Eng Victor: Namshukuru Mungu kwa Ujasiri alionipa wa kujiokoa na kuokoa wengine kwenye Ndege, naelekea Muhimbili kwa matibabu zaidi

Eng Victor: Namshukuru Mungu kwa Ujasiri alionipa wa kujiokoa na kuokoa wengine kwenye Ndege, naelekea Muhimbili kwa matibabu zaidi

Dakika au Sekunde ?, Si angeweka kitu kama Kasia au mikono yake haikuchoka ?

Unajua dakika 60 ni saa nzima ? Kwahio yeye katika Uokozi huu alishiriki kushikilia mlango ?

Hii kitu tangia itokee inaleta maswali mengi kuliko majibu na huenda ukweli mwisho wa siku ukawa ni wa version kama tano au sita hivi....
Dakika siyo sekunde

Ndio sababu Wavuvi walistaajabu kwa sababu alitumia mkono mmoja Kuokoa watu
 
Aaah kijana amekua exaggerated ila waliosaidia ni wengi mnoo kuanzia Hostess aliyefungua emergency exit, raia wa china, wavuvi waliokuja na mitumbwi all in all Majaliwa sio kama alikua better ila kitendo Cha yeye manusura kupoteza maisha sababu ya kujaribu kumuokoa Rubani nadhani ndio wanamfutia machozi nacho.

Pia serikali wamemkuza Ili kuondoa maswali ya wananchi kwenye uzembe wa kuchelewa kuokoa Ili Sasa attention iwe kwenye SHUJAA!! but ukisikiliza manusura wote utaona msaada ulitolewa na watu wengi sana na sio mtu mmoja kuokoa watu 24!!
Tatizo wanasiasa wamechukua majaliwa Kama mwamvuli wa kufichia ule uzembe wao ambao walipaswa kuwajibika
 
Dakika au Sekunde ?, Si angeweka kitu kama Kasia au mikono yake haikuchoka ?

Unajua dakika 60 ni saa nzima ? Kwahio yeye katika Uokozi huu alishiriki kushikilia mlango ?

Hii kitu tangia itokee inaleta maswali mengi kuliko majibu na huenda ukweli mwisho wa siku ukawa ni wa version kama tano au sita hivi....
Aliye quote naye kapotosha jamaa alishika mlango kwa mkono ila ulipewa balance na mtumbwi so yeye alishika tu wakati wengine wanaokoa watu ila sio kwamba aliweka mguu more so dakika zote 60!! Hizi media zetu Nazo ni tatizo.
 
Victor kasema Hata yule mtoto mdogo alimuokoa kwa kumshika na kidole

Ndio sababu anamtukuza Mungu
 
Kweli Riziki yoyote lazima Nongwa ihusike Wallah....

Majaliwa ndiyo huyo...Aliyepewa amepewa tu...
Mama ukitulia vizuri wanao hoji wana hoja.
Na kama unaifaham hiyo ATR utakubaliana na hoja za wanao hoji.

Mlango wa ndege hii kamwe huwezi kuufungua kwa kwa kuupiga kumbika huwa unafunguka kuja chini na kugeuka kuwa ngazi.
Lazima ufunguliwe kutoka ndani tena kwa kusukumwa
 
Back
Top Bottom