengu wa tatu ni utovu wa uwajibikaji. Kiongozi yuko tayari aunde zengwe na filamu kwa gharama yoyote ili tu kukwepa uwajibikaji tofauti na wenzetu ulimwengu wa kwanza kashfa moja tu inatosha kumuondoa kwenye nafasi yake.

Mpaka sasa hadithi zimekuwa nyingi utadhani ajali ilitokea usiku wa giza hadi imekuwa kitendawili kubaini Walioshiriki kuvunja mlango na kuwezesha uokozi/uopoaji. Je, ni Majaliwa? Wahudumu? Mhandisi? Kesho tunaweza kutajiwa kikosi cha zimamoto[emoji2960]

Japo hizi ngonjera hazisaidii kurejesha uhai na hasara iliyotokea lakini kwa faida ya kuweka rekodi sawa basi tupate picha sahihi ya pamoja.
 
Victor, umetupa habari na somo jema; nakushauri uendelee na matibabu utuache tuendelee kumpongeza huyo aliyeteuliwa kuwa Game/strory changer
 
Huyu jamaa ni muongo hydraulic system haiwezi fanya kazi bila umeme kama engine ya ndege ilikua off mlango hauwezi kufunguka bila kugongwa na kitu kizito kama alikua na nyundo ndani hapo sawa au kama baada ya clash mlango ukafunguka wenyewe nitamuelewa
 
Millard ayo wamemuhoji mchina anasema yey ndo alimuokoa mtoto,kwan kulikua na watoto wangap kweny ndege.Mchina anashukuru wavuvi ila watz tunaona ni waongo[emoji23][emoji23][emoji23].Anasema kwa nje kulikua na watu wanahangaika kufungua mlango though na wao ndan hawakubaki nyuma.AIR HOSTESS WAHOJIWE PIA
 
Majaliwa alipewa stahiki yake katika wakati sahihi,kusubiri ripoti ambazo sometimes huwa zinakuwa doctored ku-cure some ineffieciencies nadhani haingekuwa fair kwa Majaliwa,kumbuka RAHA YA SUPU UINYWE IKIWA YA MOTO
 
Victor, umetupa habari na somo jema; nakushauri uendelee na matibabu utuache tuendelee kumpongeza huyo aliyeteuliwa kuwa Game/strory changer
Jamaa ni Engineer mzuri sana, majengo mengi unayoona Dar na picha zikisambaa kwa hapa ni Dar kasimamia yeye,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…